Habari zenu: Tangu niolewe huu ni mwaka wa tatu lakini kuna kitu kinanitatiza huyu mwanaume mara nyingi huwa anapigiwa simu na namba mpya tofauti tofauti nikijaribu kuzipiga wanapokea wadada ukimuuliza anakwambia alikosea namba je hiyo namba yake huwa inakosewa na wadada tuu? Kingine wadada wa ofisini kwao kila siku usiku wanamtakia usiku mwema mara awaalike kwenye mitoko huwa tunaenda nae lakini nahisi huwa wananisanifu kwa nini awe na urafiki na wadada tuu?
Hayatuhusu. Haya ni mambo yenu binafsi wewe na huyo mumeo. JF sio mahala pa kuleta mambo yenu!! Peleka kwa wakwe. Ukiona anaendelea, mtose, tafuta bwana mwingine!!
nilikuwa na uhusiano nae kwa muda wa miaka miwili kabla ya kufunga ndoa mpaka alivyomaliza kusoma ndio tukaoana tuna mtoto mmoja ana miezi saba
Ukiishi kwa kuchunguza simu ya mumeo, hiyo ndoa itakushinda muda si mrefu.
Ukiishi kwa kuchunguza simu ya mumeo, hiyo ndoa itakushinda muda si mrefu.
hyo ndoa aliihitaji au wewe ndo ulimfosi akuoe?
Jaribu kuchukua namba ya kaka yako ila usiisevu hafu umueleze huyo kaka yako awe anakupigia usiku ukiwa na mzee kisha wewe jifanye hutaki kuongea kwa kuikata hiyo simu ya kaka yako ila isiwe namba hiyohiyo kila siku,chukua namba za kaka zako woote asipo kuuliza juu ya hizo namba basi inakubidi uchukue hatua za busara na sio ugomvi.
Reyna, it doesn't matter where your husband gets his appetite as long as he eats at home! Achana na simu ya mumeo, ukimchunguza sana kuku hutamla, walisema wahenga.
mi sikumfosi nikimwambia naenda nyumbani ananiahidi kunifanyia mambo mabaya kuna siku tuligombana nikaondoka ile nafika tu stendi nikakamatwa na police wakanipeleka kituoni nilikaa kama masaa mawili hivi akaniijia sasa mi simuelewi ameshanifanyia vituko vingi vinatia hasira sasa hii ni ndoa au nikutekwa?