Wakuu nawasalim sana,
Nimeamua kuandika hili hapa kiasi nipate fursa ya kulitoa moyoni mwangu kwani nipo kwenye mtihani mgumu sana. Leo hii mchana nikiwa nasikiliza mawaidha ya kiislam channel ten kutoka kwa Sheikh Mohamed Eid abu Eid, mada "matatizo katika talaka - (islamic)".
Kuna msikilizaji aliuliza swali kwamba ikiwa mwanaume katika hali ya hasira atatoa talaka "tatu" kwa kutamka, lakini punde akasema alighadhibika so itambulike ni moja, je hukumu ya kiislam inasemaje?
Jibu: Uislam hauna utani kwenye talaka, na mwanaume kapewa power ya talaka kwa kuaminiwa kwamba ni composed compared angepewa power hiyo mwanamke zingekuwa zinatumika dailly. So kitendo cha kusema tatu, itabakia kwamba umeacha talaka tatu na kuanzia hapo mwanamke sio mke wako na atakiwa arudi kwao. Utaruhusiwa kumuoa tena tu endapo ataolewa na mtu mwingine willingly na ataachika willingly bila fitna kutoka kwa mwanaume aliyekuwa amemuoa kabla.
Issue
Miaka kama minne iliyopita iliwahi kutokea sintofahamu kati yangu na mke wangu. Nakumbuka nikiwa nimelala mke wangu aliniamsha kwa hasira akitaka nimuache. Baada ya kumsihi na kushindwa nilitamka kumuacha talaka tatu...lakini aliponiomba nimuandikie kwa ajili ya uthibitisho kwao nikaandika moja kwakua ikiwa moja au mbili mwanamke anatakiwa akae eda kwako, nilimruhusu abaki eda, na alhamdulillah siku ya pili tu aliniomba radhi nikamsamehe tupo hadi leo.
What next,
Leo tulikuwa na issue nyingine na wife, nilipokuwa Ijumaa niliomba Allah anifaulishe katika mtihani wangu na wife katika kila sidja niliyoenda nikilenga amshushe jazba. Nilipofika nyumbani wakati nasubiri lunch, ndipo nikawasha channel ten marudio ya kipindi husika. Lahaula napigwa na butwaa kusikia hii kitu.
Nimebaki na butwaa nawaza kuwauliza masheikh wengine kama hili linakubalika katika madhehebu yote katika Uislam. Na ikithibitika kuwa hakuna namna wakuu nitakuwa naagana na mpenzi wangu wa 15 years.
Najiliwaza kwamba labda Allah anampango wake kwetu sisi wote. Labda ajali iliyotokea ilitakiwa itokee kwa ajili ya kusimika maandiko. Labda ndoa yetu ilikuwa ya muda mahsusi na ililenga kupata watoto wetu. Ikitokea nitaachananae nimeamua kumruhusu achague chochote katika mali zangu ambacho kitampa faraja aendako. Nitalea watoto wangu nakadhalika.
Nawatahadhalisha wanaume wenzangu, muwe makini sana. Kwa atakayemuoa mke huyu namtakia kila la kheir. sina kinyongo atakuwa mke mwema kwako. nami inshallah huenda nitapata zaidi ya huyu...
regards,
Mahwelu