nurbert
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 1,887
- 428
Naomba nikiri kwamba katika mbilinge zangu za
kuwania mabinti ujanani nilipata misukosuko
mingi sana kiasi kwamba kila nikikumbuka huwa
nacheka mwenyewe. Namuomba Mwenye Enzi
Mungu, wanangu wasije wakarithi hiki kipaji
changu. Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1990, wakati huo
nikiwa ni kijana barubaru. Nilikuwa natokea kwa
Kaka yangu Sinza naelekea Mwenge kwa shangazi
yangu nilipokuwa nikiishi. Nikiwa kituoni, ndipo nilipokutana na binti huyu.
Huyu binti alionekana mchangamfu na muongeaji
sana. Alinisalimia kama vile ananifahamu kwa
kuniuliza habari za nyumbani na kama wazazi
hawajambo. Alikuwa ni mweusi na mzuri kwa sura
na umbo. Huwa napenda sana mabinti weusi, mwenyewe huwa nawaita Black Beauty. Pia alikuwa na macho fulani ya kulegea kama vile
amekula kungu, Alionekana kuwa msomi maana
alikuwa anaongea Kiswahili huku akichanganya na
kiingereza. Kwa kuwa na mimi nilikuwa napenda
sana kuongea kiingereza, japo sikuwa nakijua
vizuri, nilijitahidi kuongea naye huku nikiweka manjonjo ya Kimarekani. Mbele ya mtoto ambaye anaonekana yuko vizuri upstairs lazima ujue kuweka mapozi japo kidogo. Kwa kuwa nilikuwa mbovu wa macho na nilikuwa
natumia miwani ya macho aina ya photo Chromic ilinifanya nionekane kuwa ni msomi wa Chuo
Kikuu wakati niliangukia pua kidato cha nne kwa
kupata ziro. Lakini hata hivyo nashukuru hizi English Course zilinitioa kimasomaso nisionekane kilaza mbele ya binti mrembo kama huyu. Nilijaribu kufikiria nilipokutana naye bila
mafanikio. Lakini alinivutia kwa ucheshi wake na
tabasamu lake. Basi pale kituoni tuliongea kidogo
na basi lilipowasili tulipanda wote ambapo
alinilipia nauli ingawa nilijifaragua kutaka
kumlipia wakati nauli ya kumlipia sikuwa nayo. Tulipofika Mwenge tuliachana ambapo alipanda
mabasi ya Kawe alipokuwa akiishi kama
alivyoniambia, lakini tulikubaliana tukutane wiki
inayofuata pale Mwenge kituoni. Ni kweli wiki iliyofuata tulikutana pale kituoni
Mwenge, alikuwa mchangamfu sana safari hii
ikiwa ni mara mbili zaidi. Alikuwa amevaa pedo
nyeupe ambayo ilikuwa imembana na kuacha
mahips yake yakiwa yametokelezea, juu alikuwa
amevaa kitopu chekundu. Basi tulitafuta mahali tulivu tukapata chipsi kuku,
na baada ya kumshawishi kufanya mapenzi wala
hakuwa mbishi, tukaenda katika Gesti ya
TURUNYA iliyoko pale Mwenye Mlalakuwa na
kufanya tendo, ambapo gharama zote alilipa yeye.
Hata hivyo kwenye ushiriki wa tendo niliogopa kidogo, kwani alikuwa anafanya vituko vya aina
nyingi. Lakini nilijua huenda mdadi wa masuala ya
mapenzi. Lakini, kwa kweli, labda kile tunachoita
kupenda ni upofu, ndicho kilichonifanya nisione
ukweli mkubwa zaidi. Tulizoeana na huyu binti
haraka sana lakini vituko vyake vilikuwa vinazidi
kila siku. Kuna siku niliamua kumpeleka nyumbani kwa shangazi yangu nilipokuwa nikiishi. Shangazi
yangu alishangazwa na uchakaramu wake. Mara anakwenda kuwasha Music System iliyokuwa pale sebuleni na kuanza kucheza mziki
Kimarekani, mara atoe hela zikanunuliwe soda,
wakati yeye ndiye mgeni pale nyumbani, ili mradi
alikuwa na vituko vingi tu na uchakaramu
uliopitiliza. Shangazi aliniuliza kama namfahamu yule binti
vizuri na nilimdanganya kwa kumwambia
napafahamu hadi kwao. Ukweli ni kwamba huyu
binti alikuwa akiniambia mara anaishi Kawe, mara
Msasani, mara Masaki na wakati mwingine
Kinondoni, ilimradi hakuwa anaeleweka. Ilikuwa kila tukikutana alikuwa analipa gharama
zote za mtoko mpaka malipo ya Guest tuliyokuwa
tukikutana na kufanya tendo. Lakini pia matumizi
yake ya fedha yalikuwa ni ya fujo. Aliniambia
kwamba alisoma nchini Marekani na baba yake ni
mtu mkubwa sana serikalini. Siku moja huyu binti aliniambia angependa
kunipeleka kwao, ilibidi nimwambie tupange siku.
Nilitaka kuwachukua marafiki zangu wa pale
mtaani kwenda nao kwao, kwani kwa kule
kutokuwa na msimamo kwake kwamba, kwao hasa
ni wapi, nilikuwa nimemwogopa kidogo. Siku tuliyokubaliana kwamba, angenipeleka kwao
ilifika. Niliwachukua rafiki zangu watatu na
kwenda nao. Ni kweli yule binti alitupeleka kwao.
Ilikuwa ni Kawe. Ile kufika tu tukaona watu wa
familia wametulaki kwa njia ya ajabu. Afadhali tunashukutu sana. Kwani mmemuokotea wapi? Ni mwezi mzima sasa tunamtafuta.
Aliondoka na shilingi laki saba hapa Mama yake alisema na sisi tukashikwa na butwaa. ..Kwani kwani .. Alipotea? Niliuliza nikiwa na kigugumizi. Mama yake alisema, Mwanangu masikini ana tatizo la kiakili karibu
mwaka wa tatu sasa .. Nilihisi nikiwa nimechoka, hata kusimama
nilishindwa. Nilijikuta nikikaa chini. Wale
marafiki zangu walinitazama tu. Nataka niwe
mkweli, katika kipindi nilichokuwa nikijivinjari na
huyu binti, nilikuwa nawaringishia sana hawa
marafiki zangu, kwa kujidai kwamba nimeopoa binti wa Kimarekani. Tuliaga na kuondoka huku wenzangu wakijifanya
kunipa moyo. Nasema walijifanya kwa sababu,
wao ndiyo walitangaza kila mahali pale mtaani
kuhusu jambo hili. Walinikera sana .. Kwa mwenzi mzima, nikawa natoka ndani usiku
tu .