Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko Rais wao?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,300
Wanabodi,
Ni ajabu Watanzania kuamini maneno haya ya Mchungaji Gwajima.

Kuliko kukiamini kiapo hiki mbele ya Rais wa JMT, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli


Ni ukweli usiofichika watu wana mwamini zaidi Mchungaji Gwajima na uongo wake kumhusu Makonda kuliko wanavyo mwamini rais wao na ukweli wake kuwa Makonda is clean, hajaghushi cheti chochote wala hajafoji jina!. Rais Magufuli anasema Makonda ni safi hana tatizo lolote la kughushi kwa kutumia lugha ya matendo ambapo ni kutamka not expressly kwa kauli but impliedly kwa matendo ya kutofanya chochote tangu kuibuka kwa tuhuma hizi hivyo ku imply Makonda is clean na tuhuma ni za uongo! .

Kuna ule msemo usemao "you can fool some people for sometimes but you can't fool all the people all the time" ukimaanisha unaweza kuwadanga baadhi tuu ya watu kwa wakati fulani au kwa muda fulani tuu lakini huwezi kuwadanganya watu wote na kwa wakati wote au mara zote na siku zote, lakini Watanzania ni watu wa ajabu kweli, unaweza kuwadanganya wote wakati wote!. (Taking JF as sampling ya Watanzania wote).

Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hili swali "how does it come the same people wanachaguliwa katika chaguzi mbalimbali kwa kuja na ahadi kem kem, mwisho wa siku, wanashindwa kuzitekeleza walichoahidi na bado wanawarudia tena watu wale wale na ahadi nyingine kem kem za uongo na mnawachagua tena?! .

Yaani watu wanawadanganya all the people all the time na bado tunawachagua tena na tena na tena na 2020 tunawachagua tena!. Kipindi cha uchaguzi niliwahi kuuliza swali hili, sikupata majibu ya kuridhisha.

Hii kadhia ya Mkuu wetu wa Mkoa kusingiziwa uongo, imenifundisha kitu. Watanzania ni watu wa ajabu sana, ni warahisi kudanganywa na kudanganyika kirahisi!. Ni wepesi kupiga kelele kulalamika na wepesi wa kusahau!, hivyo soon hata hili la Makonda ni kama upepo tuu, soon litapita na watu watasahau na maisha yataendelea.

Juzi kati Mchungaji Gwajima aliibuka na tuhuma nzito za uongo wa mchana kweupe na kumsingizia Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda kuwa amefoji vyeti baada ya kuiba cheti chenye jina la Paul Christian na kujifanya ndio yeye (kutumia cheti cha mtu mwingine ni wizi hata kama huyo mtu alikupa) na akafoji kuvitumia kusomea hadi chuo kikuu na kupata ajira ukiwemo uteuzi wa rais wa JMT kuwa DC na sasa ni RC. Mchungaji Gwajima akadai kuwa jina halisi la Makonda ni Daudi Albert Bashite. Uongo huo haukuishia hapo bali alidai kuwa anavyo vyeti vya Daudi Bashite aluvyozungusha (vinavyoonyesha alipata Division 0) na pia anavyo vyeti vya Paul Christian ambavyo Daudi Bashite aliviiba na kuvitumia kama vyake.
Baadhi ya sisi wenye imani haba, kama Tomaso tulionyesha kutomwamini Mchungaji Gwajima kwa kumuita ni muongo hadi pale atakapoonyesha hivyo vyeti alivyodai anavyo ili tuvione ndipo tuamini. Kwa nini watu wanamtaka Makonda ndio aonyeshe vyeti ili hali kuna mtu amedai anavyo?!. Nilidhani watu humu wangemdai vyeti Mchungaji Gwajima aliyesema anavyo ndio aonyeshe. Vyeti vya Makonda viko kule vinakopaswa kuwepo kwenye mamlaka yake ya ajira kwa mtu aliye mteua.

Kitu cha ajabu sana Watanzania wengi wamemwamini Mchungaji Gwajima aliedai ana vyeti, (ambavyo naamini hana mpaka atakapovionyesha), huku rais wa JMT ambaye ana nakala halisi za vyeti hivyo katulia tuli, hivyo sio tuu wanamshinikiza Makonda aonyeshe vyeti vyake bali hadi kushinikiza ajiuzulu au atumbuliwe! . Ajiuzulu kwa kosa lipi au atumbuliwe kwa lipi? .

Gwajima ni Muongo?.
Kitendo cha kuhubiri uongo na kudanganya kuwa una ushahidi lakini huutoi huo ushahidi ni uthibitisho tosha ule ulikuwa sio uongo tuu wa mchana kweupe?.

Bahati yake Makonda sio tuu ni Msukuma ambapo Wasukuma hawana makuu na wana madharau sana, hivyo amemdharau, bali pia Makonda ni Mlokole hivyo amemshitakia kwa Mungu tuu na sio kwa binadamu, akalia machozi madhabahuni na kusamehe.

Kwa Nini Gwajima ni Muongo? .
Kiongozi yoyote kabla ya kuteuliwa na rais, hufanyiwa vetting hivyo vyombo vya serikali vinazo taarifa zote sahihi kumhusu Makonda. Sasa ni ajabu sana kwa Watanzania kumwamini mtu anayezungumzia hewani tuu na kuacha kuiaminia vetting yenye vyombo vya dola vya uchunguzi? . Kutoiamini vetting ya serikali ni kutomwamini rais Magufuli!. Imani ya Magufuli kwa Makonda is based on vetting, jee nyinyi mnao mwamini Mchungaji Gwajima, imani yenu kwa Gwajima iko based on what?!.

Sasa tangu kutolewa kwa uongo huu, ungekuwa una hata chembe ya ukweli, tungeshuhudia hatua zikichukuliwa dhidi ya udanganyifu huu. Rais Magufuli alipochaguliwa alituhakikishia atatuletea watu makini kabisa na Makonda ni mmoja wa makini hawa. Iweje Gwajima amkosoe makini wa rais wetu na watu mkamwamini?!.

Kitendo cha mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi ya Makonda ni uthibitisho tosha kuwa vetting ilifanyika vizuri, jina la Paul Christian Makonda ni jina lake halisi, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Na vyeti vyake ni vyeti vyake halisi ambavyo viko kwenye mamlaka yake ya uteuzi, hivyo Paul Makonda hapaswi kumuonyesha mtu yoyote vyeti vyake ili tuu kujibu uongo wa Gwajima.

Kitendo cha kumsingizia uongo mkubwa kama huu mteule wa rais ni kuidhalilisha taasisi ya urais kwenye vetting, ambapo ni sawa na kuidhalilisha rais kuwa amefanya uteuzi wa watu bogus!. Huu pia ni uchochezi, ila bahati yake Mchungaji Gwajima, amekuta jeshi letu la polisi liko automatically tuned kubaini uchochezi toka kwa watu fulani fulani tuu mfano Tundu Lisu, Lema and the like, vingenevyo Gwajima saa hizi angepaswa nae kushitakiwa kwa uchochezi!. Yaani mtu anazungumza public kuwa rais ametuteulia mtu fake na bado anaachwa hivi hivi?!.

Sisi Watanzania wote katika umoja wetu ndio tuliomchagua kwa kura nyingi, Dr. John Pombe Magufuli awe rais wetu, kama rais wetu amemwamini Makonda based on vetting, who is Gwajima kutuletea uongo based on nothing na watu humu wanamwamini.

Wewe ambaye unajiita ni Mtanzania mzalendo, unawezaje kumwamini Gwajima based on nothing kuliko unavyo mwamini rais wako mwenye vyombo vyote vya dola?.

Nikikuuliza kati ya uongo wa Gwajima kuwa Paul Makonda ni Daudi Bashite na ukweli wa rais Magufuli kuwa Paul Makonda ni Paul Makonda ndio maana mpaka sasa ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wewe unamwamini nani? .

Shuhudia katika bandiko hili jinsi Watanzania walivyo watu wa ajabu, yaani wanamwamini Mchungaji Gwajima kuliko hata rais wao?! .

Utafiti huu umetumia kanuni ya probability sampling strategy kwa kuwatumia wana jf wanaochangia Jukwaa la Siasa as a sample ya kuwakilisha cross section ya Watanzania wote. Ukipandisha bandiko lolote kumtetea Makonda, posts za kukupinga ni nyingi kuliko posts za kukuunga mkono. Wapigaji hawa wanalazimisha Makonda tuu lazima aonyeshe vyeti kwa kumwamini Gwajima aliyesema ana vyeti. Kanuni ya tuhuma ni "he who allege must prove" nikimaanisha Gwajima anayetuhumu ndio aweke ushahidi wa hivyo vyeti alivyodai anavyo kisha ndipo mtuhumiwa ajibu. Magufuli ndie aliyemteua Makonda, vyeti viko kwa Magufuli, Magufuli mwenyewe kajiridhisha viko sawa kabisa ndio maana hajafanya lolote. Kisheria the burden of proof lies with the prosecution not the defense. Nilitaraji watu wampigie kelele Gwajima aweke ushahidi wake kwanza ndipo wamsulubu Makonda!.
Huu ni uthibitisho kuwa sisi Watanzania we don't think, ni rahisi sana kuaminishwa chochote based on nothing, na labda ndio maana hata kwenye chaguzi zetu, hatuchagui kwa kufanya informed decisions based on reasoning bali tunajichagulia tuu alimradi tumechagua kwa kufuata tuu mkumbo!.

