Nimejifunza kuwa na Roho Ngumu baada ya kupatwa na Matatizo

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,916
24,675
Ni siku mbili sasa toka Nivamiwe na wezi waliovunja Ofisi yangu iliyokuwa unaniweka mjini na kuiba kila kitu,

Hakika sikuamini ile siku Asubuhi nilipofika kufungua na kukuta OFisi nyeupe haina kitu ata kimoja ilinibidi nitazame mara mbili mbili bila kuamini kilichotokea,

Nilipatwa na mshituko ukizingatia ndio ilikuwa imepita wiki moja tu toka Nitumie kiasi changu cha pesa cha Akiba kuapdate mazingira ya ofisi, na kuongeza baadhi ya vitu ili ili pawe na muonekano mzuri wa kushawishi wateja,

Kiukweli baada ya Tukio nilitoa taarifa ofisi ya mtendaji, pia nikaenda kutoa taarifa polisi na kupewa RB,

Kinachonisikitisha ni kwamba muda wangu wote niliokuwa na ofisi ya kazi nilikuwa mtu wa kusaidia sana Washkaji, Ndugu jamaa na Marafiki panapokuwa na Shida kwa kipato changu tu hicho hicho ninachopata,

Lakini sasa baada ya kupata matatizo hakuna ambae amenishika mkono ata na kidogo,
Ndugu, rafiki na jamaa zangu wote niliwapa taarifa ya tatizo lilonikuta lakini niliishia kupewa Pole tu ya mdomo,

Hakuna ata mmoja aliyejaribu kuniuliza au kusema chukua hiki kitakusaidia wakati huu wa mpito Hakuna kabisa,

Sijui labda wanasubiri mpaka niwaombe lakini mimi Siwezi,
Katika maisha yangu neno Naomba nilishalipigaga marufuku haijarishi napitia hali gani ya kiuchumi,

Nilipambana kupata hivyo vitu kwa jasho, Naamini pia nitapata tena lakini kwa sasa Nimejifunza kitu kimoja tu kuwa na Roho Ngumu.
 
Unataka kuwalaumu bure tu.. Sasa wakupe bila kuomba! Kama wao walikuomba ukawapa nawe omba.. Kama huwezi kuomba basi pambana ndio maana wengine huwa na bima Sasa we kama uliwafanya hao jamaa zako kuwa bima ngoja wakubimike..😅
 
Unataka kuwalaumu bure tu.. Sasa wakupe bila kuomba! Kama wao walikuomba ukawapa nawe omba.. Kama huwezi kuomba basi pambana ndio maana wengine huwa na bima Sasa we kama uliwafanya hao jamaa zako kuwa bima ngoja wakubimike..
Mkuu ukiwaomba bado haisaidii wabongo ni nyoko sana.
Ukishamwambia shida yako anakupiga kalenda tutawasiliana,na ukimtafuta mara ya pili utasikia anakwambia"nipo kwenye kelele nitakucheki kaka" ndio imetoka hyo
 
Pole Sana mkuu...
Ila Wala hakuna haja ya kuwa na ROHO NGUMU....

Mtu Mwenye Kujiamini....haishi kuwa desperate mbele za watu BALI anakuwa na MIZANI katika kila Jambo...yaani ANAWEKA USAHIHI katika MUDA SAHIHI.....
Uliwasaidia km mwanajamii....nawe OMBA wakusaidie....
Acha ARROGANCE(kiburi)maishani kwani hata RAIS MAGUFULI alituomba Kura majukwaani.......

Huyu Shemeji yako NISINGEMUOMBA kumuoa asingenizalia hivi viPWA vyako vidogo.

Life's a long journey...UPS AND DOWNS kawaida...

MUNGU akusaidie KIPINDI hichi kigumu Aaaamin,nasubiria UNIOMBE nikutumie kidogo km mchango wangu.

Peace
 
Back
Top Bottom