Nimekata tamaa, moyo wangu unavuja damu

Nimekata tamaa, moyo wangu unavuja damu

ibra87

R I P
Joined
Jul 22, 2015
Posts
5,614
Reaction score
5,379
Wasalaam

Wakuu na wanajukwaa wote.

Nimekaa nyumbani nikiwa nimekosa raha kabisaa. Nimeumia na kuumia sana, sina furaha tena katika maisha yangu kuanzia leo. Mwanamke niliyewahi kumpenda na kuishi naye kwa miaka miwili akaja kuondoka Tanzania akaniaga kuwa anakwenda kusoma Saudi arabia leo nimeliona jina lake kwenye gazeti akiwa ni mmoja wa wanawake waliohukumiwa gerezani miaka tisa kwa kujihusisha na Biashara ya madawa ya kulevya.

Imeniuma na kunichanganya Sana, natamani kumuona, natamani japo niongee nae. Natamani kumuuliza inakuwaje lakini nashindwa pa kuanzia. Nini kilikusibu Shadia mpaka ujiingize Huko? Hayo ndio masomo kweli?

Nimekosa furaha, nimepoteza furaha na sijui kama nitakuwa na furaha kwa kipindi hiki.

Nisamehe Mpenzi wangu huu ndio ukweli.

MOYO WANGU UMEUMIA KUPITA KIASI
 
Mkuu hebu achana na majuto hayo. Maisha lazima yaendelee, we shukuru Mungu kakuepusha na Punda hilo aisee.

Acha kunung'unika, hakuwa stahiki yako huyo, achana nae
 
Mkuu hebu achana na majuto hayo. Maisha lazima yaendelee, we shukuru Mungu kakuepusha na Punda hilo aisee.

Acha kunung'unika, hakuwa stahiki yako huyo, achana nae

sikuwahi kuwaza wala kuzania hili, nimeshtuka na kufadhaika sana
 
Duu pole mno mno....i know how you feel pal
 
Mwenzio boss wa temeke wewe unaleta mambo ya kidosi. Angelirudi na mahela ndio ungeumia zaidi. Pumbavu tena lofa kabisa
 
Ajinyonge tu mleta mada maana hamna jinsi!!!!
Saudia arabia wanasomea usharif na makombe majin au kozi gani???

A na B yote ni majibu unaweza kuchagua moja
 
Pole sana. Dunia ina majaribu mengi na anasa za dunia zinapeleka wengi magerezani na wengine kupatwa na mauti. Utajiri wa haraka haraka bila kufanya kazi na kuiga maisha ya watu ndio tamaa zinapokuwa mbele.
Pamoja na kumpenda sana, Mshukuru Mungu huwezi jua wewe pia angekuingiza huko ma leo mngekuwa wote gerezani.
Maisha lazima yaendelee.
 
dah! mkuu ulinitisha nikajua atoto ndo kahukumiwa jela miaka 9 kumbe mwingine
 
Oya ibra huyo demu hapo juu vipi mna ugomvi kwani
 
Pole sana. Dunia ina majaribu mengi na anasa za dunia zinapeleka wengi magerezani na wengine kupatwa na mauti. Utajiri wa haraka haraka bila kufanya kazi na kuiga maisha ya watu ndio tamaa zinapokuwa mbele.
Pamoja na kumpenda sana, Mshukuru Mungu huwezi jua wewe pia angekuingiza huko ma leo mngekuwa wote gerezani.
Maisha lazima yaendelee.

yeah maisha yanaendelea mkuu lakini hili tukio sikuwahi kuligundua hapo kabla
 
Back
Top Bottom