falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,288
Wakuu habari,
Naomba moja kwa moja niwe mkweli juu ya hisia zangu kuwa nimefurahia mno utenguzi wa Nape kwenye nafasi yake ya uwaziri.
Sababu moja wapo ya furaha yangu ni kuwa sasa Nape ndio amepata rasmi muda wa kujifunza kuwa zile figisu alizozifanya ambazo baadae alikuja kukiri na kuomba msamaha kwa wapinzani leo figisu hizi zimemrudia mwenyewe.
Naamini Nape hakufurahi kutumbuliwa wala hakutegemea hata kama baadae atakuja kuonyesha ushirikiano na CCM wenzake.
Nape huyu huyu ndiye aliyetuletea bao la mkono na bao la mkono hilohilo limemrudia yeye ndio maana leo imekuwa siku ya furaha.
Kingine nilichofurahia kutumbuliwa kwa Nape ni sababu kuna wale watoto wa bongo fleva na bongo movie kama sikosei walitengenezwa na Nape huu ndio wakati wao kujulikana yupi ni CCM kweli yupi ni CCM maslahi.
Kwakweli nimefurahi lakini nimesikitika zaidi kwani Nape ameondolewa kipindi ambacho anaanza kujitambua kuwa yeye ni nani mbele ya jamii.
Jumamosi nitafunga safari hadi kwenye ofisi za CCM tawi fulani kwa wakubwa ili kupata update zote za siri za chini kwa chini zinazofukuta maana kuna ndoto niliiota sasa wanaenda kunitafsiria maana ya ndoto hiyo.
Salaam toka Mombasa Kenya