Nimegundua mke wangu ana watoto wawili nje

Lakini ana watoto wawili, na nimekaa nae miezi minne lakini sikuwahi kujua kama ana watoto,

Nimekuja kujua kama ana watoto baada ya mtoto wake kuugua na kuhitaji msaada wangu kwaajili ya matibabu,

Upendo umepungua from higher to lower point,

Naomba kuwasilisha ushauri wenu ni muhimu wadau.
Akili ndefuuuu
ukipenda boga penda na majani yake.utaacha wangapi sasa.be strong man
 
Familia yake ndo wasiri na akiongozwa na mkeo
Mpk unaoa usijue ameshazaa
 
Familia kuongezeka yaweza kuwa tatizo, lakini tatizo kubwa hapa ni kuaminiana, sidhani kama mtoa mada atamuamini huyo mkewe kama alivyokuwa akimuamini kabla ya kujua kuhusu hao watoto.

Mkuu maswala ya kumwamini mwanamke weka mbali na moyo wako kwa manufaa ya afya yako
 
Jifunze kusamehe na chukua hatua ya kuwatunza hao watoto.

Huwezi jua Mungu atakusaidia vipi huko mbeleni katika maisha yako.
 
Hiyo ndo inaitwa kuingia kwenye MAHUSIANO bila kuwa na taarifa za msingi na muhimu za mwenzako, kwa sasa endelea KUSAIDIA maana watoto hawana makosa ndg
uchumba miezi miwili atajua wapi history ya maisha ya nyuma?
Huwa siku zote nawaamia vijana ndoa haianzi na uchumba na u boy friend /girl friend. Kwanza mnaanza kwenye urafiki wa kawaida kabisa usio na mahusiano yoyote ya kimapenzi, yaani mnapotoka mpo kama mtu tatu mpaka nne, just friends hapo inakuwa rahisi mtu kuongea kujihusu kwamaana anajua hakuna anayeweza mfanya kitu, mkishajuana kiundani ndo unakuja urafiki wa kimahusiano, mkishashibana ndo unakuja uchumba kisha ndoa. sio mnakutana kwenye sherehe kisha unampenda unaomba namba za simu, mnatoana out kisha mnaongea kuhusu uchumba ndani ya miezi miwili mko ndoani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom