michibo
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 2,212
- 3,656
Ndugu zangu!
”Ukitaka kufurahia maisha, tafuta mtu wa kumlaumu.” Nimewahi kuishi katika msemo huu, kisha nikaamka na nikajitafuta upya.
Sijui kama nitakuwa na maelezo mazuri ya kuliweka vizuri hili, si unajua kuna vile ‘vi-furaha vidogo vidogo’ ambavyo hata huwezi kumsimulia mwenzio!
Mfano ni pale mnakula wengi mezani halafu randomly ukaokota (pick) kiazi kitamu kuliko vingine vyote kabla yake, enhee kale ka-feeling niaje! Unatamani tu wengine pia wajue, bad enough huwezi kusema nao wala hawakuulizi.
Basi bhana kwenye maisha kila mtu hupambana kwa nafasi yake ili kujipatia maisha yenye furaha, nimekuwa kama mwingine yeyote yule.
Si haba nimekuwa nikafanikiwa kutimiza hata kama ni kwa uchache, ila ni vitu ambavyo niliwahi kutamani na kuweka nia. Lakini kila baada ya kutimiza moja, utafurahi siku hiyo tu au na chache zingine kisha kukiona si kitu.
Kila nililotamani kumiliki, likitimia sioni tena thamani yake kwenye maisha yangu. Ila pale inapotokea kumsaidia mtu, hata kama ni kwa kumpa moja ya ‘vitu’ nilivyovihangaikia kwa muda mrefu yaani najisikia furaha ile yenyewe kabisa.
Napambana kupata vitu kwa ajili tu ya ‘status’ na kuchora picha ya nje kwa wanaonifahamu, pengine wao wanatarajia zaidi kuniona katika picha ile, lakini binafsi siioni ikinibariki kwa vyovyote.
Nimekuwa nikichelewa kupiga hatua kubwa japo nafasi inaniruhusu, kisa tu muda mwingi na kwa gharama kubwa najikita kunufaisha wengine. Hii inaleta presha kubwa kwa wategemezi wangu wasiojua hasa nahitaji nini.
Maisha ni furaha, nashukuru nimekipata chanzo cha ‘maisha’ yangu.
Je, wewe furaha yako ipo kwenye nini?