Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,058
- 134,391
Kwa week sasa huyu dada yangu wa hiari nimekuwa nikimpa ushauri nasaha baada ya kupigwa tukio na mmewe. Nimekuwa nikimtia moyo apuuze na amsamehe mumewe.
Haiba yake anaonekana kunielewa, lakini ukisoma hisia zake za ndani kabisa unaona ni mtu anayenivizia anipe mzigo kulipa kisasi.
Lengo langu ni kutaka kuwashauri dada zetu humu mlioolewa. Acheni kulipa visasi mkipigwa matukio, kwa sababu havitakusaidia.

