Kwani kulikua kuna tuzo ya msanii aliyechuma pesa zaidi au tuzo ya msanii anayejaza mashabiki wengi kwenye tamasha?
Mkuu hapa ndipo utata ulipo
Ni nini mmasharti na vigezo kumpata mshindi?
Kwa KTM inaonekana vigezo ni kura pekee ndio huamia mshindi, na kama hilo ni kweli basi Ali Kiba ana haki yakupata tuzo hizo iwapo kura zake zilikua nyingi Kuliko washindani kwa kila kategori
Tatizo la maamuzi ya kura pekee ndio huleta malala miko kama haya tunayo yaona, kura haiangalii vigezo vingine as long as umekua nominated
Tuzo nyingi kura hubeba asilimia fulani tu ya maamuzi na jopo la majaji wataalamu wanaangalia others factors
Ukiondoa vigezo vya kura kupata mshindi, Chibu amefanya vizuri sana mwaka jana kuliko Ali kiba katika nyanja zote, na ndio maana mwaka huu utaona malalamiko mengi tofauti na mwaka jana
Mwaka jana Chibu ni kama alikua peke yake tu hakuwa na mtu aliyefanya vizuri sana zaidi yake so alipochukua tuzo saba kura na others factor zikawa sawa na ikaonekana ni sahihi na haki yake
Mwaka huu tofauti kidogo, Chibu katengenezewa "mpinzani" ambaye amefanya vizuri kiasi chake, na kwenye kura nyingi zikapigwa kwa Kiba na ameshinda
Sasa shida imekuwa ni vipi kuhusu others factor?
Kweli Kiba ana ubora kuliko Diamond hadi kumzidi tunzo zote hizo?
Jibu ni HAPANA, ila ameshinda kihalali sababu ya vigezo na masharti ya only kura na si kwasababu Kiba ni bora kuliko Diamond