Nimeichukia Taarabu ya kisasa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,512
Reaction score
860,555
Taarabu ulikuwa muziki wa mwambao wenye mahadhi tulivu na yenye kuburudisha mno ,hata mashairi yake yalibeba mafumbo ya kweli aingia mipasho matusi na kejeli za wazi.

Tangu hapo taarabu ikapoteza maana kabisa kuanzia mashairi mavazi mpaka uimbaji na uchezaji.

siku hizi maonyesho ya taarabu ni sehemu muhimu ya mashoga siku hizi Taarabu ni shortcut ya kuchambana uswahilini

Taarabu imepoteza maana imechuja imechakachuliwa vibaya mno
 
Taarab ya kweli watu hawachezi......muziki wa kusikiliza tu

Ilikuwa ni aina ya mziki wa mwambao wenye kuheshimika mno ambao uliweza hata kualikwa kutumbuiza kwenye dhifa za kitaifa na kimataifa
 
Siku hizi kuna wacheza viduku kama singeli na ili kuendana na mapigo yake lazima jasho likutoke, zamani ilikuwa kwenye viti tartiiiiibu huku unapata mziki mzuri.
 
Siku hizi kuna wacheza viduku kama singeli na ili kuendana na mapigo yake lazima jasho likutoke, zamani ilikuwa kwenye viti tartiiiiibu huku unapata mziki mzuri.
 
Kuna huyu dada anajiita mashauzi ndo hovyo kabisa...kauharibu huu mziki tuliokuwa tukicheza tumekaa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…