Nimeconfirm vyuo viwil tofauti nasaidikaje

Nimeconfirm vyuo viwil tofauti nasaidikaje

doullar

Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
31
Reaction score
13
Nimechaguliwa udom na muce na vyote nimeconfirm vyote nasaidiwaje
 
Na mm imenitokea bt nimeenda udism ku unconfirm wamesema wanashugulikia maana tupo weng wenye case kama iyo
 
Tatizo lako co kucomfirm vyuo viwili ila ni ukilaza tu, ujui kuna wenzako wamekosa hiyo fursa hata ya chuo kimoja wewe unaichezea.

Subiri uone kama awa jamaa wanaposema ukicomfirm vyuo viwili unaweza poteza nafasi kama wanatania au kah...
 
Nimechaguliwa udom na muce na vyote nimeconfirm vyote nasaidiwaje

Vyuo karibu vyote vimetoa mabandiko juu ya ku-confirm halafu mwisho wa siku unalaumu TCU na vyuo husika

Haya jiandae kuwa mwanafunzi hewa
 
Umeshalikoroga. Jina lako likitumwa mara mbili Bodi ya Mikopo hautapata kabisa. Cha kufanya wasiliana na chuo husika unachotaka kuachana nacho wakuondoe kwenye orodha yao haraka iwezekenavyo.
 
wewe ni jipu linalohitaji kutumbuliwa!!!!

vyuo karibu vyote vimetoa mabandiko juu ya ku-confirm halafu mwisho wa siku unalaumu TCU na vyuo husika

Haya jiandae kuwa mwanafunzi hewa


Asome hapa jinsi walivyosema.


AARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI 2017/2018 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia umma kuwa Awamu ya Kwanza ya kudahili wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ilimalizika tarehe 30 Agosti 2017. Katika awamu hiyo, kama ilivyoelezwa katika tangazo la Tume la tarehe 20 Julai 2017 wanafunzi watarajiwa walituma maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo hapa nchini. Vyuo vilichakata maombi hayo na hatimaye kuyawasilisha Tume kwa ajili ya uhakiki. Tume inapenda kuuarifu umma kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18. Matokeo ya uhakiki ni kama ifuatavyo: a) Jumla ya idadi ya majina yaliyowasilishwa toka vyuoni yalikuwa 180,640 (wanaume 109,399, wanawake 71,241). Hata hivyo majina haya yalikuwa na kasoro kadhaa kama vile kujirudia. Tume iliyahakiki na kubakisha majina 77,756 (wanaume 47,501 wanawake 30,255) ambayo ni jumla ya maombi yote. 1 b) Jumla ya wanafunzi ambao wamechaguliwa na vyuo (kati ya waombaji 77,756) ni 44,627 (wanaume 27,116 wanawake 17,511). Hiyo ni sawa na asilimia 57.4 ya waombaji wote. Waombaji 33,129 waliosalia (42.6%) hawakuchakuguliwa na vyuo kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba. c) Katika waombaji 44,627 ambao wamechaguliwa na vyuo, Tume imejiridhisha kuwa waombaji 20,247 (45.4%) wanaweza kujiunga na vyuo walivyoomba moja kwa moja (wanaume 12,396 wanawake 7,851). Waombaji 16,584 (37.2%), wanaume 9,923 wanawake 6,661, wamechaguliwa zaidi ya chuo kimoja. Aidha waombaji 7,796 (17.4%), wanaume 4,797 wanawake 2,999, Tume imebaini kuwa hawana sifa za kujiunga na vyuo vilivyowapendekeza. Hii ina maana waombaji 36,831 (wanaume 22,319 wanawake 14,512) wanatarajiwa kujiunga na vyuo katika Awamu hii ya Kwanza. Taarifa kuhusu majina ya waombaji waliochaguliwa na wale waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja zimewasilishwa kwenye vyuo husika. Hivi sasa Tume imefungua maombi kwa Awamu ya Pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Oktoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili: a) Waombaji ambao wamechaguliwa zaidi ya chuo kimoja; waombaji hawa watatakiwa kuamua mara moja na kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo hicho b) Waombaji ambao wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba; Aidha Tume imetumia fursa hii kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili: a) Waombaji wa Kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza; b) Waombaji wenye vigezo vya Stashahada waliochelewa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN); c) Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na d) Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakaokuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali. Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi katika Awamu ya Pili ni ule ule uliotumika katika Awamu ya Kwanza ya Udahili. Hii ina maana kuwa waombaji watatakiwa kuwasilisha maombi yao moja kwa moja vyuoni na siyo kwenye Tume (TCU). Tume inawashauri waombaji wote kutumia fursa hii fupi kukamilisha maombi yao ili kuepuka kukosa udahili kwa mwaka wa masomo 2017/18. Aidha Tume inawataka waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao. Kwa wale ambao wamechaguliwa zaidi ya chuo kimoja wathibitishe sawia chaguo la chuo kimoja tu ili kuepuka uwezekano wa kukosa udahili kwa mwaka wa masomo 2017/18.<br /> Prof. Eleuther Mwageni <br />Kaimu Katibu Mtendaji <br />Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania<br /> 5 Oktoba 2017
 
Huko ni kukosa umakini kabisa. Yani ni makusudi ya hali ya juu. Sasa mwisho wake ni kuishia kukosa mkopo kwasababu majina yatatumwa Mara mbili heslb.
 
cio maksud kaka simu ilkua na tatizo la kujibonyeza nkajikuta tayar imeconfirm
 
kaka ni matatizo ya

simu haikua dhamira yangu
Umesha disco subiri mwaka kesho ufanye tena application ,ila next time kuwa muangalifu
1d856fdb8808cfb220aaad3753e657e4.jpg
 
Back
Top Bottom