pole sana! nadhani sasa kuna kila sababu ya wewe kuwa makini, ucpende kuwaamin watu kirahisi, sisi wanaume ni wajanja sana, twajua vyema kucheza na mdomo! Mwombe Mungu akusaidie kusahau na kufungua ukurasa mwingine wa maisha yako. Pole sana!
Ndugu zangu naomba msaada katika maisha yangu nimedanganywa mara nyingi lakini mara tatu nimefanywa mjinga hadi najiona sifai
1.nilidanganywa na mwanaume akanizalisha akaniacha
2.nilipata mwanaume mwingine akanitapeli kumbe ana mke na watoto
3.nilikutana na mume aliyenizalisha akaahidi kunisaidia kutunza mtoto kibaya mazingira yalinifanya nishirikiane nae kanitosa tena
chonde naomba msaada wa mawazo lakini msinitukane mtazidi kuniumiza