Nimegundua furaha yangu haipo kwenye utajiri wa vitu, nikisaidia watu nakuwa na amani zaidi

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,551
2,000
Ndugu zangu!

”Ukitaka kufurahia maisha, tafuta mtu wa kumlaumu.” Nimewahi kuishi katika msemo huu, kisha nikaamka na nikajitafuta upya.

Sijui kama nitakuwa na maelezo mazuri ya kuliweka vizuri hili, si unajua kuna vile ‘vi-furaha vidogo vidogo’ ambavyo hata huwezi kumsimulia mwenzio!

Mfano ni pale mnakula wengi mezani halafu randomly ukaokota (pick) kiazi kitamu kuliko vingine vyote kabla yake, enhee kale ka-feeling niaje! Unatamani tu wengine pia wajue, bad enough huwezi kusema nao wala hawakuulizi.

Basi bhana kwenye maisha kila mtu hupambana kwa nafasi yake ili kujipatia maisha yenye furaha, nimekuwa kama mwingine yeyote yule.

Si haba nimekuwa nikafanikiwa kutimiza hata kama ni kwa uchache, ila ni vitu ambavyo niliwahi kutamani na kuweka nia. Lakini kila baada ya kutimiza moja, utafurahi siku hiyo tu au na chache zingine kisha kukiona si kitu.

Kila nililotamani kumiliki, likitimia sioni tena thamani yake kwenye maisha yangu. Ila pale inapotokea kumsaidia mtu, hata kama ni kwa kumpa moja ya ‘vitu’ nilivyovihangaikia kwa muda mrefu yaani najisikia furaha ile yenyewe kabisa.

Napambana kupata vitu kwa ajili tu ya ‘status’ na kuchora picha ya nje kwa wanaonifahamu, pengine wao wanatarajia zaidi kuniona katika picha ile, lakini binafsi siioni ikinibariki kwa vyovyote.

Nimekuwa nikichelewa kupiga hatua kubwa japo nafasi inaniruhusu, kisa tu muda mwingi na kwa gharama kubwa najikita kunufaisha wengine. Hii inaleta presha kubwa kwa wategemezi wangu wasiojua hasa nahitaji nini.

Maisha ni furaha, nashukuru nimekipata chanzo cha ‘maisha’ yangu.

Je, wewe furaha yako ipo kwenye nini?
 

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
928
1,000
Kiongozi; unabahati sana katika maisha kupata maono ya kuwasaidia wangine. Endelea hivyo hivyo kwani umebarikiwa na Mungu. ANGALIZO; uwasaidie watu wa hali ya chini/maskini wenye uhitaji wa kweli na sio kumsaidia mtu Blue tooth speaker; Iphone nk
Wape mitaji midogo midogo na hata chakula (Kwa kadri Mungu anavyokubariki) ......nakuhakikishia huwezi kuishiwa kwani Mungu atakuwekea Mkono wake juu yako
Ubarikiwe sana!
 

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,551
2,000
Kiongozi; unabahati sana katika maisha kupata maono ya kuwasaidia wangine. Endelea hivyo hivyo kwani umebarikiwa na Mungu. ANGALIZO; uwasaidie watu wa hali ya chini/maskini wenye uhitaji wa kweli na sio kumsaidia mtu Blue tooth speaker; Iphone nk
Wape mitaji midogo midogo na hata chakula (Kwa kadri Mungu anavyokubariki) kwa ajili ya kuendesha maisha yao...
Unarikiwe sana!
Asante mkuu.
 

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,551
2,000
Kama una mke, vipi ana behave vipi ukiwa unasaidia maana hii huwa inawaletea shida sana wanawake pale mume anapokua mto msaada sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mtoa misaada sana na sitoi kwa ukubwa mno kiasi cha kuripoti au kustukiwa na mke, ndo maana nikatoa mfano wa vifuraha vidogo vidogo.

Kipato chenyewe ni hiki hiki cha kuungaunga, ni kugawana tu na wengine wenye uhitaji sawa au zaidi ya mimi. Mradi napata amani.

Familia ina nafasi yake na ndo msingi wa kupambana, sema ndo vile baadhi ya mambo yanachelewa utakelezaji kwa ku-disturb budget kwa ajili ajili ya wengine!
 

Michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
1,551
2,000
Pia usisahau sana kuendeleza urithi wa watoto wako na mke wako, i mean msaada fanya kwa average haitakua na maana unatoa msaada sana wakati nyumbani hali hujaacha nzuri, charity begins at home

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa hili nakubali mkuu, hili ni tatizo ninalohitaji kulibalansi. Siwezi kutoa kiasi cha kutelekeza nyumbani ila siko vizuri kwenye kuweka ziada kama akiba, hii sasa ni hatua inayofuata.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom