Nimechoka maisha ya kusindikiza

Nimechoka maisha ya kusindikiza

Joined
Jan 20, 2020
Posts
65
Reaction score
105
Wakuu Hongereni na Majukumu /kama sio poleni na Majukumu,

Moja kwa moja kwenye Mada wakuu ni kwamba kiukweli nimechoka kuishi maisha ya kusindikiza Na nikitizama umri unakwenda Ajira hakuna sasa basi naamua kuchukua Maamuzi magumu. Nahitaji kwenda kwa Mr sangoma japo nikajichukulie lindago mwenye connection za ndago za kweli na uhakika karibu pm kwa kunielekeza zinatolewa mkoa gani na cost zake ni kiasi gani ili nijipange kuifata.

Nimechoka kuishi maisha ya kusindikiza a.k.a Mungu ataleta naomba nisifikiriwe vibaya wala kukashifiwa na MTU yeyote kila mmoja ana maamuzi yake na Imani yake wakuu najua JF ni baba lao humu kuna kila kitu najua mpo wataalamu wa hizi mambo.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kakudanganya kuwa mganga ndiye anayeweza kukupa dawa ya kupata ajira? Ukishamwamini mganga wa kienyeji ndio utapotea mazima, hakuna mtu mwenye mafanikio ya kweli aliyefanikiwa na kudumu katika mafanikio kwa kumtegemea mganga.

Unatakiwa upambane kuumiza akili katika kujitafutia kipato halali. Mungu pekee ndiye mtoaji na ukipambana atakupatia tu. Mwombe yeye bila kuchoka na upambane. Maisha si ajira pekee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi naona nikutaftie Namba tu ufanye mambo. Au unaonaje?
 
Mkuu hakuna pesa rahisi kibongobongo matajiri wengi ni wala rushwa , mafisadi, wakwepa kodi, biashara haramu etcetc ila hawatokaa wakuambie wewe kama unaona kupiga ndumba kutakifanya utoboe piga ndumba pata pesa ya kutosha rud kanisani to mchango uone kama huitwi Mtakatifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
....Kama una hakika ya kupata fedha za kulipa gharama za ndago baada ya kuelezwa pa kuipata, basi pia unao uwezo wa kupata hela ya kufanya kabiashara hata kakuuza mkaa!
Achana na kumtegemea binadamu na Shikamana na Mungu wako na atakuvusha...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila nasikiaga wanakwambia upotayari kutoa sadaka(kafara) na sadaka hiyo inapenda sa ndugu zako, watoto wako, wazazi wako hasa Mama....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binadam wote ni matajiri lakini kuna nguvu kubwa ya upinzani mkubwa wa nguvu za giza katika kuufikia huo utajiri...
wengi wanaoufikia ni wale waliovilinda viwili wili vyao kutoguswa na nguvu za giza either kwa madawa au maombi...

kuna sauti hutoka katka mind zetu zikitueleza nini tufanye/sisi ni akina nani bt ukiona inakua ngum kua vile ur mind inasema/unaenda kinyume chake tambua hapo ushachezewa na wachawi kuharibiwa riziki yako either unaweza ipata bt ikawa yakupitiliza or ikawa ngum kupita kiasi...

suluhu ni kukilinda kiwiwili either kwa kusali or kama huwezi hata kwa madawa, hapo kila kitu kitaenda sawa...

nb: ndagu haitakusaidia bt itakufanya mtumwa wa shetani ajili ya makafara.
 
Umemaliza mkuu....ndagu ataona maisha magumu...ingawa hela anakua nayo
 
Ndumba pekee ni kupambana na kukataa kukata tamaa, hakuna shetani wala mungu wakukutajirisha, niwewe mwenyewe. Pia kumbuka, haitatokea kila mtu akawa tajiri. Siku njema kwenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unauwezo wa kukomaa mpaka ukapata pesa ya kuendea kwa mganga, kwa nini usitumie juhudi hizo kujiimarisha kuichumi na hatimae kutoboa...

Cc: mahondaw
 
kama utani lakini hizi threads za watu kukata tamaa na maisha na kutaka kufanya mambo ya hatari zinaongezeka sana humu. mamlaka ziwe macho kiukweli. kuna ambao wamesharipotiwa kujitoa uhai humu!!!!
 
Back
Top Bottom