Akili 7
JF-Expert Member
- Apr 22, 2019
- 731
- 1,421
Dah, umechelewa sana sisi tuliowagundua mapema ndio maana hatutaki hata kusikia swaga zao maana tunajua wanatupanga tu, pumbav.1. WABUNGE waliotakiwa kuwa watetezi wa Wananchi, wao wanakuwa watetezi wa mhimili wa Serikali.
2. Rais ambaye ni Kiongozi wa Serikali ambaye alitakiwa kutowabagua watumishi wake wa Serikali pamoja na Wananchi wote, yeye anaruhusu:-
I. Wabunge kujiongezea posho na mishahara mikubwa huku watumishi wengine kama vile Walimu, madaktari nk. kubaki kama walivyo.
II. Wateule wake kupata facilities nyingi kama vile Magari ya gharama kubwa, makazi, vyakula (Ma DC na Ma RC nk.) huku watumishi wengine kama vile Walimu, madaktari nk. wakijitegemea kwa kila kitu kuanzia makazi, vyakula, usafiri, matibabu nk.
Hii haikubaliki hata kidogo. Wakati huu ni lazima makundi yote yapewe haki sawa.
Haiwezekani Genge la watu wachache linapewa kipaumbele kuliko kundi jingine. Ni muhimu sana viongozi wetu wasijifanye wafalme huku jamii kubwa ya Watanzania wakiishi maisha magumu kuwahi kutokea.