Nimejifunza katika hili, Tiger Woods ni bora kuliko Ben Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimejifunza katika hili, Tiger Woods ni bora kuliko Ben Mkapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyamahodzo, Dec 17, 2009.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wakiwa ni watu wawili tofauti, toka nchi mbili tofauti, wenye kazi zilizo mbali katika kuwaingizia kipato, lakini wote wakiwa ni wa rangi nyeusi. wametofautiana mbali sana katika kuyakabili matatizo yao yanayogongana na jamii za katika namna zilizo tofauti sana kiasi cha kumpa heshaim kubwa Tiger(kijana wa chini ya miaka 30,mcheza golf) kuliko benjamin (mzee wa zaidi ya miaka 60, Rais mstaafu).

  Sababau ya msingi ya kumpa heshima Tiger ni kuwa katika kipindi kilicho chini ya mwezi mmoja, alipoulizwa ikiwa kafanya kosa lolote dhidi ya familia yake baada ya ajali, alikiri ni kweli hakuitendea haki familia yake zaidi hasa katika mahusiano ya kimapenzi kwasabababu alikuwa na wanawake aliokwishakuwa na na mahusiano ya kimapenzi. Na kwamba aliisaliti ndoa yake.
  Tofauti na woods, Benjamin yeye hata ilipothibitika kimazingira na ushahidi wazi kuwa kawaibia watanzania na kahusika vilivyo kuwaua watanzania/majirani ama kwa kuwalazimisha raia watoke na kuwapisha makaburu wakae migodini au kwa kuhusika kuuza silaha nchi jirani,pia kutengeneza tabaka la walafi na wenye uchu wa rasilimali ya watanzania bado ni mkaidi. Ni mkaidi kwa sababu hadi sasa hajawahi kukiri makosa yake hata mojawapo hadharani kwa watanzania aliowatendea ubaya huo mkuu[/.

  From that point Tiger deserves to be called a hero, rather than Mkapa.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Let me tell you something, Tiger Woods inawezekana amekiri, lakini amekiri tu kwa sababu amelazimika kukiri.

  In fact kuna interview alifanya na TV moja ya New Zealand muda kipindi si kirefu kilichopita, I can't remember how long ago but this year, ambapo ameulizwa kuhusu golf na family akajibu macho makavu kabisa "family first, absolutely"

  Tiger Woods amekiri makosa kwa sababu amelazimika kufanya hivyo, na kama asingekuwa careless kiasi cha kubumbulukiwa asingekiri.

  Ditto Mkapa, kama mnataka Mkapa akubali makosa inabidi kuanzishwa bonge la movement kumshitaki, na kumtolea irrefutable evidence, tuone atasemaje.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna faida gani za kumshitaki mkapa.???...
  let bygone be bygone

  muhimu ni kubadili system inayompa nguvu kubwa rais wa tz....

  asiruhusiwe kuingia mikataba bila bunge kuruhusu.
  asiruhusiwe kuteua mtu bila bunge kuruhusu n,k n.k
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwa che Mkapa, yalivyoibuka ya ya bulyanhuru ilitosah kukubali kosa pale hata kama ni ki utu uzima, haitoshi hilo yalivyoibuka ya Kiwira na ya EPA alikuwa na nafasi (japo hata sasa anayo) ya kuliona kosa lake na kukiri. Zaidi sasa yanapozidi kuibuka ya Meremeta , Mkapa atajificha wapi?

  Kwanini Mkapa alikubali kubadilisha mawazo mkutano mkuu wa CCM 2005 ili kumpata mgombea nafasi ya uraisi kwa kuonyeshwa Blue book ikiwa kilichokuwamo humo ni uwongo.

  Mkuu Bluray, wakili gani aliyeko Tanzania anaubavu wa kumshitaki Mkapa kwa sasa?

