Nimegundua wanawake huwa wana expire date

Nimegundua wanawake huwa wana expire date

Joined
Oct 11, 2015
Posts
15
Reaction score
12
Kuna binti tulikua tukiishi mtaa mmoja katikati mwa miaka ya tisini, alikua ni mzuri ajabu, kwa lugha ya kawaida hakuna Maneno yanayojitosheleza kuelezea uzuri wake
Wakati huo mm nilikua form four yeye form three, vijana wengi sana walijitosa kumtongoza, mm nilikua mmoja wao

Nilikua nampenda sana yule binti, nikamwandikia barua ya mapenzi, siku kadhaa mbele akanijibu kuwa hanitaki kupitia barua pia, maana wakati huo nadhan mtindo Wa kuandika barua za mapenzi ndio ulikua unaelekea ukingoni, nakumbuka kwenye 97+ ndio simu zilianza kuja ingawa waliomudu walikua wachache sana

Nikaona niongee nae uso kwa uso isije ikawa barua yangu ilichakachuliwa na dalali niliemtuma , bado alinijibu Maneno yafuatayo. Kwamba "" nakuchukia, sikupendi, kwanza wewe sio handsome kama flan na flani, hatuendani, hivyo usinifuate fuate, zaidi ya yote kwenu kumechoka, utanipa nini? nikamwelea nikafuta mawazo hayo nika concentrate na masomo yangu

Nikamaliza forum 4 then 6 then nikachaguliwa UDSM, nikafanya computer science and mathematics, then nikapata wafadhili nikapata scholarship nikaenda kufanya masters ya IT university of the Western cape SA
Nikarudi hapa nikakuta ndio mabenki mengi yanaanza mfumo Wa kufanya transactions live online, ndipo watu wengi Wa IT tulipoanza kugombaniwa na mabenki hayo mwanzoni mwa 2000 -2005
Mungu si athumani nikaingia mkataba mnono na benki moja ya makabwela iliyokua imenunua system ya EQUINOX
Ama kweli elimu haitupi mtu

Baade nikaamia benki nyingine ya kigeni ambayo nipo hadi sasa, namshukuru mungu, nimewajengea wazazi nyumba, mm zangu mbili, nimewekeza miradi kadhaa, nimewainua wadogo zangu na kadhalika

Kumbe wanawake huwa wana expire

Kama miezi mitatu iliyopita nikiwa ofisini kwangu, nilipigiwa simu na reception kuwa kuna mgeni wangu anaitwa Lydia tumruhusu aje? Nikajibu ndio, hata hivyo nilijibu ndio bila kujua ni Lydia yupi huyo kaja kunitafuta kazini?

Alipoingia nilishtuka kumuona ni Lydia Wa Mtaani kwetu miaka hiyo,ni yule binti alienikataa kwa mbwembwe, hatukuwahi kuonana tena baada ya mm kumaliza form four na kuondoka mkoani kwa safari ndefu ya shule iliyonifikisha hapa
Nilisonenaka mno moyoni, Lydia amechoka, amedhoofika, nywele zilizokosa matunzo, ingawa uzuri usoni upo lakini amekonda, alionekana wazi maisha yamemtandika vilivyo
Akanieleza alikutana na mama yangu mkoani siku za karibuni ndipo mama akamuelekeza ninapopatikana, binti akadai amenitafuta muda mrefu bila mafanikio hadi alipokutana na mama yangu, maana wazazi walishahama Mtaani long time

Jioni yake tulikaa sehemu tukaongea mengi, nikampeleka changanyikeni anakofikiaga kila akija dar, kumbe Ali fail form 4 na 1999 alifiwa na mama, 2003 Mzee akafariki

Tangu tumekutana July alipokuja ofisini nimekua nikimsaidia mambo mbali mbali, in short anaishi hapa kwa hisani yangu, kwa sasa amenona, uzuri wote umerudi, nyonyo zimesimama kama bolibo, nimekua nikimhudumia kama Rafiki Wa kawaida kumsaidia, hali ilikua mbaya sana

Mm sijamgusia neno lolote kuhusu mapenzi, lakini kwa dalili zote ni wazi anataka tuwe pamoja, kwanza alianza kuniomba msamaha kwa Maneno aliyoniambia huko nyuma, kwamba alikua bado mtoto asieweza kufikiri sasa sasa, hakujua anahitaji nini wakati huo, kwamba hayakutoka moyoni mwake, nikamwambia yalishaisha hayo siku nyingi, tukaishia hapo, hatujawahi kuongea way forward, ingawa anafika kwangu Mara nyingi anapika na kufanya usafi kama washikaji tu, maana kuna ndugu wengine naishi nao hapo, mm bahati mbaya kwa upande wangu, mapenzi kwa miaka mingi hayaniendei vizuri, eneo hilo Nina sifuri, sijakua na stable relationship, hata mwaka huwa simalizi na msichana tunashindwana, hata nilie nae sasa hivi ni kama hakuna mwelekeo, Nina watoto wawili Wa wanawake tofauti

Hata hivyo kwa hali ya huyu Dada nimejiuliza ujanja Wa wanawake uko wapi? Jinsi alivyotusumbua Mtaani you can never believe, now she is on her knees, kumbe wanawake wana expire date ikipita Basi inakua dhahama

Sasa Rafiki yangu mmoja ananishauri mchukue huyu mtoto uishi nae, mtoto mzuri kiasi hiki bado unajiuliza uliza? Anasema

Lakini kiukweli Ninasita sana kujihusisha na huyu binti kimapenzi kwa sababu ya maswali yafuatayo

(1) amepita sehemu ngapi, na amehangaika kiasi gani na wanaume hadi kufika hapa?

(2) kwa nini msichana mzuri kiasi kile ameshindwa kuolewa kwa miaka yote hiyo? Watu hawamuoni? Wasichana karibuni wote Mtaani pale nasikia waliolewa tena wengine wabaya Wa sura, yy ilikuaje? Yupo kwenye mid 30s tupo kwenye rika moja mm namzidi kidogo nipo kwenye late 30s

(3)pale Mtaani kuna wengine pia walikua wanamfuatilia enzi hizo je hakuna aliempata?

(4) je sio kwamba ugumu Wa maisha na matatizo yaliyompata ndio yamemleta kwangu na sio Upendo?

(5)je hakuna jambo kubwa lililojificha nyuma ya pazia nisilolijua? Maana sina Wa kumuuliza historia ya huyu Dada baada ya mm kuondoka Mtaani, na wengi waliondoka pale kwenda kutafuta life kwingine

Kuna yeyote anaweza kunisaidia kujibu haya maswali?

Nb, sehemu niliyoeleza mafanikio ya kielimu na kikazi ni kutaka kukupa picha ya wakati huo nakataliwa na sasa nimefanikiwa, naomba isieleweke vinginevyo
 
mh....unaeza oa,kumbe vijana wenzio kule mtaani walishapiga wote,,,,,wakija kukutembelea wamkute hapo sijui inakuaje,,,,mimi dame wa mtaani kwangu sioi
 
Siku zote Mungu anakupa kile unachohitaj ni swala la muda tu sasa leo amekupa unataka ushangae?
 
Utoto nao kazi, ujana maji ya moto, peleleza umri wa Samia Sululu na lile jicho kama kala kungu ukisema wanawake wanaexpire date wenzako tunakushangaa, by the way kwa sasa namlia misele Sophia Simba ananikuna kwelikweli, unaujuwa umri wake?

Tafuta wanaume uliosoma nao tangu shule ya msingi kama wengine hawafanani na Babu yako, usichanganye economy harassment na life style.
 
Siku zote Mungu anakupa kile unachohitaj ni swala la muda tu sasa leo amekupa unataka ushangae?
Hapo sasa, kama Mzee Mwanakijiji kahamasisha watu wafunge na kuomba kwa siku 40 kule Facebook ili ccm iondolewe madarakani hatimaye Mungu kajibu maombi kaletwa Lowasa, Mwanakijiji hataki anataka kumpangia Mungu Rais awe nani.
 
Last edited by a moderator:
Nikamaliza forum 4 then 6 then nikachaguliwa UDSM, nikafanya computer science and mathematics, then nikapata wafadhili nikapata scholarship nikaenda kufanya masters ya IT university of the Western cape SA
Nikarudi hapa

hujitambui tu na elimu iliyo nayo?
 
