club6
Senior Member
- Apr 11, 2014
- 157
- 61
Habari kwa wahitimu wote wa kidato cha sita na wahitimu wote wa stashahada mwaka 2016. Ni dhahiri kumefanyika mabadiliko makubwa Katika bodi ya usajili vyuo vikuu hii imehusisha mabadiliko ya viongozi wa bodi pamoja na baadhi ya miongozo ya usimamizi.kwa wahitimu wa kidato cha sita,wanafunzi watakao pata daraja la kwanza na la pili yaan division one na division two ndio watakosajiriwa kwa elimu ya shahada yaan degree na kwa wale watakaomaliza diploma ni wale watakaopata hazini ya ufaulu Kuanzia 3.3 na kuendelea yaani GPA ya 3.3.kwa wahitimu wa kidato cha sita watakaopata daraja la tatu yaani division 3 watasoma stashahada adhiri yaani special diploma hii itachukua na wahitimu wa stashahada ambao hawakukidhi viwango. Ieleweke wazi hakutakua na usajili wa wahitimu watakao pata daraja la nne na wale watakaopata GPA chini ya 3.3 kwa wahitimu wa stashahada pia hakutakua na mkopo wa wanafunzi wa stashahada adhiri kama ilivyokua awali,Bali patakuwa na punguzo la ada la asilimia 35 kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka 2016/2017.