Nimebaini mke wangu amezaa nje ya ndoa na amekiri, naombeni ushauri

Kaka mtu kasema hata yy ni mwanaume hawezi kukubaliana na mke wake kuzaa nje ya ndoa ni bora angefanya mapenzi tu kama kweli alikua amezidiwa ikaisha lkn sio kuzaa nje hiyo ni dharau akanambia nimpeleke kwao

Mama mkwe yy anamtetea mtoto wake ananiuliza wakati anazaa nje wewe ulikua wapi nikakata cmu sikutaka kuendelea kumsikiliza
Tatizo jingine huyu wife analazimisha kua ataondoka ila lazima aondoke na watoto wake wote,
Huyo mama mkwe hafai. Mzuie kuondoka na watoto
 
Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mimi nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kuwa mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti, (mimba ilionekana kubwa)
Pre emptying......hahahaha
 
Pole sana mzee ila wahenga walisema kitanda hakizai kharamu! Usiharibu familia yako haya mambo yapo tangu enzi na kuna jinsi wazee wali-handle haya mambo! Watafute!
Mnahendekeza Ujinga na ndio Maana Miafrika haibadiliki. Kitendo cha kutojali. ustawi na ubora wa familia.

Hizi tabia huwezi kuziona kwa wazungu, wahindi wala warabu.
 
Kisheria unaruhusiwa kumwacha.
Ila kwa Imani ya Kikristo ukimsamehe utapata thawabu zako toka kwa Mungu.
Msamaha ni jambo linalompendeza Mungu.
Hivyo msamehe tu na umlee huyo mtoto.
Kama atajutia na kukuomba msamaha wa dhati.
 
Ushauri kwa wanaosoma huu uzi ni huu hapa chini

KATAA NDOA
narudia tena. .......""""KATAA NDOA""""
 
Mkuu, hiyo isikupe shida sana na kuunyong'onyesha moyo wako. Maisha yenyewe haya ni mafupi angalia usije ukapata shida nyingine katika nafsi yako.

Nimesoma ushauri mbalimbali wa wadau ambao wameeleza hisia zao mbalimbali na baadhi ya wengine wakishauri umwache.

Lakini pia na yeye mkeo hajaonyesha moyo wa kujutia kwa kile alichakifanya, kwa maana hiyo inaonyesha kuwa bado kuna mawasiliano kati yake na huyo mtu wake ambaye wamefanya iwe hivyo.

Kwa hiyo, hata kama ukimuacha na watoto kubaki nao wewe, hata kama wawe kwa ndugu zako bado watakosa malezi ya mama.

Nijuavyo mimi, sisi wanaume tupo busy sana katika utafutaji kwa hiyo inakuwa ni vigumu kuwa karibu na watoto. Hata kama ikitokea utamwacha huyo mwanamke na kuoa mke mwingine bado litakuwa jambo gumu kwa huyo mwanamke kulea wanao vizuri. Mwanzoni anaweza kujionyesha vizuri kuwa atalea lakini mwisho ikawa tena tatizo na kuona kuwa tena ni afadhari ukamrudia tena mkeo wa awali ambaye alikukosea kuliko kadhia ambayo utaipata katika malezi ya mama mwingine kwa watoto wako.

Kwa upande wangu maoni yangu ni kama ifuatavyo:-

Kwanza, kwa sasa huyo mama muache ili aweze kulea familia

Pili, kaa mbali na huyo mama ili asijeleta sababu yoyote kuwa ulimfukuza na kama dhamiri yake inamhukumu atakuja jiengua yeye mwenyewe.

Tatu familia hudumia kama kawaida isipokuwa tendo la ndoa na ikiwezekana unaweza kuwa unatuma matumizi kama kawaida ulivyokuwa unafanya hapo mwanzo.

Hapo itakuepusha wewe kujiingiza katika migogoro isiyokuwa ya lazima na kuendelea kufanya majukumu yako kama kawaida.

Tambua kuwa huyo mama, huna imani naye tena na kama ulikuwa na asilimia 100 sasa zitakuwa 30.

Fanya kwa kuwekeza maeneo mengine kiuchumi kwa ajili yako na watoto na nyumba mliyowekeza wote achana nayo, we jiimarishe maeneo mengine, natumaini wewe ni kijana unajiweza kwa hilo.

Moyo wako upe amani, najua wewe ni kijana utahitaji kutimiza haja zako tafuta mwanamke mwingine wa mahusiano ili kujenga afya ya mwili wako.

Nasisitiza tena, jitenge mbali na huyo mwanamke kushirikiano kimwili ila majukumu mengine ya watoto yatimize kama kawaida na huyo mtoto mwingine chukulia kama analelewa kama mtoto mwingine ambaye sio wako katika familia na mama huyo.

Kwa kumalizia utakuja kunishukuru ataondoka yeye mwenyewe.
 
Sasa ushauri wako ni upi mkuu?
Soma upya ulichokiandika.
 
Mwambie ampeleke kwa babaye wakati akiwa mdogo usikae naye hiyo mtoto kunasiku utamuumiza
Akimpeleka huyo mtoto mwambie na yeye aende hukohuko
 
Broh pole kipindi kigumu sana kama una amani naomba tuliza nafsi na pia fanya kila kitu kutuliza nafsi yako pia zingatia malezi ya watoto wakue vzuri pole sana kaka
 
Naomba niende kwenye mada, mimi na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wa pili mwaka 2018.
Hapo nilipokoleza msisitizo katika andiko lako ndo penye shida.

Wewe ulitakiwa kuoa sio kuoana.

Sasa wanawake ni wataalam sana wa kusoma saikolojia. Alishakusoma toka mwanzo kuwa wewe na yeye mmeoana, na sio kwamba umemuoa.

Kwa kitendo cha wewe kushindwa kumuoa bali kuoana naye ulishindwa kutimiza hitaji la ndani sana la kila mwanamke la kutaka kuolewa.

Ndo maana akaenda kuzaa na mwanaume ambaye inawezekana anamfanya mkeo ajisikie kama ameolewa.
 
Hivi tunaposema KATAA NDOA LINDA MAISHA YAKO tunakaosea au basi
VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE VIJANA MUOE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom