Nimefanya yote sasa naomba na nyie mseme

mkulimamwema

Senior Member
Apr 14, 2011
153
18
Mimi ni mwanaume wa miaka 26,nimekuwa kwenye uchumba kwa muda wa mwaka sasa.Niliamua kumpenda huyu bibie pamoja na kuwahi kuumizwa na bwana mwingine kiasi cha kumharibia maisha hilo sikulijali.Siku zote sikupenda akumbuke yaliyompata na nilijitahidi kuwa karibu kadri nilivyoweza,maneno matamu na kila apendalo mwanamke nilimpa.Mimi nilichofanya ni kuwa mwaminifu sana na kuwa mkweli sana.Yeye hudai hawezi kuongea kiasi kwamba nabaki naongea kwenye simu muda mrefu nikimbembeleza angalau aniambie maneno ya faraja hubaki kusema hana cha kusema,nilivumilia sana.Hivi karibuni nilisafiri toka dar hadi mwanza kumwona yeye na nilifikia hotelini kwa kuwa sina ndugu kule.Kuna mambo alinidanganya nilimhoji sana ila hakuonyesha kujutia hata kuniomba msamaha,jana usiku namtakia usiku mwema alipokea simu na kunyamaza kimya,niliongea muda mrefu hata hakusema kitu,nimejitahidi kumjali mno na kweli nampenda sana na akinisikiliza napenda sana awe mke wangu maana sitaki kuwa na mwanamke mwingine,ingawa inaniuma sasa nataka kuachia ngazi,ndugu wana familia kaka zangu shemeji yenu anataka kutoka na nyie dada zangu wa hapa JF wifi yenu anasumbua nifanye nini?
 
pole. Jaribu kumweleza unavyojisikia juu yake, mwambie awe mkwel kwako cz huna NIA ya kumwumiza, icjekuwa hajiamin kutokana na hyo past yake.
 
Jaribu kuongea vizuri na umueleweshe kuwa huna nia mbaya naye..
Ukiona habadiliki basi achana nae sio wako huyo..
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 26,nimekuwa kwenye uchumba kwa muda wa mwaka sasa.Niliamua kumpenda huyu bibie pamoja na kuwahi kuumizwa na bwana mwingine kiasi cha kumharibia maisha hilo sikulijali.Siku zote sikupenda akumbuke yaliyompata na nilijitahidi kuwa karibu kadri nilivyoweza,maneno matamu na kila apendalo mwanamke nilimpa.Mimi nilichofanya ni kuwa mwaminifu sana na kuwa mkweli sana.Yeye hudai hawezi kuongea kiasi kwamba nabaki naongea kwenye simu muda mrefu nikimbembeleza angalau aniambie maneno ya faraja hubaki kusema hana cha kusema,nilivumilia sana.Hivi karibuni nilisafiri toka dar hadi mwanza kumwona yeye na nilifikia hotelini kwa kuwa sina ndugu kule.Kuna mambo alinidanganya nilimhoji sana ila hakuonyesha kujutia hata kuniomba msamaha,jana usiku namtakia usiku mwema alipokea simu na kunyamaza kimya,niliongea muda mrefu hata hakusema kitu,nimejitahidi kumjali mno na kweli nampenda sana na akinisikiliza napenda sana awe mke wangu maana sitaki kuwa na mwanamke mwingine,ingawa inaniuma sasa nataka kuachia ngazi,ndugu wana familia kaka zangu shemeji yenu anataka kutoka na nyie dada zangu wa hapa JF wifi yenu anasumbua nifanye nini?

vijana wa karne hii mna mambo mengi kuliko hata wazee wenu lol....
haya bana............................
 
Nahisi unadanganywa
Wanasema "KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU"
Yaani amewahi kukudanganya halafu hana hata chembe ya kujuta (achilia kuomba radhi) :confused2:

Wala usidanganyike kwamba HAAMINI kuwa unampenda kweli.
Wanawake wana uwezo mkubwa wa kutambua mwanaume anaewapenda kwa dhati
Na fahamu kuwa kuna wanawake wanaweza kutumia nafasi ya wao kupendwa sana kuwachezea hao wanaume
Kuumizwa isiwe sababu, labda kama kuumizwa huko ni kubakwa, kuingiliwa kwa nguvu, kupigwa au kudhalilishwa.
Lakin kama ni kugundua mpenzi wake ana mtu mwingine then ukaachana nae, baada ya muda anaweza kutulia tu.

Anadengua tu huyo, anajua unampenda sana. Kama unaweza jaribu ku-pause mawasiliano nae kwa muda ili uone reaction yake. Les say 1 week. Ukiona kimya ujue . . . .
 
Pima uzito wa hayo aliyokudanganya kwenye mizani ya athari, fikiria vizuri kwa nini awe hataki kuongea unapopiga simu. Hapa utakuta kuna mambo mengi ya kujiuliza kama vile:
1. Labda jamaa alimtenda vibaya sana na anakuona wewe ni walewale tu, ikiwezekana anaona style zenu za kumtokea zinashabihiana.
2. Labda aliachiwa ugonjwa, au aliharibikiwa kimaumbile (kama kutolewa kizazi, nk) na hivyo anaogopa kukupenda hafu akakuumiza; anaogopa kukueleza ukweli juu ya hili.
3. Labda ana mwanaume mwingine na hataki akwambie, ila anataka ukate tamaa wewe mwenyewe ili lawama zisimwangukie. Ndio maana unaweza ukapiga cmu akaipokea bila kuongea kitu akiogopa kuna mtu atayasikia maongezi yake.
4. Labda hajakupenda kabisa na alikukubali pale mwanzoni kwa sababu alikuwa ameachika na haelewi nini cha kufanya na kutofanya; uamzi wa ghafla.

Fikiria na pia uamue, miaka 26 sio mingi kiasi cha kushindwa kuanza uhusiano mpya na wa kweli. Tuliza moyo wako na uchunge tamaa mbaya, jipe moyo pia komaa na kuongeza kipato chako huku ukimtafuta mwenzi wa kweli taratibu (wakati mwingine hii mambo inachukua muda kufanikisha).

Kuna Padre mmoja niliwahi kumsikia anahubiri kuhusu zoezi la kutafuta mchumba/mke anasema kwamba siku hizi watu wengi tunamwomba Mungu huku tukisema, "Mungu naomba unisaidie niweze kumwoa flani". Badala ya kusema, "Mungu naomba unisaidie niweze kupata mke ambaye ni mwema".

Kwa hiyo pamoja na yote usisahau kumshirikisha Mungu katika mipango yako, kila la heri kaka.
 
If you love something, set it free. If it comes back to you, it is your and if not,. It was never meant to be! Pole sana
 
dahhhh
mpe muda kidogo zaidi
kama anaendelea hivyo
acha naye, utakuwa unapotezewa
muda tu....

huyo yaelekea anajificha tu nyuma
la hilo neno "kuumizwa" walioumizwa haswa wala hata
hawaingi kwenye maHusiano ya kimapenzi
kama hawako tayari..
 
Hapo umekosea njia geuka haraka, sasa kama hata kuongea hataki si makubwa haya
Utaoa gunia la misumari ndugu yangu ambalo litakuwa linakuchoma na haliongei
 
Ndugu tangu chapa lapa. Yatakayo kukuta huko mbele yatakufanya ujute maishani mwako. Huyo hakupendi, hata umlazimishe vipi hapo hakuna kitu. Kama huniamini wewe endelea tu. Kuna wenzio wengi walilazimisha mpaka wakafunga ndoa kwa matumaini kuwa akiwa ndani atabadilika. Waulize kleo nini kimetokea baada ya ndoa? Watakujibu maumivu mara 100. Kaka chapa lapa, usiwe mvivu kutongoza. Hiyo ndo fani yetu
 
Pole sana mkulima mwema, dalili za mvua siku zote ni mawingu, nashangaa sana kwa nini hujui wakati wewe ni mkulima mzuri tu, inaonekana wewe ni mtaalamu sana kwenye mapenzi kwa jinsi ulivojielezea, unajua kupenda, hadi umejitoa kwenda mwanza si mchezo, kwa kifupi huyo msichana atakuwa tayari keshachukuliwa ila anaona aibu tu kukwambia kwa jinsi alivoingia kwako kwa gia kwamba aliumizwa, inaonekana hata yule wa kwanza alimwacha kwa style kama hii ya kwako, ila fumba macho achana nae anza maisha yako utakutana na msichana mwingine atakupenda for who you are, achana na mapenzi ya mbali hayo yatakupa presha
 
Mkulima kwa mwanamke uliona bluu yeye anaiona ni kijani!Nafikiri umenielewa!
 
Back
Top Bottom