Nimeghairi kumpatia ujauzito Shamsa baada tu ya kukutana na mabinti wawili wakikicharanga kimombo

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Mipango yangu mimi pamoja na Shamsa imeingiwa kidudu maji. Tulipanga kupeana ujauzito, kisha tumtunze mwanetu mpaka pale atakapofikisha umri wa kwenda shule ili tumnunulie kiufagio na kidumu cha lita 5 akaanze vidudu, aje kutusaidia baada ya miaka 20 ijayo

Baada ya kukutana na hawa mabinti wawili aged 12 years (approximately) wakikicharanga kimalkia, nimejikuta nashikwa na aibu kali sana. Akili inenituma nitafute hela kwanza hata kama nitazipata nikiwa na 50 yrs, ndipo nimbebeshe mwanamke ujauzito

Ni kosa kubwa sana kuleta kiumbe duniani eti kijipambanie. Yale mawazo ya kila mtoto huja na bahati yake yamepitwa na wakati. Wazazi wetu walifanya makosa, hivyo hatupaswi kurudia makosa
 
Kwenye kichwa chako kiingereza ndiyo maendeleo? Bonge la mshamba sana wewe
 
Kwa level ya elimu ya msingi, kingereza hufundishwa kwenye shule za kulipia pesa ndefu, na ndiko ambako mtoto anasoma kwa raha sana huku akifurahia ujio wake duniani. Ndiko malezi bora kutoka kwa walimu yanakopatikana. Mtoto anafundishwa elimu ya darasani na stadi za maisha, anafundishwa kujiajiri. Sasa wewe kosa hela uone kama mwanao hatokwenda kusomea Shule ya Msingi Matuyuyu. Ama Mtombezane Primary School. Unadhani kipi cha maana atakipata tofauti na mafua ya vumbi la msimu, kukaa chini ama kuangukiwa na vumbi la chaki?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom