Zee1
Senior Member
- Jul 17, 2015
- 103
- 24
Kwa muda nimekuwa nikimfuatilia jinsi serikali ya JP Magufuli ikifanya kazi, inaleta matumaini ukifananisha na mtangulizi wake mzee wa Msoga. Jana kwenye hotuba yake amegusia mambo nyeti japo sio yote lakini unaona dhamira ya kweli ndani yake. Niwaase watanzania ugonjwa kuingia mwilini mwa binadamu ni rahisi sana lakini matibabu yanachukua muda. Na hata ukipona bado unahitaji muda wa ku recover! JP Magufuli yupo sahihi tumuombee na tumpe ushirikiano. Tumezidi kulalamika tafakari, chukua hatua nchi hii inakuhitaji wewe na mimi kutoka kwenye mkwamo.