Nimegoma Kuwa Mnyonge Mbele ya Polisi

chamng'asi

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
211
385
Nawasalimu! Tarehe 25/7/2022 nikiwa mizungukoni nilisimamishwa na Askari wa usalama barabarani wakaniomba leseni nikatoa kisha wakaikagua gari na kubaini sina dosari kisha nikaruhusiwa kuendelea na safari zangu.

Kesho yake tarehe 26/7/2022 nikiwa na familia yangu yaani mke na watoto wawili mahali fulani nilikutana na askari wa usalama barabarani wapatao 7, Wakanitaka niweke gari pembeni nikatii , Wakaitaka leseni nikawapa, Mmoja akaizunguka gari kisha akaja dirishani na kuniambia tairi moja imeisha hivyo nishuke garini ili waipeleke kituoni.

Shida ikaanza nilipomwambia mkuu mbona jana tu nilionekana sina tatizo lakini leo tayari tairi imeisha? Akanijibu vibaya kidogo nikaona niwe mpole, Nikamuomba niifikishe familia kisha nitaenda mwenyewe kituoni akagoma akawa mkali, Nikamuomba anipe muda mfupi ili nilifanyie kazi tatizo Akakataa na Kulazisha tushuke garini ili ipelekwe kituoni.

Kama baba Mbele ya Mke na Watoto sikuiubali Unyonge kwani Wazi Niliona Sitendewi haki, Nilishindwa kujizuwia nikamwambia Afande kusema Ukweli hakuna mtu yeyote atakayeshuka kwenye gari na Wewe au mwingine yeyote hapa hataendesha gari yangu.

Hali ikawa tete, Askari wawili wakapandisha Mori lakini kwa hakika Nilivurugwa kidogo kisaikolojia kwa wakati ule Nikawaambia wakati wowote kuanzia sasa endapo yeyote atanigusa au kufanya tofauti na maelezo yangu Hakika jambo baya sana litaenda kutokea. Mimi ni Mhehe original na kwa wakati ule nilijiona naenda kuacha historia mbaya muda wowote. Kwa Ufupi nilidhamiria kufanya jambo baya sana.

Wife anajua kuwa mimi sio mkorofi lakini nikifika kwenye point of no return huwa nakua mnyama, hivyo alishuka akawasihi wanitreat kwa tahadhari, nadhani kuna mmoja aliniangalia akajua sitanii na baada ya kujumuisha maneno ya wife akaona hapa tutaharibu hali ya hewa, Akaanza kuwasihi wenzake watulie kwanza ili yeye asolve ishu lakini hakufanikiwa.

Kufupisha ni kwamba Wawili walikomaa wakakaa garini na kunitaka nifuate maelekezo yao lakini nilivurumusha gari mpaka Ofisi za Polisi za Mkoa Nikashuka na Kuelekea Ofisini kwa RCO jamaa wakawa hawaelewi wakanifuata. Mwisho wa Yote niliacha kizaazaa kati yao na RCO. Walifokewa mno mbele yangu kwakuwaa maelezo yao hayakuwa na maana. Kitu nilipenda ni pale Walipoambiwa kuwa

"Mtakuja kufa kijinga nyinyi Watu Wamevurugwa na Maisha Na nyie mnawaletea fedheha mbele ya familia zao"

Niliambiwa niendelee na safari zangu na niachane na lolote waliloniambia wale askari, Nikawasha gari nikaondoka. Jana nimepita njia fulani nikamkuta mmoja kati ya Wale askari aliponiona aliniambia Bro mji mdogo huu tutaona mimi na wewe nani mjanja. Hii kauli imenifikirisha sana, Hebu nishaurini nifanyaje aisee manake naanza kuona dalili za kutokea kwa yale ya Iringa enzi zile za Yule mkuu wa mkoa na yule Mkulima. Nadhani nimeeleweka.

Nawasilisha.
 
Ulitaka uwa Mwamwindi

Aseeh hapo ulipo ghafirika kama nakuona, nna bro wangu mmoja akipata moto wa kumtuliza huwa ni jamaa yake mmoja.

Mkuu usimpuuze huyo jamaa maana askari Wana akili ndogo mno (hawana akili kabisa hata hii ndogo nayo hisi wanayo) nenda Katoe taarifa kwa mkubwa wao ama mpige biti mara 2 ya biti la kwanza

Tofauti na hapo lazima akuundie zengwe la kibwege sana
 
yaani gari ya kwangu, alafu mtu apande bila ridhaa yangu, zaidi sana anidhalilishe mbele ya mke wangu na watoto. hilo siwezi kulikubali. binafsi traffic akinisimamisha huwa namsalimia akisema anataka kukagua gari namwambia karibu, kagua.

Akiomba leseni uwa namwambia nimeiacha ofisini au nyumbani ila ninayo (kisheria unaruhusiwa kuipeleka ndani ya siku mbili), na sishuki kwenye gari.

Sasa atasema nishuke kwa ajili ya nini?na milango nimelock ataingiaje? aongelee pale dirishani akimaliza kwisha. kama hajipendi sana basi anizuie wakati mimi nimekaa pale usukani na gari inaunguruma.

Wanaangaliaga sura pia wakiona mjinga mjinga ndio wanakunyanyasa, wakiona huyu kichwa kina akili huwa wanajiongeza.

Nikiwa na mke wangu na watoto heshima ile huwa nailinda kuliko hata pesa. huwezi kunidhalilisha mbele ya mke au watoto wangu. huwezi.
 
shida moja ni kwamba, jamaa alifanya ujinga wa kushuka kwenye gari. kati ya ujinga hutakiwi kuwafanyia polisi ni kushuka kwenye gari, kuwapa ufunguo, na kuwapa leseni. hatari nyingine ni kwamba, ukishafura ukawatishia kama alivyofanya yeye hapa, umewapa justification ya wato kukutreat kama mtu hatari.

Yaani kama wao wanatembea na bastola, manake wanaweza kukushuti kwasababu umewatishia na pengine wanahisi na wewe una mguu wa kuku, si ukute ukawa unajikuna tu kiunoni wakajua unawavizia uwalenge wakakupa ya kichwa.

ni kosa kubwa kumtishia polisi. we ongea naye maneno ya kawaida akikuzingua washa gari ondoka zako, akianza kukufukuza nenda tu kituo cha polisi au kama una mawasiliano na wakubwa zake wapigie adhalilike.
 
Back
Top Bottom