Nimefarijika sana na site hii, naomba ushauri wa mazao ya muda mfupi Fukayosi!

chidide

Member
Nov 11, 2010
91
9
Wakuu nimefarijika sana kutembelea site hii ya business! Mimi nimekuwa natembelea sana jukwaa la siasa na lazima niseme ukweli ilifika kipindi nikaachana na jamii forums. Leo nimefarijika sana kuja huku na kukutana na wana JF ambao wana new ideas na bado hamjakuwa corrupted na wanasiasa. Sasa naimba ushauri kuhusu kilimo cha mazao ya muda mfupi maeneo ya Fukayosi Bagamoyo, nimeamua kuwa mkulima but bado sina details nyingi za kilimo cha mazao ya muda mfupi maeneo ya fukayosi na maeneo ya chalinze! Naomba ushauri please!!!
 
Thanx KA, Mananasi ni up to 2 years! Nataka mazao ambayo hayachukui zaidi ya miezi sita na ambayo soko lipo!
 
mkuu chichide ... karibu sana huku

mawazo yako ni mazuri sana na waweza ukapata mafanikio makubwa sana kiuchumi ..... cocern kubwa hapa ni rasilimali maji ambayo ndiyo tegemezi la mafanikio ya kilimo ..... kilimo cha muda mfupi maana yake utategemea kulima vipindi viwili au vitatu kwa mwaka hivyo basi utahitajika umwagiliaji

kilimo cha kutegemea mvua kwa kudura za mwenyezi mungu ni kigumu sana .... mara nyingi mvua haswa huwa ni chanzo tu cha kuongeza maji katika mito mabonde, maziwa n.k ambavyo vyote hivi ndivyo vyanzo tegemezi vya maji na ndivyo tunaweza kutegemea kuvitumia kuwa na kilimo bora kwa kufanya umwagiliaji ... vinginevyo kunauwezekano wa kupima water table ya ardhi yako na kuchimba maji kitaalam na kufanya umwagiliaji

hapo Fukayosa unaweza kulima choroko zikakubali sana
 
Mkuu na mimi nina ekari zangu kama 70 huko Fukayosi. Najikusanya kwa ajili ya kilimo huko. Nilikuwa na wazo la kulima matikiti maji na mananasi kwa kuanzia
 
Mkuu na mimi nina ekari zangu kama 70 huko Fukayosi. Najikusanya kwa ajili ya kilimo huko. Nilikuwa na wazo la kulima matikiti maji na mananasi kwa kuanzia

Karibu ndugu, una details za matikiti maji? Au unaweza kufahamu wapi nitapata details?
 
nina uzoefu na fukayosi. tatizo la huko ni ukosefu wa maji ya uhakika na nguvukazi. kuna jamaa yangu alijaribu mahindi, hakufanikiwa sana. mimi nikajaribu alizeti nikatoka kapa. may be ufuta. Choroko sina uhakika.

matikiti siyo rahisi kuyalima fukayosi kwa sababu ya ukame, labda uchimbe kisima, au utee mvua.

mimi nakubaliana na aliyekupa wazo la nanasi.
 
Nafuatilia soko la mbaazi, mbaazi huvumulia kidogo, lakini matikiti ni pasua kichwa. Nikifanikiwa kupata taarifa sahihi za soko la mbaazi nitaweka hapa.
 
Ambaye yupo fukayosi naomba tuwasiliane na mimi nimeanza kilimo cha nanasi, nimefanya geo-physical survey ya maji kupitia wale jamaa walio karibu na chuo cha maji, pia ninampango wa kutengeneza bwana la maji ili nikinge maji ya mvua. Tayari nimeishapanda nanasi ekari 12 na mpango wangu ni kufikisha ekari 30 ifikapo mwezi wa 6 mwaka kesho.

Changamoto kubwa niliyoiona Fukayosi na nguvu kazi hasa vijana ni wazembe sana ila kiboko yake ni kwamba uwe unaenda shambani mara kwa mara kwa safari za kushitukiza na uwe mkali. Kingine usiwazoeze kuwapatia pesa mara kwa mara kila unapokubaliana nao kazi maana kuna wengine wanasema eti ukipatana nao uwape advance kwanza mimi ilo nimelikataa na sasa wameishazoea.

Mengi tutawasiliana zaidi...

Je uko fukayosi sehemu gani??
 
Nafuatilia soko la mbaazi, mbaazi huvumulia kidogo, lakini matikiti ni pasua kichwa. Nikifanikiwa kupata taarifa sahihi za soko la mbaazi nitaweka hapa.
Thanx, na mimi nimesikia habari za mbaazi but sina details zake, nakutegemea uzimwage hapa!!
 
Ambaye yupo fukayosi naomba tuwasiliane na mimi nimeanza kilimo cha nanasi, nimefanya geo-physical survey ya maji kupitia wale jamaa walio karibu na chuo cha maji, pia ninampango wa kutengeneza bwana la maji ili nikinge maji ya mvua. Tayari nimeishapanda nanasi ekari 12 na mpango wangu ni kufikisha ekari 30 ifikapo mwezi wa 6 mwaka kesho.

Changamoto kubwa niliyoiona Fukayosi na nguvu kazi hasa vijana ni wazembe sana ila kiboko yake ni kwamba uwe unaenda shambani mara kwa mara kwa safari za kushitukiza na uwe mkali. Kingine usiwazoeze kuwapatia pesa mara kwa mara kila unapokubaliana nao kazi maana kuna wengine wanasema eti ukipatana nao uwape advance kwanza mimi ilo nimelikataa na sasa wameishazoea.

Mengi tutawasiliana zaidi...

Je uko fukayosi sehemu gani??

Mkuu ni miaka mitatu sasa tangu uweke hii post. Hebu tupe uzoefu wako kuhusu kilimo cha mananasi na mimi nina kishamba changu huko Fukayosi. Udongo, nguvu kazi, maji na soko maana najua tayari umeshaanza kuuza sasa. Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom