Nimejisikia uchungu mkubwa, sababu nafahamu historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Arusha

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,935
5,558
Hakuna siku nimejisikia uchungu mkubwa kama jana, kwasababu nafahamu historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto, na nimeshiriki katika hatua mbalimbali za ujenzi wa maono haya.

Lema alikuwa na ndoto hii kwa muda mrefu, na aliitangaza hadharani katika kampeni zake na CCM walimdharau na kumuona kichaa, na wakati mwingine Lema alikuwa akisema, CCM wakiendelea kumuudhi na kumkejeli na ndoto hiyo, ataijenga hiyo hospitali na ataiwekea na swimming pool mithili ya hotel.

Muda ukafika Lema kupitia ushawishi wake na timu yake wakafanikiwa kupewa kiwanja na Mawala Trust, na siku ya makabidhiano nilikuwepo, na hakukuwepo kiongozi yeyote wa Serikali, Mgeni rasmi alikuwa Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema.

Hii inaonesha wazi kabisa Mawala si tu walikuwa na moyo wa kusaidia watu wa Arusha kupata Hospitali ya kusaidia akina mama na watoto, pia walionesha mapenzi ya wazi kwa Chadema, kwa kukabidhi kiwanja hicho chini ya Ugeni Rasmi wa Mwenyekiti wa Chadema taifa.

Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutafuta udhamini wa ujenzi wa Hospitali hiyo kitu ambacho watu wa Arusha tulisema hata kwa michango binafsi tutaweza kuchangia ujenzi wa hospital hiyo, lakini Mh. Mbunge kwa ushirikiano na taasisi yake ya Arusha development Foundation (ArDF) waliendelea kutafuta wahisani hadi walipokutana na watu wa Maternity Afrika ambao waliingia nao mkataba wa kujenga Hospital hiyo kwa thamani ya Bilioni 9 za Kitanzania.

Hatua ya aibu ni ya leo ambayo huyu anayejiita mkuu wa mkoa kutaka kwa makusudi kuharibu kazi nzuri iliyofanywa kwa miaka mingi bila msaada wowote wa serikali, kisa ameitwa tu kuiwakilisha serikali kama mgeni rasmi, tena Lema akiwa hana shida yoyote ya uwepo wake.

Aina hii ya viongozi hawawezi kutufikisha kwenye nchi ya viwanda anayosema Magufuli. Wamejaa ujinga wa kichama na wanafikiria muda wote ni muda wa kufanya siasa na kutweza kazi nzuri zinazofanywa na wapinzani.

I find this to be the highest level of stupidity I have ever seen in a leader. It is so sad indeed.

Vielelezo vya picha vipo hapo, na katika hatua zote hizi muhimu hajawahi kuwepo kiongozi wa serikali hii ya CCM, hadi Leo ndo wanajitokeza na maelezo yao binafsi yasiyo na mkia wala kichwa.

FB_IMG_1476816062714.jpg
FB_IMG_1476816067451.jpg

14702272_1164170103674680_24659998827424284_n.jpg
 
Kusema kweli binafsi niliumia sana hasa kwa kitendo cha huyu RC kuja na askari wengi na silaha as if kuna ujambazi! hili linahitaji busara za Raisi ili amchukulie hatua huyu Gambo kwa lile alilolifanya. Gambo amekuwa ni tatizo kila alikofanya kazi. uswahili ameuweka mbele sana. Mikoa kama hii unahitaji Ma RC wenye busara na hekima kama Meck Sadic au Kandoro na sio watu aina ya gambo! jana ameitia aibui sana serikali kwa kiasi cha kutisha!
 
