Uchaguzi 2020 Nimegundua hizi kampeni zinafanyika kwa upendeleo “hazina usawa”

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Katika kampeni zinazoendelea, nimeona zinakibeba chama cha mapinduzi kwa sehemu kubwa, kwani viongozi wanaogombea bado wanako madarakani na wamekuwa wakiendelea kutoa maagizo kwa mamlaka zilizo chini yao,

Mfano: Unakuta mgombea urais anatoa maagizo ya kujenga barabara na pia kutoa pesa hadharani kama zawadi, Makamu wake akiagiza halmashauri kuongeza pesa za mikopo kwa vikundi mbalimbali, huku Waziri mkuu akiagiza kurejeshwa kwa baadhi ya mashamba huko Singida.

Hivi hao wapinzani wakitoa misaada wakati huu wa kampeni si watachukuliwa wanatoa rushwa?

Natamani katiba ibadilike tu, kikifika kipindi cha kampeni kila aliyekuwa na madaraka avuliwe ili waingie uwanjani wakiwa katika kiwango kimoja tofauti na sasa.
 
Pale tume kuna yule sijui mjita au mkurya anaitwa mahela, yaani ushabiki wake kwa ccm haufichwi kamwe.Leo katishia kumsimamisha lissu kwenye kupiga kampeni kisa eti katishia kuvunja amani, wakati magu kanda ya ziwa katwanga kilugha mwanzo mwisho kinyume cha maadili ya tume. Tume wako kimya tu
 
Ugunduzi wako umekusaidia nini,kama sio kupoteza muda tu kwa kulalama kama kawaida yenu. CCM mbele kwa mbele.
 
Pale tume kuna yule sijui mjita au mkurya anaitwa mahela, yaani ushabiki wake kwa ccm haufichwi kamwe.Leo katishia kumsimamisha lissu kwenye kupiga kampeni kisa eti katishia kuvunja amani, wakati magu kanda ya ziwa katwanga kilugha mwanzo mwisho kinyume cha maadili ya tume. Tume wako kimya tu
Mtu kuongea lughs yake kuna tatzo?
 
Naona unalalamika tu bila kuja na alternative,

Jambo hili lipo dunia nzima Rais anabakia kuwa madarakani na ni mgombea.
 
Umenena sahihi kabisa, sasa wazani ni kina nani wenye nguvu ya kusababisha hayo mabadiriko kwa sasa kama sio wananchi?

Walio kwenye mfumo hawako tayari na wanajitahidi kuzima jitihada za walioona hayo ili waendeleze mfumo wao. Wenye option ya mwisho ili tuachane na maigizo haya yote ni wananchi.

Siku watakayoamua kwa dhati kwa mustakabari wa maslahi mapana ya nchi hii na si kwa kikundi flani chenye kutetea mfumo uliopo bhasi ndipo utakapokuwa mwanzo wa msukumo wa kweli kuelekea kwenye maendeleo ya haraka.
 
Pale tume kuna yule sijui mjita au mkurya anaitwa mahela, yaani ushabiki wake kwa ccm haufichwi kamwe.Leo katishia kumsimamisha lissu kwenye kupiga kampeni kisa eti katishia kuvunja amani, wakati magu kanda ya ziwa katwanga kilugha mwanzo mwisho kinyume cha maadili ya tume. Tume wako kimya tu
Mahela ni msukuma
 
Pingapinga Cha Domo mpaka mjambe cheche
8b8772af65a848b2211cc750a1e7211b.jpg
 
Ina maana haujaona wapinzani wakiomba michango toka kwa wananchi waliotoka kuwaita masikini muda mfupi uliopita. Huoni kama huo nao ni ujambazi wa kisiasa?
 
Back
Top Bottom