Nimejisikia uchungu mkubwa, sababu nafahamu historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Arusha

Ni bahati mbaya siku zote watu ambao hawajiamini wanatumia nguvu kubwa ya vyombo vya dola
Eti Magufuli anapenda watumishi wanaopenda kukwaruzana na wapinzani ndiyo furahaa yake.unaenda kuzindua mradi unabeba Silaha za kivita utafikiri tuko Sudan kusini.kama anajiamini bila kutegemea polisi angeenda Ana kwa Ana siyo kujificha kwenye koti la polisi eti ulinzi na usalama
 
Hakuna siku nimejisikia uchungu mkubwa kama jana, kwasababu nafahamu historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto, na nimeshiriki katika hatua mbalimbali za ujenzi wa maono haya. Lema alikuwa na ndoto hii kwa muda mrefu, na aliitangaza hadharani katika kampeni zake na CCM walimdharau na kumuona kichaa, na wakati mwingine Lema alikuwa akisema, CCM wakiendelea kumuudhi na kumkejeli na ndoto hiyo, ataijenga hiyo hospitali na ataiwekea na swimming pool mithili ya hotel. Muda ukafika Lema kupitia ushawishi wake na timu yake wakafanikiwa kupewa kiwanja na Mawala Trust, na siku ya makabidhiano nilikuwepo, na hakukuwepo kiongozi yoyote wa Serikali, Mgeni rasmi alikuwa Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema. Hii inaonesha wazi kabisa Mawala si tu walikuwa na moyo wa kusaidia watu wa Arusha kupata Hospitali ya kusaidia akina mama na watoto, pia walionesha mapenzi ya wazi kwa Chadema, kwa kukabidhi kiwanja hicho chini ya Ugeni Rasmi wa Mwenyekiti wa Chadema taifa. hatua iliyofuata ilikuwa ni kutafuta udhamini wa ujenzi wa Hospitali hiyo kitu ambacho watu wa Arusha tulisema hata kwa michango binafsi tutaweza kuchangia ujenzi wa hospital hiyo, lakini Mh. Mbunge kwa ushirikiano na taasisi yake ya Arusha development Foundation (ArDF) waliendelea kutafuta wahisani hadi walipokutana na watu wa Maternity Afrika ambao waliingia nao mkataba wa kujenga Hospital hiyo kwa thamani ya Bilioni 9 za Kitanzania. hatua ya aibu ni ya leo ambayo huyu anayejiita mkuu wa mkoa kutaka kwa makusudi kuharibi kazi nzuri iliyofanywa kwa miaka mingi bila msaada wowote wa serikali, kisa ameitwa tu kuiwakilisha serikali kama mgeni rasmi, tena Lema akiwa hana shida yoyote ya uwepo wake. Aina hii ya viongozi hawawezi kutufikisha kwenye nchi ya viwanda anayosema Magufuli. Wamejaa ujinga wa kichama na wanafikiria muda wote ni muda wa kufanya siasa na kutweza kazi nzuri zinazofanywa na wapinzani. I find this to be the highest level of stupidity I have ever seen in a leader. It is so sad indeed. Vielelezo vya picha vipo hapo, na katika hatua zote hizi muhimu hajawahi kuwepo kiongozi wa serikali hii ya CCM, hadi Leo ndo wanajitokeza na maelezo yao binafsi yasiyo na mkia wala kichwa.
View attachment 420619 View attachment 420622
Moderator badilisheni siyo tetesi hali halisi.

Bible quotes
John 8.32
The Truth will Set You Free
31So He said to the Jews who had believed Him, “If you continue in My word, you are truly My disciples. 32 Then you will know the truth, and the truth will set you free.”

Baada ya kuona haya jana nilipitia historia ya mradi nimesoma comments nyingi kwenye Facebook page ya Mkuu wa MKoa na Pili nimesoma comment za watu huku JF na pili nilimsikiliza na Lema pia.Ila cha msingi naweza sema hekima ni kitu kikubwa sana hata Mfalme suleimani aliomba hekima ili aweze kuwatumikia watu.Kilichotokea jana ni aibu kwa sisi wananchi.Tutumie busara kufanya mambo yenye manufaa kwa jamii lastly Ukweli utatuweka huru.Siasa zikae pembeni kwenye maslahi ya nchi.
 
Pamoja na kuwa alichokifanya Lema si Busara lakini hata yule mwingine kafanya upuuzi wa hali ya juu. Siasa za ajabu ajabu tuu, sijui tutafika wapi!
 