Hakuna siku nimejisikia uchungu mkubwa kama jana, kwasababu nafahamu historia ya Mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto, na nimeshiriki katika hatua mbalimbali za ujenzi wa maono haya. Lema alikuwa na ndoto hii kwa muda mrefu, na aliitangaza hadharani katika kampeni zake na CCM walimdharau na kumuona kichaa, na wakati mwingine Lema alikuwa akisema, CCM wakiendelea kumuudhi na kumkejeli na ndoto hiyo, ataijenga hiyo hospitali na ataiwekea na swimming pool mithili ya hotel. Muda ukafika Lema kupitia ushawishi wake na timu yake wakafanikiwa kupewa kiwanja na Mawala Trust, na siku ya makabidhiano nilikuwepo, na hakukuwepo kiongozi yoyote wa Serikali, Mgeni rasmi alikuwa Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema. Hii inaonesha wazi kabisa Mawala si tu walikuwa na moyo wa kusaidia watu wa Arusha kupata Hospitali ya kusaidia akina mama na watoto, pia walionesha mapenzi ya wazi kwa Chadema, kwa kukabidhi kiwanja hicho chini ya Ugeni Rasmi wa Mwenyekiti wa Chadema taifa. hatua iliyofuata ilikuwa ni kutafuta udhamini wa ujenzi wa Hospitali hiyo kitu ambacho watu wa Arusha tulisema hata kwa michango binafsi tutaweza kuchangia ujenzi wa hospital hiyo, lakini Mh. Mbunge kwa ushirikiano na taasisi yake ya Arusha development Foundation (ArDF) waliendelea kutafuta wahisani hadi walipokutana na watu wa Maternity Afrika ambao waliingia nao mkataba wa kujenga Hospital hiyo kwa thamani ya Bilioni 9 za Kitanzania. hatua ya aibu ni ya leo ambayo huyu anayejiita mkuu wa mkoa kutaka kwa makusudi kuharibi kazi nzuri iliyofanywa kwa miaka mingi bila msaada wowote wa serikali, kisa ameitwa tu kuiwakilisha serikali kama mgeni rasmi, tena Lema akiwa hana shida yoyote ya uwepo wake. Aina hii ya viongozi hawawezi kutufikisha kwenye nchi ya viwanda anayosema Magufuli. Wamejaa ujinga wa kichama na wanafikiria muda wote ni muda wa kufanya siasa na kutweza kazi nzuri zinazofanywa na wapinzani. I find this to be the highest level of stupidity I have ever seen in a leader. It is so sad indeed. Vielelezo vya picha vipo hapo, na katika hatua zote hizi muhimu hajawahi kuwepo kiongozi wa serikali hii ya CCM, hadi Leo ndo wanajitokeza na maelezo yao binafsi yasiyo na mkia wala kichwa.
Moderator badilisheni siyo tetesi hali halisi.
Wewe acha kupotosha....Unajua kama LEMA angekuwa ana nia njema na huu mradi yeye asinge lalama angemuacha rc Apige porojo ambazo yeye LEMA na walio wengi wanaamini si kweli kwa RC ANACHOKISEMA then ANGETAFUTA PRESS CONFERENCE NA kueleza ukweli halisi ama kupinga alicho kisema RC juu ya huu mradi but alivyo provokes pale moja kwa moja hii inajionyesha ya kuwa HAPA KUNA HARUFU YA DILI thus why jamaa aliwai kupaniki sana AKAMUONA RC kama kauzibe kwenye hii DILI yake,,,,,,NA NDIO MAANA HUMU VIJANA WENGI WA CHADEMA MLIKIMBILIA KUPOST VIDEO YA LEMA TU mlitakiwa kupost full VIDEO ya hata hile ua RC akiwa anaongea
 
RC alionyesha hajui chochote kuhusu huu mradi baada ya kusema ArDY badala ya ArDF. Na alionyesha kukusudia na alikua anaongea kwa dharau kubwa.
Kiaibisha Ccm na kamuaibisha Rais .
Rais alikosea kumchagua uyu kijana aliekosa malezi ya wazazi kakakaa kama kibaka.
 
Huyu RC ana maono finyu anadhani anaweza kuwadanganya wanaArusha kuwa ujenzi huo ni juhudi za serikali hii ambayo haiwezi kununua hata dawa kwa hospital zake
Tatizo lake na maRC wengi ni kufanya kazi kwa kutaka kumfurahisha Mtawala,hawajui lingine lolote
Gambo ni janga
 
Wewe acha kupotosha....Unajua kama LEMA angekuwa ana nia njema na huu mradi yeye asinge lalama angemuacha rc Apige porojo ambazo yeye LEMA na walio wengi wanaamini si kweli kwa RC ANACHOKISEMA then ANGETAFUTA PRESS CONFERENCE NA kueleza ukweli halisi ama kupinga alicho kisema RC juu ya huu mradi but alivyo provokes pale moja kwa moja hii inajionyesha ya kuwa HAPA KUNA HARUFU YA DILI thus why jamaa aliwai kupaniki sana AKAMUONA RC kama kauzibe kwenye hii DILI yake,,,,,,NA NDIO MAANA HUMU VIJANA WENGI WA CHADEMA MLIKIMBILIA KUPOST VIDEO YA LEMA TU mlitakiwa kupost full VIDEO ya hata hile ua RC akiwa anaongea
IQ za Watanzania kama wewe ni majanga ya kimataifa.
 
Kujiamini kipumbavu tunao hasa sisi makada wa CCM ukweli siku zote umeniacha huru..! CCM sasa nadhani ni muda wa kuwaonesha wapinzani kuwa sisi ni baba, mama, kaka na dada zao, ujinga wa namna hii ndiyo huwa unatupati wakati mgumu kipindi cha uchaguzi mh. Rais aonywe huyu Gambo sifa za kijinga hizi.
 
Eti Magufuli anapenda watumishi wanaopenda kukwaruzana na wapinzani ndiyo furahaa yake.unaenda kuzindua mradi unabeba Silaha za kivita utafikiri tuko Sudan kusini.kama anajiamini bila kutegemea polisi angeenda Ana kwa Ana siyo kujificha kwenye koti la polisi eti ulinzi na usalama
 
wapi alipokosea mkuuu wa mkoa.....sijasikia sehem yeyote akisema wao serikali ndio walioleta wafadhili ,,,,,,ukiwa chadema lazima uwe kichaa tuuuuu hawana busara kuanzia wa juu mpaka wa chini
Kweli kabisa na ndiyo maana Mh. Lema, mbunge kupitia cdm, akafaulu kuhakikisha hospitali inajengwwa. Kitendo hili kinaweza kufanywa na kichaa tu kwani wenye hekima na busara watazuia ujenzi wa huduma za Afya.
 
Back
Top Bottom