Nimefanyiziwa na rafiki!!!!

Kupata evidence kuna ugumu kidogo maana nilimpa mkononi na hakuna meseji tuliyoandikiana zaidi ya meseji yake ya mwisho aliniandikia ya kuniambia amekaa Samaki samaki karibu na entrance baada ya hapo kila kitu tumekuwa tukipigiana simu tu, najifikiria kama inawezekana kupata sauti yake pale Vodacom lakini naona nitajichoresha sana maana hela yenyewe ni mbuzi ukilinganisha na mchakato wa kupata evidence
 

Pole sana ndugu usipo onana na mtu kwa miaka miwili, tegemea mabadiliko makubwa sana kwa huyo mtu. Rafiki yako amebadilika, amekuwa tapeli.
 
Tafuta manati ya mzungu. Mtokee umwambie kwamba umeshafanya maamuzi. Kitakachofuata ni news tuu. Rafiki wa hivi anakera sana.

Manati ya mzungu yapo kaka ila niliwahi kufikiria kitu kama hicho wife akanishauri nisifanye hivyo maana tunaweza kuzalisha tatizo kubwa zaidi ya hilo
 
Una uhakika bado yuko kwenye hiyo kazi mpaka sasa? manake hapa pananukia harufu ya utapeli!! huyu jamaa ni tapeli mzoefu.

Ni mfanyakazi bado katika taasisi hiyo.
 
Kibaya zaidi si kila mtu yupo hivyo, hii ni changamoto kwakweli

Umenikumbusha na mimi mtu kasepa na 2m zangu ni wiki ya 3 sasa simu yake haipatikani. Kwa hiyo nimeamua kupotezea na kuendelea kulipa deni alilonisababishia. Yaani sometimes nikiwaza hadi naogopa tutashindwa kusaidiana kwenye shida kwa kuwa hatuaminiani sijui tunajenga jamii ya aina gani?
 
Very useful!!!!
 
Pole mkuu umenikumbusha the same story ya kudhulumiwa na rafiki wa karibu, kwa sasa mimi ninapotoa ela kwa rafiki au ndugu ninatoa kama sadaka zikirudi sawa zisiporudi sawa. Hapo roho itakuuma zaidi kwa mambo na maneno yatakayotokea baada ya wewe kuchukua hatua wewe ndio utaonekana hujui ubinadamu na maneno mengi, usimuamini mtu siku nyingine kwani kukopesha kunaweza kukugombanisha na marafiki na ndugu.
 

Kwa hili kweli na kubali upeo wangu uliishia pale
 
Benki gani inatoa muamala wa zaidi ya mil. 1 kwa siku kwa njia ya ATM? Ungelifikiria hilo nadhani ungepambanua ukweli na uongo!
 
Kuna kitu cha kujifunza hapa.... Asante mkuu kwa Stori yako hii sina ushauri kwakuwa na mimi huwa ni Muhanga wa kudai hata kama nina ushahidi lakini nitabadili Tabia.
 
kweli aisee mimi siachi kumkopesha mtu kama nnacho!!!ila nakukopesha kwa bond ukienda kulalama huko ooh jamaa nimempa laptop ya 1m kwa laki 3 cjui nini cjui nini utajiju ila mi najua nimekusaidia na utarudisha nitamsaidia mwingine!!!na ukizingua nauza laki saba nakupa laki nne zako...na sio muda nafungua micro ili niwe naweka na riba na kuchukua vitu juu....maana naona wanakuja kukopa wanaweka bond wanaenda kunisengenya wanalipa wanaenda kunisengenya tena etii ooh nimemrudishia viela vyake mara blah blah...wanaishiwa wanakuja tena na laptop ile ile nawapa kwa masharti yale yale na wanaendelea kulipa sasa nitaweka hiyo twenty % ya kujifutia machungu ya majungu...hakuna ubinadamu
 
acha tu ...kuna watu jamani hawajuagi wengine nao wana shida ya hela..mi nimemuachia tu mungu !
 
Huyo hakuwa rafiki wa ukweli,muhimu ni kumfuta Ofisini kwake kama unapafahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…