Nimechelewa, Yamenikuta

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
NIMECHELEWA, YAMENIKUTA.

Na. Robert Heriel.

Nitaficha wapi uso wangu. Wapi nitajificha nisionekane. Dunia imenigeukia.

Walimwengu wananicheka. Ndugu, jamaa na marafiki wamenikimbia.

Wananisengenya. Hakuna aliye upande wangu. Loooh! Masikini Taikon wapi nitaficha uso wangu.

Hapo nikaichukua Album yangu ya kuhifadhia picha. Nikaifungua. Zilikuwa ni picha zangu nyingi sana. Ambazo nilipiga kipindi cha nyuma.

Zipo nilizopiga mwenyewe na zipo nilizopiga nikiwa na ndugu, jamaa na marafiki. Hapo nikaanza kufungua ukurasa mmoja baada ya mwingine nikizitazama, picha.

Kila picha ilibeba historia yenye kumbukumbu isiyofutika. Picha zote zilinikumbusha mambo yaliyoufanya moyo wangu uugue kusikosemeka.

Niliziona picha wakati nikiwa nasoma shule ya msingi. Hii picha nilionekana nikiwa nimebeba kidumu cha maji na fagio mkononi.

Picha hii ilinikumbusha enzi nikiwa nasoma elimu ya msingi huko kijijini kwetu, Makanya.

Kumbukumbu mbalimbali zilipita kichwani nikikumbuka maisha ya Makanya. Hapo nilikumbuka rafiki zangu niliokuwa nasoma nao. Wengine kwa sasa ni Marehemu. Mungu awarehemu.

Hapo nilishusha pumzi. Kisha nikafungua ukurasa mwingine. Na mwingine mpaka nilipofika kwenye picha iliyoibua simanzi moyoni mwangu.

Ilikuwa ni picha iliyomuonyesha Msichana mmoja aliyevaa Suruali na blauzi iliyomkaa vyema. Nilimtazama kama ndio siku ya kwanza kuiona sura hiyo. Kumbe sivyo.

Alikuwa ni mchumba wangu kipindi nasoma chuo. Wote tulikuwa tunachukua Shahada ya awali. Picha hii ilichukua kumbukumbu zangu mpaka katika ufukwe wa CocoBeach.

"Taikon nina mimba yako. Hapa nimechanganyikiwa. Ndio kwanza tupo Mwaka wa kwanza" Mchumba wangu aliniambia maneno yaliyonifanya nimchukie.

Ati unashangaa niliposema nimchukie. Ndio, nilimchukia mno. Sikutaka kuwa Baba kwa muda ule. Unajua kwa nini. Huenda unajua lakini acha nikuambie.

Sikuwa tayari kuwa Baba kwa muda ule. Hivi ningekuaje Baba ilhali bado kijana mbichi kabisa niliyetaka kuzisomba Raha za dunia. Nisijue kuwa ule ndio mwanzo wa kusombwa na mafuriko ya Raha za dunia na kunipeleka kwenye shimo la mauti.

Niliikataa ile mimba. Nikamwambia aitoe. Masikini Mchumba wangu aliitoa lakini bahati haikuwa wake. Alipata majeraha mabaya yaliyopelekea apate saratani ya kizazi. Kinachonitoa machozi muda huu.

Kinachoniliza na kuuchoma moyo wangu ni kuwa sikuenda hata kumuona mchumba wangu mpaka anakufa. Alikufa kifo cha uchungu sana. Sitaki kuelezea hata ujumbe wake wa mwisho alionitumia. Inauma jamani.

Ona! Nimekumbuka, kumbe hata sikuenda kwenye msiba wake. Wanachuo wenzangu walienda kumzika mchumba wangu mimi nikiwa nipo na mwanamke mwingine. Loooh! Taikon Mimi.

Kumbukumbu zilizimika na akili yangu ikarudi kwenye ile picha ya mchumba wangu iliyokuwa kwenye Album. Muda huo machozi yalikuwa tayari yapo mashavuni.

Nikafungua picha zingine kwenye ile Album. Tena na tena nikafungua. Hapo niliduwaaa. Nilitoa macho ya kuhamanika. Ilikuwa ni picha niko na familia yangu. Nilikuwa mimi, Mke wangu na watoto wetu.

Picha ile ilituonyesha tukiwa kwenye Bembea. Mimi na mke wangu tukiwa nyuma ya watoto wetu waliokalia bembea. Wote tulikuwa tumetabasamu. Hii picha niliitoa kwenye Album nikaishika mkononi. Kisha nikasimama nikitembea tembea nayo mule chumbani.

Mpaka kumbukumbu zilipokuja ndio nikawa siioni ile picha ingawaje nilikuwa nimeiweka usawa wa macho yangu. Nilikumbuka miaka kadhaa nyuma iliyopita. Nikiwa tayari nimeoa na kupata watoto.

Kumbukumbu zilikuwa nyingi kupitia picha hii. Nilikumbuka maneno mengi ya mke wangu.

"Mume wangu, miaka inaenda. Tutapanga mpaka lini. Tujenge nyumba. Ni bora tukajenge hata kijijini kuliko kukaa mjini lakini hatuna hata nyumba"

Mke wangu aliongea. Maneno hayo ambayo ni hekima tupu lakini nilimuona hamnazo. Nilimwambia kama ni kujenga tutajenga.

Kazi tunazo, pesa tunayo. Hatuna haja ya kuharakisha. Nilimuambia siwezi kuishi shamba. Mimi sio Mkulima wala sio mfugaji. Mimi sio muwindaji. Sasa iweje nikae kijini.

