Ambaye yupo fukayosi naomba tuwasiliane na mimi nimeanza kilimo cha nanasi, nimefanya geo-physical survey ya maji kupitia wale jamaa walio karibu na chuo cha maji, pia ninampango wa kutengeneza bwana la maji ili nikinge maji ya mvua. Tayari nimeishapanda nanasi ekari 12 na mpango wangu ni kufikisha ekari 30 ifikapo mwezi wa 6 mwaka kesho.
Changamoto kubwa niliyoiona Fukayosi na nguvu kazi hasa vijana ni wazembe sana ila kiboko yake ni kwamba uwe unaenda shambani mara kwa mara kwa safari za kushitukiza na uwe mkali. Kingine usiwazoeze kuwapatia pesa mara kwa mara kila unapokubaliana nao kazi maana kuna wengine wanasema eti ukipatana nao uwape advance kwanza mimi ilo nimelikataa na sasa wameishazoea.
Mengi tutawasiliana zaidi...
Je uko fukayosi sehemu gani??