When can we start to think, reason and make informed decisions kabla hatujaendelea kudanganywa tena na tena na tena?!. Yaani hapa watu wamedanganywa na Gwajima tuu na wameamini badala ya kushikamana ukweli halisi wa rais wao kwa mteule wake ni mtu safi kabisa, hajafoji jina lolote wala kughushi cheti chochote, vipi kuhusu wanasiasa?!.

Paskali.
 
Kwa Nini Gwajima ni Muongo? .
Kiongozi yoyote kabla ya kuteuliwa na rais, hufanyiwa vetting hivyo vyombo vya serikali vinazo taarifa zote sahihi kumhusu Makonda.
Kwani uliambiwa vetting ni Msaafu au bible,unaweza usikidhi vigezo lakini bado ukateuliwa kutokana na mtu anayetaka kukuteua ana kazi gani nawe!
 
Mchungaji wa mwenyezi mungu anatuma Mapepo yamuendee Makonda!!
huyu mchungaji wa mungu au shetani!!
Watanzania wanao Ipenda Tanzania na walio na uchungu na nchi yao Tanzania
hawawezi kumpinga na Kumkashfu Makonda,
hawa tunao waona leo ni kikundi cha Watu wasio na matendo mazuri walio amua kumchafua makonda
na kwavile wana mikono na nguvu za shetani lazima wasumbue japo hawata shinda wala kupenya.

Hii ni vita Na makonda anaijua kuwa ni vita ngumu
lakini kwakuwa Mungu husimama na watu wake Itakwisha vita hii.
 
Teh teh......kweli mkuu, tumuamini sana raisi maana mpaka sasa tuna viwanda vya kutosha, uchumi unakuwa kwa kasi ya ajabu, wanafunzi elimu ya juu wanapata mikopo mingine mpaka wananunulia magari, mishahara ya watumishi ipo juu, ajira ni nyingi mpaka waajiriwa wanakosekana, kilimo kinakuwa, rushwa imekwisha kabisa mpaka sasa tunatoa pesa ya kubrashi viatu vya askari nk.
Mara Mwanahalisi wamekuja na uongo mwingine.
Kweli ni mkweli kweli kweli, tumuamini.
 
Wanabodi,
Ni ukweli usiofichika watu wana mwamini zaidi Mchungaji Gwajima na uongo wake kumhusu Makonda kuliko wanavyo mwamini rais wao na ukweli wake kuwa Makonda is clean, hajaghushi cheti chochote wala hajafoji jina! .

Kuna ule msemo usemao "you can fool some people for sometimes but you can't fool all the people all the time" ukimaanisha unaweza kuwadanga baadhi tuu ya watu kwa wakati fulani au kwa muda fulani tuu lakini huwezi kuwadanganya watu wote na kwa wakati wote au mara zote na siku zote, lakini Watanzania ni watu wa ajabu kweli, unaweza kuwadanganya wote na wakati wote! .

Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hili swali "how does it come the same people wanachaguliwa katika chaguzi mbalimbali kwa kuja na ahadi kem kem, mwisho wa siku, wanashindwa kuzitekeleza, na bado wanawarudia na ahadi nyingine kem kem na mnawachagua tena? . Yaani wanawadanganya all the people all the time na bado tunawachagua?. Kipindi cha uchaguzi niliwahi kuuliza swali hili, sikupata majibu ya kuridhisha.

Hii kadhia ya Mkuu wetu wa Mkoa kusingiziwa uongo, imenifundisha kitu. Watanzania ni watu wa ajabu sana, ni warahisi kudanganyika na wepesi wa kusahau.

