Rais Samia Suluhu ametoa moja ya hotuba bora sana, nina matumaini ataziba nyufa nyingi za utawala uliopita

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Binafsi nilikuwa na mashaka na namna atavolimiliki jukwaa mbele ya viongozi wabobezi na malegandary wa siasa za kusini mwa Afrika. Ila ukweli kabisa nimeridhika, kwa hotuba ya leo nampa maksi 97% hizo maksi 3% nilizomnyima ni makosa madogo madogo ambayo nadhani yanachangiwa na ugeni na ukifananisha pia kwamba amekula kiapo cha urais siku tano zilizopita, ila kwa ujumla ametoa hotuba ambayo naweza sema kwa ubora imewazidi watangulizi wake na kupitia hotuba hii, nimenusa kwa mbali mwelekeo wa itikadi wa serikali ya Madam President na nimeridhika kwamba utaweza kufanikiwa sana kwenye baadhi ya maeneo ambayo utawala wa Hayati JPM uliboronga.

Kwa ufupi, mambo makubwa niliyoyaona kutoka kwenye hotuba ya leo ni haya

1. Uhusiano na nchi majirani - Haukua mzuri, na hususani uhusiano na jirani yetu Kenya ambaye tuna muingiliano mkubwa sana wa kibiashara na kijamii kuliko majirani wetu wote. Ila kwa namna ya namna alivotoa hotuba yake, nna imani sana kwamba ataboresha na kuponya haya mahusiano na majirani. Na sio Kenya tu, hata wale ambao walibatizwa kwamba ni 'mebeberu' nadhani Madam President ni kama amefungua mkono kupitia hotuba yake kitu ambacho ni kizuri.

2. Umoja wa kitaifa - amegusia pia kwenye hotuba yake na nadhani ni jambo jema, maana taifa tulishafika mahali pabaya sana

3. Moyo wa kuendeleza yale mazuri ya mtangulizi wake Hayati JPM - Hapa pia nimefurahi kuona kwamba amerithi mtizamo wa JPM kuhusu kuendeleza miundo mbinu, Hili ni jambo bora pia, kwa sababu naamini kwamba Magufuli kuna mahali alifanya vizuri na panastahili kuendelezwa, na nimefurahi kwa yeye kututhibitishia hilo.

4. Kusikiliza ushauri wa viongozi waliomtangulia - hii point nyngine ambayo naona imempa credit kubwa sana, maana technically viongozi waliopita wanaifahamu hii nchi vema na sio mbaya kuchukua ushauri kwao, japokuwa ninaamini itabidi kwanza awe ana mtizamo wake kwanza kabla ya kupokea ushauri ili asiingie kwenye hatari ya kuonekana ni kiongozi asiyeamua kwa akili yake.

Binafsi haya ni machache niliyoona kwenye hotuba ya leo, na kwa kweli nimeyafurahia kwa Madam President, na hili ni angalizo natoa. Madam President anaweza kufanya wonders kama atasimamia alichohutubia leo, na niseme tu wazi, anaweza kutawala mpaka 2030!...

Kwa hotuba ya leo, hata wale waliokuwa wanapiga ramli za ndoto za urais 2025, watakuwa wamaogopa sana. Angalia body language ya Mwinyi wakati Madam President anamaliza hotuba yake, hakika utaona kabisa ametiwa uwoga fulani. Ni kama leo viongozi wengi hawakutegemea kama Madam President angetoa speech ambayo ipo authoritative kiasi hicho.

Cha mwisho ni kumshauri tu, aache mara moja kuinamisha kichwa kwa heshima, Rais unatakiwa u express Authority kila dakika, so sijapendezwa na akisalimiwa kila saa anainamisha kichwa, awe straight kila saa hata akisalimiwa.

Nawasilisha
N.Mushi
 
Mama Samia should learn to look people in the eye ; that is a sign of strength!!! Rais hutakiwi kuonekana mnyonge; kwani una dhamana ya watu million 60 na Ardhi yote ya nchi!! "YOU ARE NOW COMMANDER OF OUR ARMED FORCES."

Rais chukua ushauri lakini Sio lazima uufuate, uamuzi ni wako kwani wewe ndio muwajibikaji.
 
Mama Samia should learn to look people in the eye ; that is a sign of strength! Rais hutakiwi kuonekana mnyonge; kwani una dhamana ya watu million 60 na Ardhi yote ya nchi!! Rais chukua ushauri lakini Sio lazima uufuate, uamuzi ni wako kwani wewe ndio muwajibikaji.
Itabidi ajifunze. Nimeona pia ni kama weakness ambayo itamfanya aonekane yupo weak. Kwenye kusalimiana na viongozi wenzake itabidi apewe shule
 
Kuinamisha kichwa ni kama gesture wanayofanya baadhi ya mabinti wanaposalimia wakubwa ?..au vipi?,sijaelewa.

Sema Mama akisimama imara na kutenda haki na kuboresha mambo uliyoyaorodhesha na mengine kama ajira,biashara na uwekezaji,afya n.k basi atapendwa sana..nani atakayemchukia mama?..sioni
 
Nina moja tu: Kuinamisha kichwa siyo udhaifu. Kuinamisha kichwa ni alama ya unyeyekevu ambayo anatakiwa awe nayo kila kiongozi.

Inasikitisha wabongo tumezoea viongozi wenye viburi na kujikweza kiasi ambacho ukimwona anayenyenyekea unamwona kama ni mjinga. Hili la kuinama ni zuri sana na aliendeleze.
 
Kuinamisha kichwa ni kama gesture wanayofanya baadhi ya mabinti wanaposalimia wakubwa ?..au vipi?,sijaelewa.

Sema Mama akisimama imara na kutenda haki na kuboresha mambo uliyoyaorodhesha na mengine kama ajira,biashara na uwekezaji,afya n.k basi atapendwa sana..nani atakayemchukia mama?..sioni
Ni kuonesha heshima ila kwa Rais sioni kama ni jambo la lazima kufanya. Ni mtizamo lakini. ila sio kitu poa.. wajuvi watuambie embu kama kuinamisha kichwa ni sahihi kwa mtawala kufanya.
 
Mimi na stake she is but a right candidate.
What is good for the goose is good for the gander. Watu wenye mitazamo ya kidhalimu waache kumtazama kwa jicho la kushindwa kisa tu ya jinsi yake.
Nimeona hata mimi .. ndo mana wanasemaga viongozi wanachuguliwa na Mungu. Hii kitu inaeza kuwa kweli.
 
Nina moja tu: Kuinamisha kichwa siyo udhaifu. Kuinamisha kichwa ni alama ya unyeyekevu ambayo anatakiwa awe nayo kila kiongozi. Inasikitisha wabongo tumezoea viongozi wenye viburi na kujikweza kiasi ambacho ukimwona anayenyenyekea unamwona kama ni mjinga. Hili la kuinama ni zuri sana na aliendeleze.
Ni heshima ila mtu anaweza ku take advantage kwa kudhani ni udhaifu. Mi naona aache kuinamisha kichwa. Itamfanya azidi kuwa na Authority
 
Nina moja tu: Kuinamisha kichwa siyo udhaifu. Kuinamisha kichwa ni alama ya unyeyekevu ambayo anatakiwa awe nayo kila kiongozi. Inasikitisha wabongo tumezoea viongozi wenye viburi na kujikweza kiasi ambacho ukimwona anayenyenyekea unamwona kama ni mjinga. Hili la kuinama ni zuri sana na aliendeleze.
Anaweza kufanya hivyo kwa masheikh na Maaskofu hapa nyumbani ikimpendeza, lakini kwenye International arena it is a no no haitamsaidia yeye na nchi pia.

Just for reference muangalie yule mama Harris VP wa ubeberuni! Au aangalie clips za marehemu Benazir Bhutto to see how she carried herself on the world stage!
 
Mama Samia should learn to look people in the eye ; that is a sign of strength!!! Rais hutakiwi kuonekana mnyonge; kwani una dhamana ya watu million 60 na Ardhi yote ya nchi!! Rais chukua ushauri lakini Sio lazima uufuate, uamuzi ni wako kwani wewe ndio muwajibikaji.
Yes, because she is now a chief in Commander of all armed forces

Sasa ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote nchini

Na askari huwa namna Fulani ya kutazama

Tuko salama, tuchape kazi, tutende haki, uadilifu, weledi, uwajibikaji, na kutii sheria na Mamlaka!

Mungu yu pamoja nasi daima!
 
Anaweza kufanya hivyo kwa masheikh na Maaskofu haha nyumbani , lakini kwenye International arena it is a no no haitamsaidia yeye na nchi pia!! Just for reference muangalie yule mama Harris VP wa ubeberuni!!!
Kila mtu na kaliba yake. Kwani ni lazima aige? Mbona viongozi wa India wanainama tena ni wanaume?
 
Back
Top Bottom