Nimegundua Gwajima ni mwoga, mnafiki na mwepesi mno!

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
25,854
35,992
Nlitegemea baada ya rais kumkingia kifua ndugu Makonda, basi Gwajima angeelekeza mashambulizi yake kwa rais. Lakini katika ibada ya jumapili ya jana eti anawaambia watu waache kumsumbua rais, badala yake wamuunge mkono rais ila bashite asiungwe mkono!

Ameendelea kusema, mamlaka ya rais hayahojiwi na asisumbuliwe!

"Tumuunge mkono mheshimiwa rais, na kuanzia leo nisisikie mtu akimshutumu na kumsumbua mheshimiwa rais. Tumuunge mkono, tumwombee mh. Rais, lakini bashite asiungwe mkono hapanaaa"

Inajulikana wazi Makonda yuko pale kwa mamlaka ya rais, sasa yeye si anajiita jasiri? Kwanini asipige pale panapompa jeuri Makonda?

Gwajima acha unafiki na uoga!
 
Sikutegemea kama kuna mtu anaakili za kuandika ushuzi kama huu, kwani gwajima alisema tumuunge mkono raisi katika kumtetea bashite au? Kwa hiyo hata wapinzani kwako wakisema tumuunge mkono raisi unatasfiri ni woga? Gwajima kashafanya part yake imetosha, sasa kama ulienda kanisani jana kusikiliza habari za bashite basi mekula kwako. Kuna mijitu inapenda kusikia kauli za kishari shari ndio inafurahi
 
Kweli kabisa, ni bora angeendelea kumshambulia Makonda, asimtaje raisi, kuliko kujifanya raisi ni msafi makonda ni mchafu. Unafiki ni kujua kitu kipo hivi, alafu unasema kinyume chake. Gwajima anaelewa kabisa raisi na makonda ni kitu kimoja, alafu leo uwatenganishe, huo ni uwoga na unafiki.

Nadhani amesahau kuwa wanafiki hawata kwenda mbinguni.
 
Sikutegemea kama kuna mtu anaakili za kuandika ushuzi kama huu, kwani gwajima alisema tumuunge mkono raisi katika kumtetea bashite au? Kwa hiyo hata wapinzani kwako wakisema tumuunge mkono raisi unatasfiri ni woga? Gwajima kashafanya part yake imetosha, sasa kama ulienda kanisani jana kusikiliza habari za bashite basi mekula kwako. Kuna mijitu inapenda kusikia kauli za kishari shari ndio inafurahi
Inaonekana hujaelewa nlichoandika!

Umeshaona adui yako humpati kwa sababu kuna shimo kajificha humo, kachimbue hilo shimo sasa!
 
Back
Top Bottom