Bible quotes
John 8.32
The Truth will Set You Free
31So He said to the Jews who had believed Him, “If you continue in My word, you are truly My disciples. 32 Then you will know the truth, and the truth will set you free.”

Baada ya kuona haya jana nilipitia historia ya mradi nimesoma comments nyingi kwenye Facebook page ya Mkuu wa MKoa na Pili nimesoma comment za watu huku JF na pili nilimsikiliza na Lema pia.Ila cha msingi naweza sema hekima ni kitu kikubwa sana hata Mfalme suleimani aliomba hekima ili aweze kuwatumikia watu.Kilichotokea jana ni aibu kwa sisi wananchi.Tutumie busara kufanya mambo yenye manufaa kwa jamii lastly Ukweli utatuweka huru.Siasa zikae pembeni kwenye maslahi ya nchi.
Uko sahihi mkuu siasa zinatakiwa kuwekwa pembeni kwa mambo yenye maslahi kwa wananchi kwa taifa kwa ujumla.
 
Hospitali tu imekutia uchungu kiasi hichi, je waliopigania uhuru uhuru ambao leo hawatajwi unafikiri wanajisikiaje na familia zao. Mzee Mohamed Said alisema uchungu wa watu waliopigania uhuru na kishwakuachwa katika historia mkasema mbaguzi, leo ka hospital tena hujatoa hata shilingi yako umejifanya mtu katu mnapiga kelele namna hii, achene unafiki. rudisheni uzi wa Mohamed Said kuhusu historia ya kweli ya Tanganyika halafumje na vi ishu vyenu vya kitoto ili vipate back up kutoka kwa ishu kubwa!
 
Huyu RC ana maono finyu anadhani anaweza kuwadanganya wanaArusha kuwa ujenzi huo ni juhudi za serikali hii ambayo haiwezi kununua hata dawa kwa hospital zake
Tatizo lake na maRC wengi ni kufanya kazi kwa kutaka kumfurahisha Mtawala,hawajui lingine lolote
Gambo ni janga
Huyu hafai tena kuendelea kuwa kiongozi.
 
Hospitali tu imekutia uchungu kiasi hichi, je waliopigania uhuru uhuru ambao leo hawatajwi unafikiri wanajisikiaje na familia zao. Mzee Mohamed Said alisema uchungu wa watu waliopigania uhuru na kishwakuachwa katika historia mkasema mbaguzi, leo ka hospital tena hujatoa hata shilingi yako umejifanya mtu katu mnapiga kelele namna hii, achene unafiki. rudisheni uzi wa Mohamed Said kuhusu historia ya kweli ya Tanganyika halafumje na vi ishu vyenu vya kitoto ili vipate back up kutoka kwa ishu kubwa!
Uzuri wewe ni mwanamama, ingekuwa vema ukaenda kliniki...........
Siwezi kuwalaumu sana maana uwezo wenu wa kufikiri ndo umeishia hapo mtakuwa na utapiamlo wa akili!
 
Hospitali tu imekutia uchungu kiasi hichi, je waliopigania uhuru uhuru ambao leo hawatajwi unafikiri wanajisikiaje na familia zao. Mzee Mohamed Said alisema uchungu wa watu waliopigania uhuru na kishwakuachwa katika historia mkasema mbaguzi, leo ka hospital tena hujatoa hata shilingi yako umejifanya mtu katu mnapiga kelele namna hii, achene unafiki. rudisheni uzi wa Mohamed Said kuhusu historia ya kweli ya Tanganyika halafumje na vi ishu vyenu vya kitoto ili vipate back up kutoka kwa ishu kubwa!

Hawana hata chembe ya historia ya Watanzania walikotoka. Wangekuwa na uchungu wasingetaka sera ya USHOGA, kweli hawa matapeli wa kisiasa wanawatakia mema WATANZANIA ????
 
Siwezi kuwalaumu sana maana uwezo wenu wa kufikiri ndo umeishia hapo mtakuwa na utapiamlo wa akili!