Ni kwl mkuu,7bu yey mwenyew kakir kuwa hajawah kuwa na stable relation,mim naona amchukue kwan kajifunza meng huyo dada
 
Unajiuliza na kushangaa kwanini mpaka leo hajaolewa pamoja na uzuri wote aliokuwa nao, kama ni ajabu basi hata wewe unastaajabisha manake mbona hata wewe mpaka leo hujaoa pamoja na mafanikio yote uliyonayo? Na swala la kusema eti kapitiwa na wangapi, kwani wewe umepitia wangap? Anza kutoa kwanza boriti lako ndo utoe la mwenzio
 
1. Story ndeeefu ya Equinox sijui bank ya kabwela, umewajengea wazazi, eti una miradi kadhaa yote ya nn!?
2. Wewe sisi tutawezaje humu ndani kuyajibu maswali yote hayo kama we unashindwa kuyajibu!?

3. late 30's kwan bado hujaoa na hata mwanamke mwenye uelekeo inaonekana hauna,lazima una tatizo lililojificha.

kukushauri,
kama mwanaume usitazame sana ameshatembea na wangapi au nani amepiga, cha muhimu ni kucheki kama anasifa stahiki za yeye kuwa mke, ikiwemo akili ya maisha, kuyatambua majukumu yake vizuri, uhusiano mzuri na Mungu, ana uwezo wa kufanya kazi vizuri na kuzalisha na la mwisho ni kuwa awe ana afya timamu kwa maana ya kupima HIV
 
bora usioe. mm sitaoa and i'll only have single-dad family. nachukizwa na kufanywa chanzo cha mapato, sipendi kulea financially mwanamke ambae muda wowote anakukataa ukimess maisha. ntakula starehe zote peke yangu na watoto wangu na housegilr anayewalea..i'll never touch her kwasababu at every moment, i'll have short relationships (hit and run). swala la kununua papuchi moja na kuiweka ndani (kuoa) mwisho wa siku ntaichoka na kuwa mtu wa michepuko...bora nisioe na michepuko iitwe girlfriends.

Ndoa inazima mwamko wa mapenzi, nimekuja kugundua kuwa raha kubwa ya uhusiano kwa mwanaume ni kuwa na active sexual feelings...lkn ikifikia stage ukimwona mkeo hata hujiskii kugegeda...tafua jibu. ninahitimisha kwa kusema kuwa; mapenzi ni sawa na chakula, huwezi kula wali kila siku. idea ya kuoa na kuwa na familia inahimiziwa ili dunia ilendelee kuzunguka, lkn sio lazima niwe mmoja wao (watakao ijaza dunia - kwa kuoa, kuzaa na kumentain familia). ile shauku ya kukuzwa na wazazi waliooana na kuona kila kukicha watu wanaona ndio ilinisukuma kuoa (bila kusahau penzi zito la niliyemuoa)..nimehitimisha kwa kuona kuwa "all is corrupt", ndoa ni advantage kwa mwnamke tu (for security purpose of course, mainly financially), if i can live happily without it...LET IT BE,
 
Kwa umri wake ni kawaida wala hajaexpire sasa ulitaka awe kama alivyokuwa kwenye 18's amekula ujana wake na sasa amekuja kupumzika na mzee mwenzie. Na alichokisema siku za nyuma alikuwa anakimaanisha "Kwamba nakuchukia, sikupendi, kwanza wewe sio handsome kama flan na flani, hatuendani, hivyo usinifuate fuate, zaidi ya yote kwenu kumechoka, utanipa nini? Sasa hapo mkuu si unaona kwamba alikukataa kwavile haukuwa handsome na sasa kwa kupata kazi nzuri na hela naamini wewe ni handsome kuliko hao aliokuwa anawataja ndo maana hata yeye ulimwona amedhoofika ukashtuka na kumwita kwamba amexpire kwa sababu unajiona uko sawa kuliko wengine na kingine alikuuliza kwenu kumechoka utanipa nini? Na sasa cha kumpa unacho hana wasiwasi wewe unafikiri ungekuwa huna hela angekufata? na kwanza ungekuwa umeshazeeka bado angeendelea kukuona humfai. Kama ni kuoa oa tu hajaexpire bali ameona sasa ndo umefika kwenye level zake tofauti na miaka ile ulipokuwa choka mbaya na sura iliyokomaa.
 
Back
Top Bottom