Juzi kati Mchungaji Gwajima aliibuka na uongo wa mchana kweupe na kumsingizia Makonda ameiba jina la Paul Christian, na ameghushi vyeti vya Paul Christian kujifanya ndio yeye na akafoji kuvitumia kusomea chuo kikuu na kupata ajira ukiwemo uteuzi wa rais wa JMT kuwa DC na sasa ni RC. Mchungaji Gwajima akadai kuwa jina halisi la Makonda ni Daudi Albert Bashite. Uongo huo haukuishia hapo bali alidai kuwa anavyo vyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha alipata Division 0 na pia anavyo vyeti vya Paul Christian ambavyo Daudi Bashite aliviiba na kuvitumia kama vyake.

Baadhi ya sisi wenye imani haba, kama Tomato tulionyesha kutomwamini Mchungaji Gwajima kwa kumuita ni muongo hadi pale atakapoonyesha hivyo vyeti tuvione ndipo tuamini.

Kitu cha ajabu sana Watanzania wengi wamemwani Gwajima, hivyo sio tuu kumtaka Makonda aonyeshe vyeti vyake bali hadi kushinikiza ajiuzulu au atumbuliwe! . Ajiuzulu kwa kosa lipi au atumbuliwe kwa lipi? .

Gwajima ni Muongo.
Kitendo cha kuhubiri uongo na kudanganya kuwa una ushahidi lakini huutoi huo ushahidi ni uthibitisho tosha ule ulikuwa ni uongo tuu wa mchana kweupe.

Bahati yake Makonda sio tuu ni Msukuma ambapo Wasukuma hawana makuu na wana madharau sana, hivyo amemdharau, bali pia Makonda ni Mlokole hivyo amemshtakia kwa Mungu, akalia machozi madhabahuni na kusamehe.

Kwa Nini Gwajima ni Muongo? .
Kiongozi yoyote kabla ya kuteuliwa na rais, hufanyiwa vetting hivyo vyombo vya serikali vinazo taarifa zote sahihi kumhusu Makonda.

Sasa tangu kutolewa kwa uongo huu, ungekuwa na ukweli hata chembe, tungeshuhudia hatua zikichukuliwa dhidi ya udanganyifu huu.

Kitendo cha mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi ya Makonda ni uthibitisho kuwa vetting ilifanyika vizuri, jina la Paul Christian Makonda ni jina lake halisi, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Na vyeti vyake ni vyeti vyake halisi ambavyo viko kwenye mamlaka yake ya uteuzi, hivyo Paul Makonda hapaswi kumuonyesha mtu yoyote vyeti vyake ili tuu kujibu uongo wa Gwajima.

Sisi Watanzania wote katika umoja wetu ndio tuliomchagua kwa kura nyingi, Dr. John Pombe Magufuli awe rais wetu, kama rais wetu amemwamini Makonda, who is Gwajima kutuletea uongo na kuuamini.

Wewe ambaye unajiita ni Mtanzania mzalendo, unawezaje kumwamini Gwajima kuliko unavyo mwamini rais wako?!.

Nikikuuliza kati ya uongo wa Gwajima kuwa Paul Makonda ni Daudi Bashite na ukweli wa rais Magufuli kuwa Paul Makonda ni Paul Makonda ndio maana mpaka sasa ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ubamwamini nani? .
Shuhudia jinsi Watanzania walivyo watu wa ajabu, yaani wanamwamini Mchungaji Gwajima kuliko hata rais wao! .

Utafiti na Sampling ya Watanzania.
Utafiti huu uko based on jf, kuwatumia wana jf kama cross section ya sampling ya Watanzania wote. Ukipandisha bandiko lolote kumtetea Makonda, posts za kukupinga ni nyingi kuliko posts za kukosoa.

Huu ni uthibitisho kuwa sisi Watanzania we don't think, name hata kwenye chaguzi zetu huwa tunajichagulia tuu kufuata mkumbo.

When can we start to think kabla hatujaendelea kudanganywa tena na tena na tena?!.

Paskali.

Sema CHADEMA siyo watanzania wote. ama at the very least sema baadhi ya watanzania
 
heeeeeh weee waajabu vetting ni machine gani iyoo ya kukoboa mpunga ama.......alaaaah

tunamwamin yeye ambae ameleta ushahidi wa vielelezo saa uyo raisi mwenyew kanyamaz kimya kama kafa

shoga maana kifo cha shoga ndo kimya kimya hakuna kulia.........

Basi ata mh, angetoa tamko lakin ndo kwanza yuko kimya alaf unaniambia nisimuamin gwajima uwezz kuwa ujalewa....tena yule mtumishi wa mungu unaweza kuta kaoteshwa kwamba jamaa kala buyu
 
Back
Top Bottom