Nimechanganyikwa naomba mawazo yenu wanajf wenzangu.


ASANTE kwa ushauri wako,
kuanzia jumatatu itabidi nifanye kazi ya kuzunguka vyuoni na kuonana na watu wa administration ili nifahamishwe zaidi nitakiwacho kufanya.
Hata kwa ngazi ya cheti nipo tayari kuanza ili mradi nipate ujuzi mwingine.
SAMAHANI KWA LATE REPLY.
 

ASANTE KWA KUNIPA MOYO ZAID,
Nimeumia sana ,PIA KUFELI KUNAUMIZA MNO,
Wakati mwingine nahisi kama naota,
Lakin sina budi kujipangusa na kuendelea na safari ya kutafuta elimu,
huku nikiamini kuwa ipo siku ntatimiza ndoto zangu.
Mawazo yenu ni fimbo yangu ya kunyanyukia, ASANTE SANA.
 
mkuu we waza kuresiti mitihan usiogope na mungu akukunyima upande wa pili mashallah komaa na shule muulize shyrose banji akwambie umuhimu wa kurisiti mtihan..

NASHUKURU SANA Pdidy,
kwa kunipa mawazo ya kuniinua tena imani yangu juu ya elimu,
na safari ya kuelimika mtu kama miye ninayehitaji sana kutoa,
tongotongo la ujinga akilini mwangu,pamoja na kuwa na ufahamu
mpana juu ya elimu.
Shukurani sana ,nimekuelewa vizuri.
 

Asante sana Asha D,
nashukuru umetambua juhudi zangu japo hazijazaa matunda mazuri,
lakin sina budi kujifunga mkanda na kuendelea.
Watu wengine wanafika kwenye vilele vya mafanikio pasipo vikwazo vingi sana,
lakin mtu kama mimi naona nahitaji kujituma na kuongeza mapambano zaidi,
ili nami siku moja nilie kivulini.
Shukurani nyingi kwa mchango wako,
samahani kwa late reply jana ilinisumbua ku log in.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…