Kwa kweli mimi uwezo wangu wa kufikiri na kukumbuka umeishia hapo kama wewe uwezo wako wa majungu, kutofahamu taratibu na kung'ang;ania kupewa sifa kwa vijitu vidogo umeishia hapo
 
Wewe acha kupotosha....Unajua kama LEMA angekuwa ana nia njema na huu mradi yeye asinge lalama angemuacha rc Apige porojo ambazo yeye LEMA na walio wengi wanaamini si kweli kwa RC ANACHOKISEMA then ANGETAFUTA PRESS CONFERENCE NA kueleza ukweli halisi ama kupinga alicho kisema RC juu ya huu mradi but alivyo provokes pale moja kwa moja hii inajionyesha ya kuwa HAPA KUNA HARUFU YA DILI thus why jamaa aliwai kupaniki sana AKAMUONA RC kama kauzibe kwenye hii DILI yake,,,,,,NA NDIO MAANA HUMU VIJANA WENGI WA CHADEMA MLIKIMBILIA KUPOST VIDEO YA LEMA TU mlitakiwa kupost full VIDEO ya hata hile ua RC akiwa anaongea
Mkuu Kibstec, kwa namna ilivyo kwenye hiyo project, Lema angeweza kushawishi hata mkuu wa mkoa asiwepo na angetafutwa mtu mwingine wa kuzindua. Ukifuatilia taarifa za tukio hilo unaweza kubaini kwamba RC hakutaka kabisa kutokea kwenye hilo tukio kwa sababu tu mradi huo umefanikishwa na Lema kwa kiwango kikubwa sana. Lema alitaka RC ashuhudie kama mwakilishi wa rais kuwa wao Chadema wanaweza kushawishi na kufanikisha miradi mikubwa kama huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa jamii, jambo ambalo limedhihirika RC halipendi! RC alianza kukwepa kwenda hadi alipopigiwa simu katibu mkuu kiongozi pamoja na katibu mkuu tamisemi, ndipo RC akaenda. Lakini, kwa kuwa alikuwa na hila akaenda kwa nia mbaya huku akiwa ameandaa taarifa yake ya kuokoteza kuhusu mradi huo ili kumfanya Lema aonekane si chochote.

Binafsi, kwa mazingira yalivyo, alichokifanya Lema ni sawa kabisa, hapakuwa na sababu ya kusubiri kufanya press conference baada ya tukio hilo. Ni vizuri wafadhili na watu wengine ambao walihudhuria waone upuuzi wa aina ya watu ambao serikali imewaona ndio wanafaa kuongoza, kwani kusubiri kufanya press conference pengine watu walioshuhudia uhuni wa RC wasingepata muda wa kuangalia/kusoma habari ambayo ingetokana na hiyo press conference. Alichokifanya Lema ndicho kiliwafanya wananchi wamzomee RC. Na dawa ya moto ni moto!
 
Kwa vyovyote vile hakuna mtu timam atapinga mradi wa maendeleo. Naomba maelezo ya kina Mkuu wa mkoa alifanya nini hasa kilicholeta mtafaruku? Na alichosema/fanya huyu rc kina impact gani kwa lema au mradi wenyewe kias ilitakiwa nguvu ya haraka kwa counter attack? Naona video hazijanisaidia.
 
Wewe acha kupotosha....Unajua kama LEMA angekuwa ana nia njema na huu mradi yeye asinge lalama angemuacha rc Apige porojo ambazo yeye LEMA na walio wengi wanaamini si kweli kwa RC ANACHOKISEMA then ANGETAFUTA PRESS CONFERENCE NA kueleza ukweli halisi ama kupinga alicho kisema RC juu ya huu mradi but alivyo provokes pale moja kwa moja hii inajionyesha ya kuwa HAPA KUNA HARUFU YA DILI thus why jamaa aliwai kupaniki sana AKAMUONA RC kama kauzibe kwenye hii DILI yake,,,,,,NA NDIO MAANA HUMU VIJANA WENGI WA CHADEMA MLIKIMBILIA KUPOST VIDEO YA LEMA TU mlitakiwa kupost full VIDEO ya hata hile ua RC akiwa anaongea

kiukweli inauma ...vaa viatu vyake
wako wengi wanavumilia hadi kutukanwa kwenye mikutano ..na anayeongoza kuwatukana wanamuiga ..Mameya wanatukanwa ...wakialikwa wakihudhuria ,wasipohudhuria kwakuwa hawakualikwa wanatungiwa maneno kuwa hawapendi maendeleo ndio maana hawajaja au wanaunga mkono ujambazi ...maneno kama hayo ..
sidhani watu kama Joseph mbilinyi na Lema wanakiwango hicho cha uvumilivu ..pengine wakuu wa mikoa watajifunza iko siku zitapigwa jukwaani na wananchi watatetea wabunge wao itakuwa maafa
 
Back
Top Bottom