Nimeingia choo cha kike ...... part 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kike ...... part 7

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Mar 27, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Inaendelea toka sehemu ya 6 ....

  Nilibaki kinywa wazi, na ni dhahiri nilijua kuwa nimeingia mtegoni. Nilifumba macho, nikavuta pumzi,na kutaka kuongea jambo nikashindwa. Ghafla mlango ulifunguliwa, na HR akaingia akiwa na mfanyakazi wa kumtambulisha. Nilitumia mwanya huo kurudi ofcn kwangu na kuendelea na kazi huku nikitafakari mustakabali wa kumaliza tatizo nililojianzishia mwenye. Ukweli ni kuwa nilimpenda sana binti huyu, ila nilishangazwa na nafsi yangu kuonyesha kusita kwa uhusiano huo.

  Tulipanga kukutana jioni yake na ndivyo ilivyokuwa. Usiku ule hakuna hata mmoja aliyekumbushia mambo wala maongezi ya ofcn, ni dhahiri kila moja wetu hakutamani kuyaongelea. Tuliishia kwa maongezi ya utani na kuchekeshana huku tukiburudishwa na mziki. Tulipeana kampani nzr, na ilipofikia usiku sana kila mtu aliingia kwenye gari lake na kurudi kwake. Hali hiyo iliendelea kwa takribani wiki nne tukikutana na kuongea na kucheka, huku kila mtu akienjoy kampani ya mwenzake.

  Jmosi iliyofuata nilienda nyumbani kwake. Alinipokea lakini alionekana ni mtu mwenye mawazo sana. Nilimsogelea na kumuuliza kulikoni, alinistukiza kwa swali "Unanipenda?" "Yes, sana tu si kidogo …" Nilijibu. "Ningependa nikwambie kitu, utakuwa tayari?" "Ohhh, yes, kwako ni tayari muda wote!!!" Nilijibu kwa mbwembwe. "Nakwambia wewe kwa kuwa ni mtu pekee ninaye kuamini sana, na naomba unitunzie siri hii …" alisema. Nilihisi mwili kuingiwa na woga lakini nikajipa moyo. "Usijali tuko pamoja" Nilimjibu kwa upole. "Na je uko tayari kunioa?" "Yes, Angel kwanini nisifanye hivyo?" Niliuliza. "Ktk hali niliyonayo?" Nilitafakari kwa muda, kwa nini aseme ktk hali aliyonayo sikupata jibu la maana. "Ndiyo" Nilijikuta nimemjibu. Angel aliingia ndani na kurudi na box la makaratasi na vidonge ambavyo niligundua kwa haraka kuwa ni ARVs. Sikuhitaji kuviangalia mara mbili, nilivifahamu sana maana tumekuwa tukivigawa pale ofcn kuwasaidia watu wenye HIV. Pumzi iliniisha ghafla. "Nimeathirika" Alinitamkia. Nilihisi kitu baridi kikipita katikati ya utosi wangu kikipasua mwili wangu na kuteremkia miguuni. Nikakosa cha kusema. "Nina amani na ujasiri wa kusema haya maana ninajua niko na mtu ambaye ninaweza kuchukuliana nami!" aliongeza. "HIV ni ugonjwa tu kama malaria, sema watu tuna tafsiri mbaya, ni ugonjwa ambao unaweza kumpata yeyote, popote!" Nilijibu kwa kujikaza. "Naamini, hutaniacha mpweke baada ya kuujua ukweli huu" Alitamka, nilikosa jibu la kumpa. Kiukweli zoezi la kuwa na uchumba na mtu mwenye HIV wakati mimi sina lilinipa mawazo makubwa. Tulipiga stori kwa dk chache nikiwa nimejawa na mawazo tele, nikamfariji na kumuaga nakuondoka.

  Usiku sikupata usingizi, niliwaza na kuwazia juu ya jambo hili bila majibu. Nioe mtu mwenye HIV? Nilijiuliza. "Kama una upendo wa dhati unapaswa kufanya hivyo" Nilijikuta najijibu mwenyewe. Sasa nitakuwa na maisha gani? Mbona naingia pabaya? Tatizo ni wewe moyo wangu mbona unanifanyia hivi? Nilijikuta naulalamika moyo wangu. Sikuwa na mtu wa kunijibu. Lakini kuoa mtu mwenye HIV si sawa na kujiua mwenyewe? Sasa kwa nini nijaangamize? Lakini nini hasa upendo maana yake? Si kuwa mwaminifu na kushiriki ktk hali kama hii? Lakini nikimkataa jamii itanichukuliaje? Na nikimkubalia familia je? lakini mbona moyo wangu bado unampenda? Hivi kuna tatizo gani nikiutii moyo wangu? Moyo wangu moyo wangu, mbona unanitenda? Jamani kupenda nini? Maswali hayakuniisha! Usiku ule ule nilimka na kwenda kwa Katunzi na kumueleza mkasa mzima. "Hapana HP huna sababu ya kujitafutia matatizo! Mwambie mtaendelea kuwa marafiki lakini ndoa hapana" Yap, hilo ndilo jibu nililotoka nalo hapo. Nilirudi kwangu na kupiga magoti kumuomba Mungu anisamahe sana sana kwa yote, kwani sina uwezo wa kufunga ndoa na binti huyu. Nilihisi moyo wangu kuumia sana, na kuhisi matone ya machozi yakidondoka toka moyoni mwangu. Nikiwa katika msongo wa mawazo meseji iliingia, kwa uvivu sana nilinyanyuka kuifuata simu, nilipofungua inbox, sikuamini nilichokiona …  ***** Itaendelea baada ya muda mfupi, again sorry! SEHEMU IJAYO, NI YA MWISHO, USIKOSE! *****
   
 2. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ​we mkaaareeee
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Imebaki sehemu ya mwisho naendelea kuichapa nitakupatieni muda si mrefu ...
   
 4. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tunaisubiria hiyo last episode
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145

  No Problem.
   
 6. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  HP hii ni nzuri. Ila Mwisho wake ndio nautamani zaidi

  Maana ukiacha tu UME MNYANYAPAA mdada
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Wewe unataka kuanzisha topic nyingine pana hapa, ungekuwa ww ungekubali kuolewa?
   
 8. BAOSITA

  BAOSITA JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo naona kama huyo Angel hana HIV vilee...labda alikuwa anamtega HP aone upendo wake.Hahah,I'm just guessing!
  ---Believdat---
   
 9. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tusubiri mwisho , tusije mfanya HP aanze ku editi story yake ili kuufurahisha umma
   
 10. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 817
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  unatisha mkuu big up
   
 11. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Usimchezee Chatu oooo Chatu ooo Gongo Usimtupie Utaukosa Ushindi Natoa Onyo kwa wale wote wanaomchezea chatu
   
Loading...