  Nakubali kuwa miongoni mwa hao watakaokuwa katika hiyo movement.
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mazee,

  Ukimshitaki Mkapa

  1. Utaonyesha Tanzania ni nchi inayofuata rule of law, na no matter who you are the law will be applied to you.

  2. Tuta set precedents kwa future presidents.

  3. Tutapata wasaa wa kumuuliza mengi tusiyoyajua sasa.

  4. Mkapa mwenyewe atapata nafasi ya kujitetea, suppose Mkapa anaonewa na ana utetezi thabiti, tukiacha kumshitaki na kumpa nafasi ya kuwa cleared in a court of law tunamnyima haki yake ya msingi. Sasa hivi watu wengi wanafikiri Mkapa ni fisadi, mpelekeni kortini apate nafasi ya kujisafisha na watu tujue blow by blow za kesi zimeendaje, ikibidi tupate transcripts kama za kesi ya uhaini a la Muccadam Lakha kwenye Mfanyakazi.

  5. Hata kimataifa watu watajua kwamba kuna Watanzania huko hawataki mchezo, unaweza kuwa rais halafu wajkakushitaki vile vile.

  Umesema "muhimu ni kubadili system inayompa nguvu kubwa rais wa tz....". Kumshitaki Mkapa ni namna nzuri sana ya kuanzisha hili, hii trial itam humanize rais ambaye watu wanaona kama mtu akiwa rais anakuwa demigod asiyeweza kufanya maovu.Tutaona kwa nini inabidi nguvu za rais zipunguzwe vizuri sana.
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kaka, mabo mengi yalianza haribika 1996 during his leadership era. after the death of hero Nyerere things went more worse not undergroung but openly.

  Poor, Benjamin, who can defend him not to be blamed ?
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  kimsingi nakubaliana na wewe but sioni hiyo posibility..
  halafu tuta waste muda mwingi,na energy nyingi while nchi
  bado inazidi kwenda chini....

  tukipunguza nguvu ya rais sasa hivi hasa kwenye masuala ya mikataba
  ya madini kwa mfano,faida yake itakuwa kubwa...

  tujali zaidi future kuliko kutafuta mchawi.....

  muhimu makosa yasirudiwe,na njia nzuri ni kuhakikisha kila
  jambo linapitishwa bungeni kwa kujadiliwa,kuanzia
  uteuzi wa watu,mpaka mikataba..
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naelewa concerns zako zote, na mimi nina concerns kama hizo.

  Lakini, bottom line ni kwamba, Mkapa hajalazimishwa kujibu shutuma.Humlazimishi mtu kujibu shutuma kwa kuandika magazetini tu, kama ana ngozi ngumu - na Mkapa Mmakua yule ana ngozi ya mamba- anaweza kupeta tu, hata migazeti yenu anayo isnob asiisome, awe anasoma The Economist na kunywa Blue label Johny.

  Ukitaka kumlazimisha kujibu mashtaka unamfungulia mashtaka/ subpoena/ any available legal avenue that will force him to appear in court or risk contempt of court.

  Mpaka sasa hakuna legal action iliyochukuliwa juu ya Mkapa, ni maneno tu ambayo yanaweza kuwa dismissed au hata ignored totally.

  Amani will do what he can get away with, na kwa sasa Mkapa can get away with not apologising.Kwa hiyo ndiyo maana ninasema, mforce ku apologize, usitegemee Mkapa mwenyewe apate revelation na ku apologize tu.
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  In retrospect, all revolutions seem inevitable. Beforehand, all revolutions seem impossible.
  Michael McFaul


  Vitu vingi kabla ya kutokea huonekana impossible, vikitokea, ukiangalia nyuma unaona kwamba vilikuwa inevitable.

  Mwaka 1990 nani alifikiri kwamba in 1992 tutakuwa na vyama vingi Tanzania? Walioona hilo wanahesabika. Lakini sasa hivi tukiangalia nyuma tunaona kwamba it was inevitable. Kwa hiyo, it may be hard but not impossible the only thing thats impossible is impossible.

