Nimeibiwa kwenye kituo cha kuuzia mafuta ya petrol Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeibiwa kwenye kituo cha kuuzia mafuta ya petrol Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ntemi Kazwile, Jun 25, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana nilikuwa nasafiri kutokea Iringa nilikokuwa nimeenda kikazi, nilipofika Morogoro ikanibidi niingie sheli mojawapo hapo kujaza mawese (Sheli hii iko barabara ya Moro-Iringa kwenye junction na barabara ya Mazimbu).

  Nikaomba nijaziwe full tank, kwa sababu najaza hapo mara kwa mara sikuwa na wasiwasi hadi nilipotupa jicho kwenye mita nikaona inaelekea lita 87 (huku gari bado inadai). Kiwango cha juu kabisa ambacho niliwahi kujaza kwenye gari langu ilikuwa ni lita 75 wakati taa ilikuwa imewaka na mshale kugota mwisho. Nilipata mshituko kwa sababu kwanza gari ilikuwa na mafuta yamepungua kidogo tu kwenye robo tank na halafu bado yalikuwa yanaendelea kutiririka (huenda hata 95 zingeingia).

  Maswali yangu je kuna chombo chochote kinachowalinda walaji kuhakikisha kuwa hawaibiwa katika vipimo kama ambavyo mimi nimeibiwa jana??

  Baada ya kuendelea kutuharibia magari yetu kwa chakachua sasa wanaelekeza nguvu kwenye mita sijui kama hii nchi itaendelea kwa ukesefu wa usimamizi wa sheria kama hivi.

  Naomba wakazi wa Morogoro na wasafiri wengine wawe makini na sheli hii, ni hatari
   
 2. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii petrol station kuna wizi. Nami wiki mbili zilizopitanilifika kituoni hapo kujaza mafuta. Yule petrol attendant akataka kunizubaisha. Alipomaliza kujaza mafuta, akataka nilipe gharama ya mafuta iliyokuwa juu kwa kiasi cha Tsh 15000. Kwa kuwa nilikuwa makini kuangalia kiwango kilichowekwa, ilibidi kupishana na yule jamaa. Hatimaye nililipa kiwango sahihi.

  Ni vyema tukawa waangalifu na kituo hiki.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Juzi niliwasikia Ewura wakiomba taarifa kama hizo so mkubwa nakuhauri uwatafute!
   
 4. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WanaJF nawashauri msijaze kwenye hiki kituo cha TIOT ni cha Barabuu aliyefulia kwa sasa, wale ni wezi na wachakachuaji wa wese wazuri, kajazeni pale Msamvu BP au ingieni ndani hadi hapa Agip opp. na hosp ya mkoa(Morogoro).

  Hawa EWURA wameshakula hela hawana meno tena, Ni biashara Holela sio Huria, Bongo zaidi ya uijuavyo.

  :dance:
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Contact zao ni zipi mkuu. Mimi ningependa kiripoti hii incidence angalau hata wasipofuatilia nimetimiza wajibu wangu. Iliniuma sana
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwenye pump kuna mahali ukibonyeza inatoa hewa tu so mkuu ulikuwa ukijaziwa hewa.
   
 7. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  aisee ndo mana magari yetu kwishnei kabisa
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mi bado nadhani njia nzuri zaidi ni wana jamvi kuvianika vituo vyote ambavyo vina michezo michafu ya namna hii au kuchanganya mafuta. Itawasaidia wengi sana!

