Nimechaguliwa kinyume cha sheria - Naibu Meya mteule Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimechaguliwa kinyume cha sheria - Naibu Meya mteule Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Dec 20, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Diwani wa Kata ya Sokoni kupitia TLP, Michael Kivuyo amesema Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo wa CCM pamoja na yeye wamechaguliwa kinyume na kanuni ila kinachopaswa kufanywa na Chadema ni kufuata taratibu za kisheria na sio kuleta vurugu na kutuhumiana kwani huo sio wakati muafaka kwa sasa.

  'Meya amechaguliwa kinyume na kanuni na hata mimi nimechaguliwa kinyume na kanuni sasa Chadema wanalia nini? Sheria si ziko wazi, mahakama zipo kwa ajili ya watu wafuate taratibu kudai haki zao za msingi na sio kulaumu watu eti nimenunuliwa?" alisema Diwani huyo wa Sokoni One.

  Alisema kanuni ziko wazi na hata kipofu anajua hilo na kinachopaswa kufanywa na Chadema ni kwenda katika vyombo vya sheria na sio kuleta vurugu na kupayuka ovyo barabarani.

  Kifungu cha 8(3) kinaeleza bayana kuwa uchaguzi utafanyika kwa wajumbe (madiwani) kufika theluthi mbili na hilo ndilo tatizo kwa CCM wako 17 pamoja na diwani wa TLP, lakini sheria inakinzana na hilo na ili uchaguzi ufanyike lazima kuwe na wajumbe zaidi ya 21

  Habari Leo:
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huyo diwani wa TLP anapashwa apigwe mawe mpaka kufa kwa kitendo chake cha kukubali kununuliwa na kukubali kuuza utu wake na kukumbatia vibaka wa demokrasia.

  Tiba
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Yee uuuwi! Tiba, taratibu mzindawangu! taratibu mzalendo, Mawe hadi msiba !Ooops! Punguza munkari mkubwa.
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mfano wa Arusha ni muendelezo mwingi tu wa uvunjaji sheria na hali ya watu kuendelea kuamini kuwa wapo juu ya sheria. lakini hata hivyo CHADEMA wanalo la kujifunza. Hawa CHADEMA walikataa alliance na vyama vya TLP, NCCR mageuzi na UDP kwa madai kuwa vinatumiwa na hatimaye kuzua mtafaruku na CUF. Lakini pia CHADEMA hawa wanataka waungwe mkono na TLP kwenye chaguzi zao nyingine. Hapa ndio ambapo watu wengi hujiuliza uwezo wa CHADEMA uko wapi. Inaonekana wanaona sasa hivi lakini hawawezi kufikiria mbeleni.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,648
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  Kilichotokea Arusha ni picha halisi ya jinsi CCM inavyoibaka demokrasia ya nchi hii,wanacholalamikia Chadema juu ya uchakachuaji wa kura za urais ni negative sasa kule Arusha picha ndiyo imesafishwa kila mtu aione vizuri. Matumizi ya Polisi,Msimamizi wa uchaguzi,kununua wapinzani (diwani wa TLP), hapa hakuna shaka CCM ni mafia, ndiyo maana hata mimi naunga mkono hoja kuwa JK ni rais wa NEC,TISS,POLISI &MAFISADI, kamwe hakushinda. Loo RAIS MWIZI, tumekwisha.
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi huyo diwani wa TLP aligombea? Alijieleza wakati wa uchaguzi? Alipochaguliwa akijua ilikuwa kinyume cha kanuni, je alikubali uchaguzi huo?
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyo amehongwa, katika hali ya kawaida huwezi kuchaguliwa bila kufuata sheria na wewe unakubaliana. kimsingi yeye ndo alitakiwa akatae nafasi hiyo kama yeye ni mpenda haki.

  Ndio sababu Chadema wakisema TLP, NCCR, CUF si wapinzani wa kweli.


  Peoples Power.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo Diwani hana hata aibu japo kidogo, anakuja hadharani kukiri kwamba hakuchaguliwa kihalali na wakati huo huo "anatoa ushauri" kwa chadema.
  Kweli mwaka huu tutashuudia vituko vingi vitakavyobaki kwenye kumbukumbu za kihistoria.
   
