Nimekataa kumpongeza Mrisho Gambo

Nimekataa kumpongeza Mrisho Gambo

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
“TUNATAKA kuona taifa hili likiwa na vijana jeuri na wenye kujiamini, wasiwe vijana waoga aina ya ‘ndiyo’ bwana, mkubwa; vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya Kitanzania. Tunataka vijana wenye misimamo thabiti dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika taifa,”

Haya ni maneno aliyopata kuyanena, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Siku moja wakati nasoma Biblia nilikutana na ujumbe wa Mwanzo 45:5, ulisema “Yusufu akawaambia kaka zake, ingawa ninyi mliniuza ila Mungu alikusudia kunitanguliza ili niwasaidie”

Maendeleo ama mabadiliko katika nchi yoyote yanaletwa pale kunapokuwapo na watu walio tayari kuishi maisha ya kujitoa, watu ambao wanaamini kuwa wanao wajibu mkubwa kwa jamii yao.

gambo.JPG


Kimsingi mimi simfahamu sana na sina maelezo mengi kuhusu mtu niliyeamua kumzungumza leo mwenye jina la MRISHO MASHAKA GAMBO, maana yeye akiwa kwenye Umoja wa Vijana wa CCM kama mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM 2008 – 2012 kutoka Mkoa wa Arusha, mimi nilikuwa BAVICHA, wakati mimi nikijiunga na UVCCM na CCM mwaka 2013 mwanzoni yeye alikuwa ameshateuliwa kuwa DC wa Korogwe (akiwa DC wa Kwanza kwa wakati huo kubeba matofali na kushiriki kujenga shule na zahanati na Wananchi). Hivyo ni mtu ambaye nimekuta maneno yaliyovumisha sifa yake lakini sikupata bahati ya kumfahamu vizuri.

Lakini maneno niliyoyakuta ambayo yanamuelezea GAMBO yalishabihiana sana na maneno ya Mwalimu niliyoyanukuu, kuwa GAMBO ni Kijana JEURI, JASIRI na ANAYEJIAMINI.

Nimeambiwa katika historia ya maisha yake, halijawahi kutumika neno la MUOGA, kumuelezea juu ya wajihi wake na sifa yake…wala yeye mwenyewe hajawahi kusikika katika maisha yake akitamka neno NAOGOPA, ni Kijana anayehoji kwa HOJA.

Lakini hayo ni tisa, Kumi Mrisho Gambo ni Icon kamili ya Mwanamapinduzi anayechukia mifumo kandamizi, mifumo ya Ubwana na UFISADI. Historia yake inatueleza hivyo, alimkataa Mhe Lowassa ingawa alikuwa anatoka nae Mkoa mmoja tangu akiwa UVCCM kwa sababu moja kuu UFISADI.

Kwenye title ya andiko langu nimesema nimekataa kumpongeza Gambo, ni kweli nimekataa..!! Maana sio kwa juhudi za Mrisho pekee ndizo zilizomfikisha hapo bali malezi mazuri yanayotolewa na CCM na UVCCM kwa vijana wake ndio yaliyofanikisha kuwapata Mawaziri kama akina Makamba, Mavunde, Masauni na wengineo, ni mazao ya UVCCM yaliyotuletea wakuu wa Mikoa mahiri kama akina Makonda, Gambo, Mtaka na wengineo pamoja nao Ma-DC katika maeneo mbalimbali ya Nchi yetu. Kwa malezi haya nimeamua kuipongeza UVCCM na CCM na kukataa kumpongeza GAMBO.

Ni CCM pekee inayojenga Vijana majasiri wanaoweza kuwahoji Viongozi wao hadharani, katika historia yake GAMBO alipishana mawazo na kuhoji hadharani juu ya Lowassa, alihojiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na wakubwa wengine pale alipoona wanaenda kinyume na matakwa na matarajio ya jamii yetu, Jamii yetu ina kiu ya Maendeleo, Kiongozi yeyote anayekwamisha maendeleo katika eneo ambalo GAMBO yupo basi huyo amejitangazia Vita na Uadui mkubwa na Kijana huyu. Daima alitaka kuona haki ikitendeka na wananchi wanahudumiwa. Hata hivi karibuni Yule jamaa wa M4C wa Arusha Mjini alipotaka kupima ubavu, alijikuta kadondokewa na kitu kizito chenye ncha kali (maana sasa hivi Serikali imepiga marufuku zile posho zao za kifisadi) Ni CCM na UVCCM sio CHADEMA, sio BAVICHA wenye uwezo wa kutoa Vijana makini na wasio waoga na mabwana ndio Mzee. Wao ni Vijana wa kusubiri maelekezo na kutumwa kubweka.

Mungu amemchagua na kumuinua GAMBO, akamtenga mbali na dhulma na wafitini. Ni kama ilivyo kwa Yusuph, MUNGU ameamua kumtanguliza Gambo ili awasaidie. Mkoa wa Arusha unakufa, biashara zimesimama, utalii unadorora, mahoteli yanafungwa kwa sababu za kipuuzu na upuuzi wa mtu mmoja na kijikikundi chake, MUNGU amemuinua GAMBO ili awasaidie kuirudisha heshima ya ARUSHA.

Nimekataa kumpongeza GAMBO lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru na kumpongeza Mhe John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwapa nafasi, hakika mimi nachukua ahadi kwako kwa niaba yao kuwa HATUTOKUANGUSHA.
 
... Kimsingi mimi simfahamu sana na sina maelezo mengi
... Mrisho Gambo ni Icon kamili ya Mwanamapinduzi anayechukia mifumo kandamizi, mifumo ya Ubwana na UFISADI.
...Mungu amemchagua na kumuinua GAMBO, akamtenga mbali na dhulma na wafitini.
Yaani mwenye sifa zote ulizomwaga hapo ni mtu unayekiri kuwa haumfahamu! Naomba basi unielekeze kitabu kinachomuhusu kinaitwaje ili na mimi nimfahamu kupitia historia yake!
 
CCM bwaaaaaana LOWASA tu ndio fisadi kwao hapa tu ndio uwa nashindwa kuwaamini kabisa na sitaweza kuja kupiga kura kwa mtu yoyote wa CCM wala sitaweza kuja kujitolea kwa kitu chochote kwa CCM mana ntakuwa nafanya unafiki na mimi sio mnafiki majizi yamejaaa uko kama yule wa bariadi, wale wa ESCROW, chenji ya radar, nyumba za serikali, lugumi at least wangekuwa wanayataja na mengine kama wanavyomtaja LOWASA ningekuwa na imani ila wao fisadi lowasa wakati kuna wakina lowasa umo na zaidi ya lowasa kibao.
 
Mbona hueleweki? Kwenye uzi wako umemsifia sana GAMBO kuliko hata hao UVCCM wako na CCM kwa ujumla! Unapotoa heading basi weka na mada inayoendana nayo.

Unajifanya kutuvuta kusoma uzi wako huku imejaa umbummbu tu.
 
Juiana Shonza umezita posho za madiwani wa Jiji la Arusha kuwa ni za kifisadi na umeonekana kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuzifuta.

Sasa nikuulize wewe unaepokea sitting allowance pale Bungeni unajiona ndio uko sahihi?

Wewe unaelipwa perdiem na sitting allowance juu,unapata wapi uhalali/ujasiri wa kuita posho ya hao madiwani kuwa ni ya kifisadi?!

Kama kwei unaguswa na posho za aina hii,umewahi hata kupeleka hoja binafsi Bungeni kupendekeza sitting allowance za wabunge kufutwa?!

Tuache unafiki,kwenye swala la posho wote mko pamoja CCM na wapinzani na bora hata wapinzani wakati mwingine huwa wana-sacrifice posho zao wanapoamua kupinga baadhi ya mambo kama vile waliyofanya kwenye Bunge la Katiba na hivi majuzi walipokuwa wanatoka nje kumpinga Naibu Spika bila kujali kuwa wanakosa posho.

Angeongea mh. Elibariki Kingu aliepinga posho hii na mkashindwa kumuunga mkono nimengemuelewa lakini kamwe sio wewe au mbunge mwingine yoyote maana ni Kingu pekee ndie aliethubutu kuandika Barua kutaka asilipwe hiyo posho ingawa sijui issue yenyewe iliishaje.

Kuhusu Zitto nae sijui kama aliandika Barua au aliishi kutamka tu mimi sijui ila najua nae aliwahi pinga hii posho na hakuungwa mkono.

Acheni kutufanya watanzania wajinga!

Inakera sana!
 
Ni kweli Juliana Shonza

Humfahamu Mrisho Gambo,na nashangaa unatowaje sifa kwa mtu usiyemfahamu.Mrisho kweli ni jeuri,ana kiburi na matusi ya nguoni.Hata wewe ukikaa vibaya lazima akutukanie hata mzazi wako.

Ingekuwa vema ungekaa kimya kuliko kujipendekeza wakati humjui Gambo.Wewe unayejiita mwanamke mpambanaji inabidi ujipambambanue,maana wanawake wenzako alikopita Gambo kama kiongozi wamedharirishwa sana,kuanzia Korogwe mpaka Uvinza.

Nilidhani utamuonyaa aachane na tabia za matusi....Hapa chini ni ushahidi wa wanawake wenzake,wenye kuzunguka round about kila mwezi walivyoshuhudia tabia mbovu za huyo unayemsifia.


"Mhe. Gambo analalamikiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Matumizi mabaya ya uongozi yakiwemo matumizi ya lugha chafu, kukiuka sheria mbalimbali pamoja na ubabe wakati wa kutekeleza majukumu yake kama Mkuu wa Wilaya ya Korogwe

Pia Shahidi huyo alidai kuwa Mkuu huyo wa Wilaya aliwahi kumtukana hadharani matusi ya nguoni Mtumishi mmoja wa kike wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ambaye alikuwa ni Mwanasheria wa Halmashauri hiyo na kupelekea mtumishi huyo kufungua kesi Mahakamani dhidi ya Mkuu huyo wa Wilaya, kesi ambayo alidai bado inaendelea mpaka sasa

Kwa mujibu wa Mhandisi Mwahalende, katika kipindi hicho utendaji wa Mkuu huyo wa Wilaya haukuwa mzuri kwa mambo ambayo yeye mwenyewe ameshuhudia ambayo ni pamoja na lugha chafu ambayo haistahili kuzungumzwa na Kiongozi, Utawala wa mabavu na amekuwa ni kikwazo cha maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwa kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo"
 
Mnafiki saan huyu dada,eti anjiita Mlokole.Ukishaingia kwenye siasa za ulaghai na chuki pamoja na ufitini kama za CCM huwezi kujigamba kwa ulokole.

Ilikuwa ni kuchagua moja,utajili katka roho au fahari ya maisha katika mwili.Umechagua lililo moja na hakika huko ndio mahali pako.
 
Huyu Mwana Mama Juliana Shonza anaongelea vi UVCCM vijambaza ambayo takribani wiki imepita vinashutumiana kwa Wivi wa mali zao wenyewe kwa wenyewe ?????
 
Achaneni na Juliana,huyo hawezi kujenga hoja. Anaandikiwa ndipo anaipost huku jukwaani. Sijawahi kumsikia hata akitoa hoja bungeni.

Huku anaandikiwa kisha kuanzisha uzi wake wa ajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom