Nimechanganyikiwa !!!

della

New Member
May 22, 2008
4
0
Nawashukuru kwa kunipokea katika JF.
Naamini kabisa ni mahali pa watu kupata msaada wa kimawazo,n.k.Nilikuwa natafuta ni wapi pa kusemea ,naona labda nianzie hapa naombeni ushauri.. sijui nianzeje.

Mimi nina mtoto mmoja.namtaunza mwenyewe tu kwa kila kitu, baba yake yupo ila anajifanya kama haoni na ana uwezo ,na mara ingine akikutana na marafiki zake anaanza kujisifia ..kwangu sioni tatizo ila niliamua baada ya kukaa muda mrefu sina mtu wa karibu wa kuongea nae nikapata boyfriend,mimi kwa kweli sielewi huyu (naweza kusema sio type yangu)sijui kanitokea wapi? najiuliza,Approach yake,utanashati kwa kweli nikaona nimepata mtu na anaongea kwa busara,
Nimekuwa na uhusiano nae kwa muda wa miezi kama 3 tu ila nimegundua tabia na mwenendo wake si mzuri hata kidogo,makucha yake yalianza kujitokeza pale nilipogundua ana mke anaishi nae,mke alinipigia na kuniambia tuonane mimi ni mke wa jamaa.Jamaa akanikatalia sana nisionane na mkewe nimegundua pia kwamba kwa mkewe yeye amejiweka ni mlokole pai amebadilisha kabila ,simjui ndugu yake hata mmoja ila ni marafiki tu .Jamani najuta mimi!!!
watu husema za mwizi ni arubaini ,tabia ingine ya huyu jamaa ni dhuluma sasa kaenda kumdhulumu mke wa mtu mwingine ndio yakaja mambo yote ya huyu jamani ni kwamba ameathirika siku nyingi sana! kuna mwanamke alifiwa na mume yeye alikuwa anatembea nae maana anapenda sana dezzo.haikutosha yupo mwingine amefariki mwisho wa mwezi wa tatu 2008 nae alizaa nae mtoto alifikisha umri wa 8 months.akafariki,(sio kwamb natunga jamani ni ya kweli na aliesimulia ni rafiki yake mpenzi na one of the inlaws wa huyu mwanamke aliefariki mwisho wa mwezi wa tatu),nilijiona mdogo kama piriton nilihisi kama moyo umeruka mapigo yake ,sio hayo tuu hapo anapoishi jamaa an mwanamke mwenye mtoto mchanga wa umri wa miezi 4,pia ametelekeza mke na watoto 4 wanateseka kweli,jamaa anchukua watoto wa shule tena wachafu wachafu akiwahonga sana ni 500.00!!akishavuruga anakutema anachukua mwengine ,jamani nimfanyeje ?sasa iv anaishi kam digidigi, kwa kuniogopa labda nitamshataki au chochote, anavyodai,mimi jamani ntaenda wapi nahisi nimeukwaa ntawaambiaje ndugu zangu??wazazi je? jamii ndio kabisa sijui nitaitazamaje ..nisaidieni naogopa kwenda kupima maana mpaka sasa sio siri naona mapigo ya moyo yanasimama kila saa.kazi naharibu,siwezi hata kula ,,jamani naombeni uashauri wenu, Najuta mimi.
 
Della,

Kwanza karibu tena Hapa JF, mimi sio medical personell lakini nilikuwa nafanya kazi na waathirika hadi miaka miwili iliyopita nilibadili kazi. Kikubwa upo uwezekano mkubwa kwamba hujaathirika ingawa inaonekana mlikua hamtumii kinga(condom).

Huna sababu ya kupanic wala kuwaza sana bila kula maana utaudhoofisha mwili kinga itangua na hata kuwa attacked na magonjwa ya kawaida na hata kupoteza maisha wakayi hata huo UKIMWI hauna.

Kama mmekuwa wapenzi kwa kipindi cha miezi mitatu ni kipindi tosha cha wewe kwenda kuangalia afya yako. Kupima kutakusaidia sana kupunguza hisia mbaya, hofu, na msongo wa mawazo ulio nao.

Lakini pia kupima inahitaji moyo, ila ndio njia muafaka ya kutuliza nafsi yako kuondokana na hisia zote ulizo nazo. Lakini ujue ukipima na kujua afya yako itakusaidia kujua njia gani ufuate namna gani ujilinde na watu wengine wenye tabia kama ya huyo bwana ili usije ukawa hujaathirika lakini kwa sababu umekata tamaa uakenda kwenye mtego wenyewe .
 
Pole sana dada della!mimi ningekushauri kapime kwanza!kama umeathirika utapewa ushauri wa kidakitari!kuwa na HIV siyo mwisho wa maisha!utaishi na utamtunza mwanao bila wasiwasi!
Inawezekana pia hujaambukizwa!hivyo basi dawa ni kwenda kupima!
Jipe Moyo mkuu muombe MUNGU akutie nguvu kweli ni ngumu lakini kwa MUNGU yote yawezekana kwake yeye aaminie!
Uwe na Amani!ukimwi ni ugonjwa kama magonjwa mengine!sema umekuwa mediatised sana!
 
Pole sana dada Della kwa yaliyokukuta kama walivyokushauri wengine huna aja ya kuogopa nenda ukafanye vipimo ujijue utaishi vipi. Kuwa na UKIMWI si mwisho wa maisha. Nakuombea Mungu akupe ujasiri wa kwenda kupima.
 
Kwa mrorongo wa matukio hayo ambayo umeeleza dada della nenda kapime.Kama ukikuta huna ukimwi...shukuru mungu kwani itakuwa ni bahati sana na ujue mungu yu nawe bado.

Anataka kuona ukibadilika kimaisha zaidi ya hayo uliyo nayo....kwa sasa ni hilo ukisha pima welcome back tutakuwa na maelezo zaidi....its all about possibility ya kuwa nao au kutokuwa nao..

Good lucky and pole sana kwa kuingia kwenye ungo wa huyo bwana.
 
Pima Ujue Una Hali Gani Unaweza Ukawa Mzima Ila Kwakua Una Mawazo Mengi Basi Unaweza Jimaliza Kwa Mawazo Tu.

Pole Sana Ila Kapime Ndugu Yangu
 
Kilinzibar natoka nje ya mada hiyo picha yako imebidi nicheke kabla ya kosoma ulichoondika
 
Kwanza uache mapepe pili huyo jamaa alikuwa anabipu tu,tatu wako wengi sana wa dizaini hiyo, nne kumbuka kuwa usilete emotions zako kwa mtu usiyemjua especially katika suala la mapenzi.Kwa sababu the other party atatumia kigezo hichohicho kukutia mikononi mwake. Tano nyie mademu mmezidi sana sio wewe peke yako wako wengi sana wa dizaini yako. Sita mimi ninakushauri uache kugawa uchi kama pipi tena bila kinga.
 
Dada jitahidi, jipe nguvu upya uende kupima japo ufahamu una hali gani ila ningeona ni bora kwanza uupitishe muda kidogoi kama janga hili limwekutokea mapema, kama ni la muda basi amini kuwa Ukimwi ni kama mafua tu, kwanza kufanya tendo la ndoa si kuwa na ukimwi so kama limekutokea hivi karibuni jitahidi upate walau miezi mitatu kisha akili ikitulia ndio ukapime, maana ukiwa hot kiivo unaweza kuambiwa huna ukasema wanakudanganya!!
 
Mdogo Wangu Pole Sana,kwanza ,wewe Ni Jasiri Sana ,na Kwakuandika Haya Umepunguza Tatizo Moja Kati Ya Kumi,

Nisikilize Kwa Makini,nenda Ukapime Kama Haujaathirika Basi ,ni Salama,nakama Umeaathirika ,bado Sio Mwisho Wa Dunia,kuanzia Saa Hii Utakayosoma Hii Message Anza Kuhesabu Ni Wangapi Mungu Amewachukua Kwa Vifo Vya Kawaida Tu ,such As Malaria ,accident Etc.ni Wengi Sana,so Wewe Unaweza Kuishi Hata Miaka 50,ni Kuzingatia Masharti Tu ,na Kumuomba Mungu Pia ,usikate Tamaaa Kabisa ,kwanza Ndio Uanze Maisha Upya ,na Huyo Mtu Ni Vyema Umkanye Asiendelee Kuambukiza Wengine ,atunlie Atunze Familia Yake.
 
Pole sana, nausijali nenda kapime na ukijua ukweli utaishi maisha mazuri kuliko kuwa na wasiwasi.
 
tafadhali KAPIME, KAPIME, KAPIME, KAPIME, KAPIME, KAPIME............then uta-come back na majibu, hii ni forum yenye vitengo vyote vya kukusaidia wewe.
 
Kwanza uache mapepe pili huyo jamaa alikuwa anabipu tu,tatu wako wengi sana wa dizaini hiyo, nne kumbuka kuwa usilete emotions zako kwa mtu usiyemjua especially katika suala la mapenzi.Kwa sababu the other party atatumia kigezo hichohicho kukutia mikononi mwake. Tano nyie mademu mmezidi sana sio wewe peke yako wako wengi sana wa dizaini yako. Sita mimi ninakushauri uache kugawa uchi kama pipi tena bila kinga.

Duh...
Too straight...but its the hard truth...

Anyway i think Della unastahili kwanza kupima na ujue baada ya kupima una mawili either uishi kwa matumaini kama muathirika au uishi vile vile kwa matumaini na kubadili tabia kama asiye muathirika!!

Pili naomba ujue kwamba wewe sio wa kwanza kupatwa na hali kama hiyo kwa hiyo nafurahi kuona umepata hata ujasiri wa kuja JF kupata japo ushauri. Jitahidi kuituliza akili yako.
 
Thanks wanaJF mliopata nafasi kumjibu Della, the best thing really ni kupima, you never know labda umepona, usijiue bure na mawazo bora kupima ujue hali ilivyo then can you only live a meaningful life.The worst fear is the fear of the unknown, get the courage and do the right thing!
 
Della.
Ningekushauri ukapime ili kama umeathirika uanze kutumia ARVs. Kuwa muathirika haimaanishi kuwa utakufa mapema. Nina jamaa yangu ambaye sasa ni zaidi ya miaka kumi tangu aathirike lakini ukimwangalia kwa nje, ana afya yake nzuri tu kutokana na dawa anazokunywa na anafanya shughuli zake kama kawaida. Mgonjwa ni yule aliyelazwa hospitali. Usisubiri mpaka uanze kuugua.
 
Kila mtu ukapime, ukapime......., hebu kupima unadhani mchezo? acheni hizo,kama ungekuwa wewe ungekurupuka ukapime? nadhani yeye dada Delle, ana njia moja tu ya kumsaidia, ni kwenda pale kwa Kakobe kwanza, (kama yuko Dar na kama hayuko dar atafute kanisa la watu waliookoka atapata salama yake)atiwe imani kuwa hana ugonjwa huu, kisha hatakua nao kamwe,Amini.
 
Nawashukuru kwa kunipokea katika JF.
Naamini kabisa ni mahali pa watu kupata msaada wa kimawazo,n.k.Nilikuwa natafuta ni wapi pa kusemea ,naona labda nianzie hapa naombeni ushauri.. sijui nianzeje.

Mimi nina mtoto mmoja.namtaunza mwenyewe tu kwa kila kitu, baba yake yupo ila anajifanya kama haoni na ana uwezo ,na mara ingine akikutana na marafiki zake anaanza kujisifia ..kwangu sioni tatizo ila niliamua baada ya kukaa muda mrefu sina mtu wa karibu wa kuongea nae nikapata boyfriend,mimi kwa kweli sielewi huyu (naweza kusema sio type yangu)sijui kanitokea wapi? najiuliza,Approach yake,utanashati kwa kweli nikaona nimepata mtu na anaongea kwa busara,
Nimekuwa na uhusiano nae kwa muda wa miezi kama 3 tu ila nimegundua tabia na mwenendo wake si mzuri hata kidogo,makucha yake yalianza kujitokeza pale nilipogundua ana mke anaishi nae,mke alinipigia na kuniambia tuonane mimi ni mke wa jamaa.Jamaa akanikatalia sana nisionane na mkewe nimegundua pia kwamba kwa mkewe yeye amejiweka ni mlokole pai amebadilisha kabila ,simjui ndugu yake hata mmoja ila ni marafiki tu .Jamani najuta mimi!!!
watu husema za mwizi ni arubaini ,tabia ingine ya huyu jamaa ni dhuluma sasa kaenda kumdhulumu mke wa mtu mwingine ndio yakaja mambo yote ya huyu jamani ni kwamba ameathirika siku nyingi sana! kuna mwanamke alifiwa na mume yeye alikuwa anatembea nae maana anapenda sana dezzo.haikutosha yupo mwingine amefariki mwisho wa mwezi wa tatu 2008 nae alizaa nae mtoto alifikisha umri wa 8 months.akafariki,(sio kwamb natunga jamani ni ya kweli na aliesimulia ni rafiki yake mpenzi na one of the inlaws wa huyu mwanamke aliefariki mwisho wa mwezi wa tatu),nilijiona mdogo kama piriton nilihisi kama moyo umeruka mapigo yake ,sio hayo tuu hapo anapoishi jamaa an mwanamke mwenye mtoto mchanga wa umri wa miezi 4,pia ametelekeza mke na watoto 4 wanateseka kweli,jamaa anchukua watoto wa shule tena wachafu wachafu akiwahonga sana ni 500.00!!akishavuruga anakutema anachukua mwengine ,jamani nimfanyeje ?sasa iv anaishi kam digidigi, kwa kuniogopa labda nitamshataki au chochote, anavyodai,mimi jamani ntaenda wapi nahisi nimeukwaa ntawaambiaje ndugu zangu??wazazi je? jamii ndio kabisa sijui nitaitazamaje ..nisaidieni naogopa kwenda kupima maana mpaka sasa sio siri naona mapigo ya moyo yanasimama kila saa.kazi naharibu,siwezi hata kula ,,jamani naombeni uashauri wenu, Najuta mimi.

Pole sana dada ! lakini kama unachosema ni kweli, basi ninaweza kukusaidia ! Kwanza upo dar sehemu gani ? kama vipi naweza kuwasiliana na watu then wakamuweka kwenye uchunguzi na tabia zake huyo jamaa, na ikithibika then achukuliwe hatua za kisheria !

Pole sana, lakini hakuna haja ya kuwa na wasi wasi ila kuwa mwangalifu zaidi !
 
Wewe ndio umetoa point ya kumsaidia huyu dada etu. Kwa kuongezea tu, kwa sasa usivue kabisa, kauka. Inawezekana kabisa hujaambukizwa na inawezekana hata jamaa mwenyewe hana. Sasa, wewe tulia kwanza. Uamuzi wa kupima uwe ni wa kwako tena usiende kwa shinikizo wala pupa. Halafu utakaamua sehemu ya kupima uwe makini katika kuchagua hiyo sehemu; kuna sehemu kibao wana lostisha.
 
Pole dada LAKINI ngoma hauna.
Binamu yangu alikufa miaka 13 iliyopita kwa ngoma iliyothibitishwa hospital. Death certificate ninayo kwa sabu mimi ndo nilishughulikia ishu ya kifo chake. Alikuwa na mademu 11 ninao wafahamu. Kati ya hao ni mmoja tu aliyekuwa amemuambukiza ngoma japo alikuwa hatumii condom kwa mademu wote. (Alikuwa totally against using condom)

Ninachotaka kusema ni kwamba unaweza ukawa ume-save kimtindo.
Hata kama umepata ngoma usiwe na wasiwasi. Watakufa wengi tu na maralia, TB, Cancer, etc kabla wewe haujarudisha hiyo namba, na wadogo kwa umri kuliko wewe, kwani wao wanakosa gani kwa mungu sasa?
Tulirithi dhambi ndio maana tunakufa; dying shouldnt be a suprise to you, you nkow what i'm saying? Sote njia moja na unapokufa unakuwa umeshalipia dhambi zako, haudaiwi tena na Sir God, Biblia inatuambia. Unakuwa umeenda kupumzika, kwani hapa duniani ni shida tu. Unapokufa hauendi popote, si motoni si peponi, you simply cease to exist. Wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi!!!!!
Usiogope kifo kwa sababu karibu wafu wote watafufuliwa hivi karibuni, yaliyotabiriwa yote yametokea. Kwa hiyo basi ukifa hata kesho, kufa ukijua karibu utafufuliwa!!! Cha msingi mrudie mungu, fanya kazi aliyokuleta hapa kufanya, hakukuleta duniani kuwaridhisha ma-boy friend wanaoambukiza ukimwi.
Kama hujui upo hapa kufanya nini tuwasiliane kwa email okon35@yahoo.com. Ntakupa somo na utaona kwamba kumbe haupo hapa duniani kwa bahati mbaya. LAKINI KUBWA KULIKO YOTE NI KWAMBA UNAWEZA UKAWA HAUJAAMBUKIZWA KWA SABABU MUNGU ANATAKA KUKUTUMIA.
Halafu hizo hofu zote ulizonazo zinafutika mara tu unapoacha kumtumikia shetani na unapoanza kumtumikia Mungu (I mean YEHOVA, siyo mungu alimradi mungu). Halafu hauna haja ya kubeba hilo zigo zito hivyo (HOFU) wakati JESUS amekwambia NJOONI ENYI NYOTE MNAOLEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA!!
Yehova akupe hekima utambue ninayosema. KWA JINA LA YESU KRISTO. AMINA
 
Last edited:

Similar Discussions

Back
Top Bottom