 9. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sasa kama alijua hajuchaguliwa kihalali kwanini alikubali hiyo post...! Hizi politics za mwaka huu na upinzani feki wa hawa wajukuu wa lyatonga sijui mwisho wake wapi...! Dawa yake ni kumyima hata ubalozi 2015...!:redfaces:
   
 10. sbilingi

  sbilingi Senior Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila mimi nakuja kuamini kwamba haya yote ni sababu ya mwenyekiti wetu kutowashirikisha kwenye kinyang'anyiro cha kambi ya upinzani.
   
 11. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Acha uzandiki wewe......
   
 12. m

  mams JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wahusika si wajisarimishe polisi. Hapa kuna utata, Diwani anachaguliwa kwa simple majority au 2/3 ya wajumbe. Na kama kikao hakikua na wajumbe 2/3 kwa nini kiliendelea kufanyika na kuchagua meya na naibu wake. Kama kikao hakikuwa na 2/3 maana yake kilikuwa batili na kikao batili matokeo yake hufanya maamuzi ambaya ni batili kwa hiyo meya na naibu wake wote siyo halali. Ugumu wa sheria uko wapi hapo?
   
 13. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ugumu hapo ni kwamba Sasa hivi ni wizi mtupu!
  Toka JUU mpaka chini
  Hao akina Meya wanafuata tu mfano na ukileta za kwako tutakubambika Bange na tukupigeeee tukuvunje kiuno!
  Du! naanza kumlaumu aliyetuanzishia sisiemu!
   
 14. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Huyo Diwani ni kimeo sana,
  Inaonekana amefutwa na wenye busara na kumpa vifungu ndiyo leo kageuka.
  CDM ni wapinzani pekee TANZANIA,
  Vyama vingine ni Fuata Upepo!
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huyu diwani hamnazo nini ndio anasema nini sasa? si bora kukaa kimya tu.

  mimi simwelewi anadai kwamba kiti alichokalia kina kasoro na bado kakikalia!!!!!!!!!!!
   
 16. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kuna mwanamuziki mmoja aliwahi sema hivi nanukuu" Since, the fools are now ruling the smart, then Am now starting to believe that foolishness is a brach of Science" Huyu diwani ni mjinga sana lakini kutokana na sentensi hiyo hapo juu sina comments zaidi!
   
 17. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh!!!!!! Na wakati uchaguzi unafanyika wengine walikuwa wapi??
   
 18. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  Si KWELI KIVUYO HAWEZI SEMA HIVYO ANANJAA KALI NAMJUA,HUU NI UZUSHI
   
 19. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo Mh. Mizengo Pinda ataonyesha iwapo yeye kweli ni muadirifu ama hiyo taswila yake ya uadilifu ni ya mpakazo tu, inayomfanya aonekane kama kondoo wakati katika hali halisi ni fisi. Kwani haina budi ieleweke ya kuwa yeye ndiye waziri wa sirikali za mitaa, na hivyo ikiwa kweli uchaguzi wa meyor na naibu wake huko Arusha umefanyika kinyume na sheria, hakuna sababu yeyote kwa Pinda kunyamazia uovu huo, ambao kama ukiachwa kutatuliwa kwa njia ya mkondo wa sheria utateketeza mabilioni ya fedha ya walipa kodi. Hivyo kama mtu mwenye uchungu na nchi hii, tunatarajia atatumia madaraka aliyo nayo chini ya sheria kutatua mgogoro huo nje ya mahakama.
   
 20. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  CCM wana kazi moja tu ..........................
  Kuondoa wazee kwenye nafasi muhimu za chama ili kurudisha heshima ya chama hicho otherwise wataleta MAAFA. Kinachotokea hivi sasa nchini ni wazee wa CCM kutumia mbinu za miaka ya sabuni kueneza propaganda UCHWARA wakidhani Watanzania hawana uwezo wa kutafuta habari kwenye vyanzo vingine! Haingii akilini kuona miji yote penye nguvu ya chadema uchaguzi kushindikana pasi hata maelezo shibishi. Angalia Mwanza, Mbeya, Rorya na kwingineko aibu tupu! hii yote inasababishwa na VIJIBABU vya CCM! CCM isifikiri propaganda za amani amani zitaendelea milele itafika sehemu tutasema sasa amani pembeni ila HAKI Kwanza. IT IS STUPIDITY TO HAIL PEACE WHILE OUR RIGHTS ARE TAKEN FROM US by a small GANG!!
   
Loading...