  Kupunguza nguvu za rais sasa hivi kunaendana na kumshitaki rais aliyepita. Kwa mfano, kuna watu wana hii misguided idea kwamba rais mstaafu ana blanket ya kinga wakati ukweli wa mambo ni kwamba rais ana kinga katika shughuli za kiserikali tu. Kwa hiyo, Mkapa ni vigumu sana kushtakiwa kwa mauaji ya January 27 Zanzibar, kwa sababu alisign order kama rais na anaweza ku cite national security clauses.Lakini anaweza kushtakiwa kama Benjamin William Mkapa aliyejiuzia Kiwira, kwa sababu hapo hakuwa ana act kama rais.

  Kwa hiyo usiangalie hii process ya kumshtaki Mkapa kama ku dwell in the past, it is an issue that is also very much in the present with repercussions in the future.Ndiyo maana nikasema ni muhimu tu set precedents, ili kesho akija rais Aziz, ajue kuwa ukijiuzia mgodi utashtakiwa, awe na adabu.Tukimwacha Mkapa rais Aziz hataogopa kujiuzia mgodi, na anaweza hata ku cite precedent ya Mkapa.

  Tatizo unaona future kama haiko related na past na present, haya mambo yanaendana. Na hapa hatuongelei kuhusu kutafuta mchawi ingawa hiyo nayo inaweza kuwa necessary katika kuset precedents ili tusipate wachawi zaidi, hapa tunaongea kuhusu rule of law na justice. Justice hata kwa Mkapa mwenyewe, kama nilivyosema hapo juu, kwamba apate nafasi ya kujitetea.Vipi kama ushahidi dhidi yake ni finyu na kwa kutompeleka mahakamani tunamhukumu katika vyombo vya habari bila kujua undani wa mambo?


  Huwezi ku reconcile commitment yako juu ya umuhimu wa kuhakikisha makosa hayarudiwi na kutetea Mkapa asihukumiwe.

  Ukiacha kumpeleka Mkapa mahakamani unaacha mwanya wa makosa kurudiwa.

  Kama kweli hutaki makosa yasirudiwe, ni lazima umpeleke Mkapa mahakamani.

  Ukisema "muhimu makosa yasirudiwe" unakuwa kama mzazi anayeona mtoto wake kakosea, halafu anaogopa kutoa disciplinary action, anasema tu "usirudie".Hata watoto wengine wanaona mzazi huyu weak na hawezi kufanya kitu, ngoja turudie tumuone atafanyaje, wanakuchezea over and over. Inabidi makosa yote yawe na proportionate consequences ili tuhakikishe kwamba kuna deterring factor.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Noted.
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Dec 18, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Mbona Bluray na Boss mnaongelea kitu kimoja kwa nyakati fofauti!

  Boss anasema tubadilisystem inayompa nguvu rais

  wakati Bluray anasema ashtakiwe leo,

  Mkapa kutoshtakiwa leo ni system mbaya anayoisema Boss.

  Just Imagine, jaji mkuu, mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi n.k, wote wanateuliwa na rais, kesho raia akiondoka hawa waliopewa ulaji na rais hawawezi kumshtaki.Utasema kipindi chake kilipita, weel kuna uwezekano walioteuliwa na mkapa ndio walioinfluence JK hwateue wa sasa hivi, cycl e inaendelea na ndio utakuta hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole, labda kama hauko kwenye system yao yaani SIO MTU WAO! kweli watakushughulikia!

  I wish vyama vya siasa vingeanzisha hiyo movement ya kubadili katiba n.k, forget about uchaguzi; ukiviangalia vyama ndio hao, kila kukicha wanawaza nani anataka kuwaharibia kula, nani atahama lini, nani kasema nini, upuuzi mtupu!

  The fact that we have been talking over and over on the same issue then it is certain something is wrong somewhere!

  Mkapa ndiye alliye engineer fedha za EPA zitumike ili JK aingie madarakani, leo hii mnataka JK amshtaki Mkapa!!!! haingii akilini!
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  egg and chicken case...kipi kianza kumshitaki mkapa ili tuweke precedent (bluray) au turekekbishe system ili yasijirudie..mimi nafikiri yanaweza kwenda yote kwa pamoja.

  mfano wakati mkapa anashtakiwa kwa system iliyopo inasaidia kuonyesha uzuri na ubaya wa systems iliyopo (loophole)

  wakati huohuo wale wanasiasa na wanaharakati wanashinikiza mabadiliko ya system (overall) wakionyesha jamii upungufu wake kutokana na kesi ya mkapa ambaye dhahiri anaonekana kafanya faulu...
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nani anataka JK amshtaki Mkapa?