Nilikumbuka siku niliyofumaniwa na Mke wangu nikiwa na kimada ndani ya nyumba. Looh! Mke wangu alilia sana. Aliongea maneno ambayo mpala leo yanacheza kwenye akili yangu. Hata hivyo pamoja na kulia kwake lakini sikumuonea huruma. Nilikuwa kama Bokasa kama sio Nduli nisiye na huruma.

Sikumuonea huruma Mke wangu. Mama wa watoto wangu. Mwanamke aliyenipenda na kuniheshimu. Lakini mimi nilimlipa mateke kama shukrani ya punda. Sitaki mimi! Sitaki kukumbuka.

Alikufa! Alijiua yeye na watoto wetu kwa sumu. Nilijua hivyo kwa kupigiwa simu na Housegirl wetu. Moyo uliniuma sana. Sikutegemea angefikia maamuzi makubwa kiasi kile.

Mimi ndio chanzo cha kifo cha familia yangu. Mimi ndiye muuaji. Nilisababisha kifo cha Mchumba wangu aliyekufa kwa kutoa mimba na sasa nimesababisha kifo cha mke wangu kipenzi. Nitakuwa mgeni wa nani sasa. Looh!

Nilirudi kwenye ile picha uso ukiwa umelowa machozi mikono ikitetemeka. Kutokana na macho kujaa machozi ile picha sikuiona vizuri tena. Niliona inamawimbi mawimbi kama lenzi. Nilijifuta machozi.

Sasa nikarudi kwenye Album kuendelea kuangalia picha zingine. Nilipita picha nyingi mpaka niliposimama kuliko na picha iliyoshika ufahamu wangu. Ilikuwa ni picha iliyonionyesha nikiwa nimevaa suti iliyonyooka pembeni yangu akiwa amesimama Mwanamke mrembo aliyevalia Kisketi kifupi kilichoshika mapaja yake manene mazito yenye hipsi zisizohitaji nyongeza. Huyo alikuwa ni mhasibu katika Kampuni niliyokuwa nafanya kazi.

Nilianza mahusiano ya kimapenzi na Muhasibu wa kampuni yetu. Tulipeana raha bila kujua kuwa kuna karaha. Tukapeana utamu bila kujua kuna uchungu.

Basi kumbe Meneja naye alikuwa anamtaka huyo mwanamke, Mhasibu. Bila kujua nilijikuta katika vita baridi ya penzi tukimgombania Mhasibu. Mimi sina hili wala lile nikashangaa nimelimwa barua ya kufukuzwa kazi. Sasa palizi nitalifanyia kitaani.

Umri umeenda, sina kazi, sina pesa, sina nyumba, sina Familia. Maisha ya kuendesha mandinga yamebadilika. Kwa sasa Maisha yananiendesha tofauti na awali.

Kijijini sitaki kurudi. Kwa wazazi naona aibu kwenda. Sikuwajali kipindi ninapesa. Sikuwathamini kipindi nina kazi. Aibu ipo utosini mpaka miguuni.

Nyumba yangu haina rafiki isipokuwa nzi, mende na panya. Hawa kwa sasa tumekuwa marafiki wa kuzikana. Tunapendana mno. Nje sitaki kutoka. Nitoke watu wanizomee. Nitoke ili watu wanisimange. Loooh!.

Nimechelewa na yamenikuta. Yamenikuta nikiwa na mvi. Akheri yangenikuta nikiwa bado kijana mdogo ninanguvu zangu. Ningepambana. Lakini Yamenikuta nikiwa sina nguvu.

Nimechelewa kuomba msamaha kwa Mchumba wangu. Kwa mke wangu na familia. Wamekufa bila kunisamehe. Nimechelewa sasa yananikuta huku.

Nimechelewa kujenga nyumba. Sasa yananikuta kutolewa kwenye nyumba hii niliyopanga. Kodi yangu inaisha mwezi huu.

Sina pesa ya kulipa kodi. Hata nikisema niwauze hawa panya, au hawa mende na nzi bado pesa haitatosha hata ya kulipia kodi.

Nimechelewa sasa yananikuta. Kurudi kijijini siwezi. Kurudi kwa Wazazi naona Aibu.

Mbaya zaidi sijui kiafya kama kweli nitasalimika au ndio tayari nimeukwaa. Looh! Nimechelewa kutambua hekima.

Hapo nikafungua Ukurasa wa mwisho wa ile Album. Hapo nikakuta maandishi ya wimbo ambao aliuandika Mke wangu miaka ishirini iliyopita. Wimbo ulikuwa huu;
"Muda hauendi ukarudi,
Nafasi haiji ikarudi,
Maisha ni leo weka juhudi,
Usisubiri kesho, leo ikibidi"

Wimbo huo ulimaliza Mlolongo wa Album yangu yenye picha mbalimbali.

Hapo nikaifunga Album. Roho ikiniuma huku tumbo likiwa na njaa ya siku mbili. Madeni kila kona yanayonipa msongo wa mawazo.

Punde nilidondoka sakafuni. Macho yakawa mazito nikawa sioni vizuri. Njaa na msongo wa mawazo vinanifanya nikazimia.
Hatimaye macho yakafumba kukawa giza machoni na ubongoni. Mwisho kukawa kimya.

Niite Taikon wa Fasihi. Mtu kutoka nyota ya Jibi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
0693322300
 
Sawasawa mkuu nimependezewa na huo wimbo wa;

"Muda hauendi ukarudi,
Nafasi haiji ikarudi,
Maisha ni leo weka juhudi,
Usisubiri kesho, leo ikibidi"
 
Back
Top Bottom