Habari wakuu
Wazee wamekuwa wakinishauri sana kwa namna kama ya kuni-force nitafute mchumba nioe sijakataa nimewaomba wanipe mda wa kujishauri na kuangalia wa kuendana nami nifanye mpango wa kuoa.
Nimekuwa safari kwa mda mrefu na hapo mtaani kwetu kumekuwa na michezo ya ovyo wakihisi una vijipesa; sasa naona nisimame kidogo maswala ya kutafuta mchumba kwa ajili ya kuoa kutokana na hizi mambo zinazoendelea kunitokea kiuhalisia sio mtu wa kubadili badili wanawake ninapopata tulizo na nikiwa bize kama Sipo katika mahusiano napumzikaga kabsa, now nimerudi mtaani na baadhi ya watu wanahisi kuwa nina vijipesa simu zimekuwa nyingi kwa wadada na baadhi ya wengi wao wapo kwenye ndoa zao..
Na lengo lao kuu ni kunipa penzi ili niwape pesa kinachonichanganya akili ni wadada wazuri ambao wapo kwenye ndoa zao wengi wao na kwa kuangalia kwa macho kwa kawaida wanaonekana wanawapenda waume zao na maisha yanaenda vizuri tu yaani mahitaji yale ya kuonekana wanayapata uzuri tu najiuliza tatzo nini? Kinachowafanya watafute wanaume kwa ajili ya kuwapa penzi ili wapatiwe pesa “” kwa kweli siwezi kufanya ujinga huo hali ya kuwa najua fika kuwa wapo kwenye ndoa zao “” sio maadili yangu na swali lingine itawezekana kweli kwa mke wangu ntakayemuoa naye akapata matamanio ya vijipesa akataka atembee na mwanaume ampe pesa.. kichwa kinauma sana..
Nimepanga niwaombe wazee wanipe miaka kama mitatu mbele ili nipate utulivu kidogo kwenye kutafuta mtu sahihi na sio kukurupuka kwa wao kutaka kwa haraka hivyo”” kwanza mtu wa ndoto zako atafutwi unakutana naye tu.. M/Mungu atabariki InshAAllah .. sitaki kusema nawadharau wazazi ila nawaheshimu sana kuwaletea mtu sahihi asiyekuja kuwakwaza wasinipe baraka zao kisa mtu mwingine.. nawapenda sana wazee wangu..
Inabidi utulize sana akili kabla ya kutafuta mtu wakuishi nae katika ndoa “ na kuomba sana M/Mungu akujaalie/akupe mwema uinjoy maisha haya mamali na mapesa, majumba hayafai kama utakuwa na mwenzako mkorofi katika ndoa yenu.
M/Mungu awabariki..