  Mkuu pole sana, naisukuma hii kwena EWURA tuone kama watachukua hatua zozote
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  ...hebu endelea na story!!! hukurusha ngumi??
  Mi nisingelipa, na ningeondoka!!

  jamani tuwe makini sana!! mi nilishawekewa mafuta ya 30,000/ Iringa oryx badala ya 50,000 niliyosema yawekwe.
  Wana-time kama hutoki kwenye gari kuangalia pump, wanaset pump kutoa mafuta kidogo, then unatumia muda mwingi ukifikiri, 50,000 ndo imetumika kumbe 30,000.
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Pole Mpwa! Naamini EWURA watasikia kilio chako na hatua zitachukuliwa. Mwaka wa uchaguzi huu bana ndio wakati wa wananchi kutatuliwa matatizo yao
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,814
  Likes Received: 20,786
  Trophy Points: 280
  1.inawezekana muuzaji wakati anakuwekea hakuset pump at 00.00 so alianzia wakati pump inasema 15litres[may be]
  2.inategemea una gari gani,lingine linawaka taa[warning] lkn mafuta yanakuwa mengi so siku ulipoweka lita 75 level haikuwa chini kama hii siku ingine ''ulivyoibiwa''

  WABONGO acheni umwinyi shikeni pump jazeni mafuta wenyewe msiwachie hao wezi wawaibie kirahisi.....huku kijijini unajaza mafuta mwenyewe then unaenda kulipa.
   
 12. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii sheli ni mpya inaitwa Petro. Nilikasilika na yule dada aliyekuwa ananijazia alijua kabisa kwamba ameniibia kwani nilipokuwa nalalamika alikuwa na guilty consious lakini kwa kuwa sikuwa na namna ya kuthibitisha kuwa nimeibiwa nililazika kulipa, kwa shingo upande! EWRA basi wasichuke fees bila kutoa huduma kwa sababu nasikia kwenye kila lita wana mkwanja wao.
   
 13. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Invisible mi naanza,hapa moro viko kadhaa.Hicho cha TIOT iringa road karibu na njia ya kwenda Mazimbu, Kingine kipo mita chache toka keep left ya SUA kama unaenda SUA, Kingine ni TIOT iringa road njia panda ya kuingia mjini toka mzumbe, Hapa Oilcom karibu na mjimpya nao siku moja moja mafuta yao sio mazuri, pia na hiki kilichopo opp na CRDB mandela branch kinawalakini, Kwa moro sana sana ni hivyo, ila TIOT ni vituo namba moja vinavyochakachua wese na kwa bahati mbaya viko highway kama pale nane nane na kingulwira. EWURA mpoooooooooo? Chukueni hatua za kisheria sio kuchukua hela tu.
   
 14. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,814
  Likes Received: 20,786
  Trophy Points: 280

  hio ndio dawa yao mkuu.........kuvianika na kuwatangazia watu wawe makini wakienda kuweka mafuta huko.......
   
 15. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hata ukishika pampu mwenye haisaidii. Na kumbuka kuwa gari hili ninalo tangia 2006 na kuna nyakati si moja ambayo nimejaza wakati mafuta yakiwa yameisha kabisa na sijawahi hata siku moja kufikisha lita 80!!!!
   
 16. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mimi nawashauri wanaJF pamoja kwamba tunaibiwa ukiwa unaweka mafuta sehemu yoyote shuka kwenye gari uangalie anavyoweka.

  Usimuruhusu kubonyeza kwa nguvu mwembie aweke taratibu. Akiweka kwa speed badala ya kukuwekea 20,000 anakuwekea 10,000
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Underlined hapo umenena mkuu
   
 18. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni petrol stesheni gani bongo hii watakupa pump ujaze mwenyewe? hapa dar sijaona hata moja.........! Ukichangia sometimes changia kibongo bongo kwa ku-reflect hali halisi mkuu
   
 19. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #19
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  KoK,

  Umenifanya nishtuke. Kama ni hivyo basi wengi wanalizwa bila kujua!
   
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Tabia ya kutokulipa fweza kwa watumishi kihalali. Kama wafanyakazi wangelipwa kwa haki hao waweka mafuta wasingekuwepo, wapo kwa sababu serikali imeshindwa kuona haki inatendeka kuweka kiwango cha mshahara kinachoendana na maisha. Aibu kwa serikali ya JK na Chama Cha Majambazi.
   
Loading...