  Mtu yeyote anayeelewa timidity ya JK na system ya CCM hawezi kufikiri hivi.JK aliyeshindwa kumbadilisha Makamba katibu mkuu wake anayeongea kama hana akili nzuri, ndiye atakayeweza kumshtaki Mkapa?

  Mimi ninavyoongea naongea kama JK na Mkapa wote ni team moja.Ninachoongea mimi ni wananchi watoe pressure moja kwa moja kwa system nzima, kuanzia wabunge, mpaka DPP na hata huko serikalini ambako kuna wachache wanaelewa, kufanya movement ya kumshtaki Mkapa, ku clarify kwamba Mkapa hana presidential immunity over prosecution about Kiwira etc etc.

  Mimi naongea power to the people, siongei kumuomba Kikwete.Central point ya post zangu ni kwamba, watu watafanya kile tu walicholazimishwa kufanya, sasa hivi watu wote wanaoweza kuanzisha movement ya kumshtaki Mkapa hawajalazimishwa na wananchi, wananchi hawana muamko, hakuna maandamano, hakuna lobbyst wanaojipanga nje ya bunge na mabango, waandishi wa habari wanaandika vitu havina kichwa wala mguu, hakuna investigative journalism yenye strategy etc, in short hakuna organization.

  As far as I am concerned Kikwete mwenyewe anatakiwa kuwa impeached na kushtakiwa, sasa atakuwaje na uwezo wa kumshtaki Mkapa?
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  bora mzinzi kuliko mwizi
   
 15. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sina uhakika kama ubora huo uliufikiria kwa kina. unajuaje huenda huyo mwizi anaiba ili akazini. Je kama anaiba ili apate fedha za kwenda kufanya uzinzi ndiyo kusema kosa lake la wizi linapunguzwa nguvu na huo uzinzi wake?
   
 16. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, ni makosa makubwa sana kufikiri kuwa Kikwete anaweza akamshitaki mkapa wala kutoa msaada kumshitaki che.

  Bluray, kasema inabidi ianzishwe movement itakayo mfanya mkapa atoke na kukiri makosa yake hadharani. ideally, movement hii usitegemee itaongozwa na serikali. inabidi iongozwe na wananchi waliochoka kuonewa, kunyanyaswa, kudhurumiwa na kudanganywa-danganywa; na wakiuliza jambo wanatishiwi kuanzishiwa zengwe hadi wanafirisika ama kufa.

  Mkapa na Kikwete wakiwa wote ni mafisadi tofauti yao kubwa ni hii, wakati mmkapa ni fisadi anayekumbuka kukusanya kodi na kuruhusu barabara zijengwe, Kikwete ni fisadi asiyejua kukusanya kodi na mfikiria kuzurura kwenye ma-barabara na ma-ndege ya watu wa nchi nyingine.
   
 17. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hapo kwenye nyekundu, unaposema hivyo jicho ninalokupiga nikama lile unloweza mpiga mtu pale anapokwambia twende tukamfuate Macho Mawili yupo kitongoji kile(ambacho kipo umbali wa km 15 toka mlipo) ili mkachukue funguo za kuinglia ndani ya nyumba. Mnaanza safari kwa mwendo wa kasi, mnapobakiza mita 80 kufika mahali husika anakwambia "Nimesahau! Alisema ataficha chini ya jiwe karibu na mlango, tusipoziona basi takumuulize wema(ambaye ni jirani yenu). Huku hajaja, ila kesho ndiyo atakuja"

  hadi sasa naweza sema ni movement moja tu iliyoweza onyesha mafanikio ambayo vyama vya siasa vimeifanya, nayo ni "Operesheni Sangala". watu wengi wamebadilisha msimamo na fikra zao. na kusema "Alaa! Kumbe!"
   
Loading...