Nimegundua mke wangu ana watoto wawili nje

Dec 6, 2017
14
45
Lakini ana watoto wawili, na nimekaa nae miezi minne lakini sikuwahi kujua kama ana watoto,

Nimekuja kujua kama ana watoto baada ya mtoto wake kuugua na kuhitaji msaada wangu kwaajili ya matibabu,

Upendo umepungua from higher to lower point,

Naomba kuwasilisha ushauri wenu ni muhimu wadau.
Akili ndefuuuuhttp://
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,113
2,000
Waswahili walisema kwamba, ukipenda Boga......sasa hayo ndio yakukufanya upende tena, kwani utamu umepungua??
 

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,314
2,000
Lakini anawatoto wa wili, na nimekaa nae miezi minne lakini sikuwahi kujua kama ana watoto, nimekuja kujua kama anawatoto baada ya mtoto wake kuugua na kuhitaji msaada wangu kwaajili ya matibabu, upendo umedencrease from higher to lower point, naomba kuwasilisha ushauli wenu ni muhimu wadau. Akili ndefuuuu

dah.....huu msala.....
sasa alificha watoto wa nini.......?......
 

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
4,610
2,000
Ni kweli kuwa ukipenda boga penda na UA lake lakini, huyo mwanamke si muaminifu na inawezekana kuna mengi nyuma ya pazia anayaficha.
Alitakiwa akueleze ukweli tangu mwanzo ili wewe mwenyewe ufanye maamuzi kama kuishi nae au la.

Chamsingi kaeni myamalize,msameheane lakini unatakiwa kumuonya abadilike kama kweli mnaipenda ndoa yenu.
Dawa ya ndoa ni msamaha.
 

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
17,934
2,000
Hiyo ndo inaitwa kuingia kwenye MAHUSIANO bila kuwa na taarifa za msingi na muhimu za mwenzako, kwa sasa endelea KUSAIDIA maana watoto hawana makosa ndg
Wanawake wengi wanaficha hilo la kuwa na watoto na vigumu sana kujua.

Mimi napenda mwanamke muwazi hata kama ana watoto 20 nje aseme mapema.
Duh makubwa inamaana pindi unatongoza ulikuwa Ujui historia yake pole mkuu vumilia tu amna namna sasa saidia tu
 

jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Jan 23, 2013
5,374
2,000
Kama ni mimi hapo hakuna kuyamaliza wala nini nampiga chini,

Yeah nampiga chini watoto ninkitu kikubwa sana ilitakiwa niwe na taarifa toka mwanzo,

She is a killer huyo anaweza kukuua kama aliweza kuficha jambo kubwa na muhimu kama hilo kwa mustakabal wa ndoa yenu,

Alifikiria haitafahamika mwanamke huyo piga chini
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,920
2,000
Lakini anawatoto wa wili, na nimekaa nae miezi minne lakini sikuwahi kujua kama ana watoto, nimekuja kujua kama anawatoto baada ya mtoto wake kuugua na kuhitaji msaada wangu kwaajili ya matibabu, upendo umedencrease from higher to lower point, naomba kuwasilisha ushauli wenu ni muhimu wadau. Akili ndefuuuuhttp://
mwaka wa nne wa ndoa yako ndio uje uyaseme hayo
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
18,407
2,000
Once trust has broken ndiyo basi tena....

They say:trust is like a mirror, you can fix it if its broken.But you can still see the crack in that reflection
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,300
2,000
Huyu mwanamke anakupenda sana, kukuficha kuhusu watoto aliogopa kukupoteza na inaelekea hana confidence na life.

Mueleze haya uliyoandika hapa na myamalize kwa mechi bora kabisa weekend hii.

Kumbuka duniani hakuna malaika na hata wewe una mapungufu yako.
 

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
17,934
2,000
Kama ni mimi hapo hakuna kuyamaliza wala nini nampiga chini,

Yeah nampiga chini watoto ninkitu kikubwa sana ilitakiwa niwe na taarifa toka mwanzo,

She is a killer huyo anaweza kukuua kama aliweza kuficha jambo kubwa na muhimu kama hilo kwa mustakabal wa ndoa yenu,

Alifikiria haitafahamika mwanamke huyo piga chini
Kweli Kabisa.
 

Shadeeya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
40,383
2,000
Pole sana Mkuu sababu kwa usawa huu halafu itokee ghafla familia inaongezeka naona ni bonge la mtihani aiseee. Hapo hakuna jinsi kaa naye mjue namna ya kutunza hao watoto na sio kuchukua maamuzi ya kuachana sababu ndio wanavyofanya wanaume walio wengi pindi vinapotokea vitu kama hivyo.

Ila huyo mwanamke naye kiazi.
 

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
4,610
2,000
Pole sana Mkuu sababu kwa usawa huu halafu itokee ghafla familia inaongezeka naona ni bonge la mtihani aiseee. Hapo hakuna jinsi kaa naye mjue namna ya kutunza hao watoto na sio kuchukua maamuzi ya kuachana sababu ndio wanavyofanya wanaume walio wengi pindi vinapotokea vitu kama hivyo.

Ila huyo mwanamke naye kiazi.
I see you
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom