Dah! mapema mwaka huu? Hiv mhJafo anafaham maana ya mapema? Afu watu wengine wanapenda sifa eti mlitumia vibaya boom, hivi unajua watu wote wanapata asalimia mia? Je, unajua kuwa kuja kupata boom unakuwa una madeni lukuki, na baada ya boom la kwanza kwa linalofuatia hucheleweshwa sana hadi mipango ya bajeti kuvurugika? Unaposema mtu ajiajiri, mwalimu atajiajiri wapi? Serikali iache ukiritimba huu, mtu anakaa mtaani mwaka mzima ili hali kuna upungufu mkubwa wa walimu nchini pamoja na mrundikano wa wanafubnzi hasa baada ya elimu bure, visingizio vya hakuna pesa siyo vya msingi, serikali inakusanya mapato yake hadi kuvuka malengo kwa sasa, na ikumbukwa ajira za walimu mwaka huu ni kwa bajeti inayoisha muda wake yaani 2015/16 na si 2016/17 kama baadhi yetu tunavyopotosha. Hivi unahangaika na madawati wanafunzi wakakae tu darasani bila walimu? Mtu anayeleta dhihaka na kejeli asidhan anamkomoa mtoa mada bali halitakii mema taifa, mwalimu ndo anamuandaa mtaalam wa kufanya kazi viwandani hapo baadae, leo unategemea matokeo mazuri ili hali mwalimu 1 anafundisha wanafunzi 200 na kuendelea tofauti na idadi halisi ya wanafunzi 45, serikali inadai nchi haina walimu wa sayansi, leo unawakalisha mwaka mzima utadhani hjamna uhitaji. Where are we going as a nation?