Wanajamii wenzangu habari za mda huu,
Kufuatia tangazo ambalo tulitangaziwa na mwenyekiti wetu bwana alikaeli mbowe kuwa September moja ni siku ya maandamano nchi nzima nilikuwa kwenye maandalizi ya kuandamana lakin ntaomba mnisamehe SITAFANYA MAANDAMANO HAYO.
Sababu kuu za kunifanya nisiandamane ni hizi
1. Amani ya nchi Yetu, nimefuatilia nchi kadhaa zilizoitisha maandamano yasiyo na kikomo, zimejikuta hazipati kile zilichotegemea matokeo yake imekuwa ni machafuko ya kupinduana kila Mara na watu wamekuwa wakimbizi wa nchi zao,
2. Pili maandalizi ya September 1 yameingiliwa na JWTZ jambo ambalo ni hatari zaidi , chezea kwa kamanda sirro lakin si kwa mwamunyange, yaan hujui kusoma hata picha huoni kuwa huyu ni mbuzi Huyo ni kondoo,? Kujitolea kwa wanajeshi kufanya usafi we upite na mabango yako unaleta FYOKOFYOKO zako na unachafua tena haisee ,patella will be dislocated in your body system , ni bora ni kakaa nyumbani kwangu tu,
3. Majukumu yanayonikabili,
Majukumu niliyonayo kikazi ni mengi sana, kuna familia na kusomesha watoto, Nina wategemezi kibao, Nina mipango mingi sana mbeleni sioni sababu ya kufupisha maisha yangu kisa namsaidia LOWASSA na MBOWE kutimiza azima zao,
NOTE THAT ikitokea nikafa kama mwangosi, au alphonce mawazo , nitaishia kutumika kwenye kumbukumbu za kuleta umaarufu wa chama lakin Ipo Siku wana chadema watanisahau na kutelekeza familia yangu,
4. Tuheshimu katiba ya nchi Yetu, ambayo kuna majukumu na wajibu wa raia, ikiwemo kutii sheria na amri za wakubwa akiwemo mkuu wa nchi ambaye kimaandishi hayuko juu ya sheria lakin kiuhalisia neno lake lolote ni sheria, sipaswi kupingana naye , ****** wengi kama 30% ya watanzania wanaonekan kumpinga lakin ndiyo rais, hata angepingwa na 90% lakin ameshakuwa rais wetu.
5. Tukio la Jana kati ya lowassa na Mheshimiwa rais limenionesha kuwa Wenda hawa wakubwa wanaelewana vizuri tu ila sisi ndiyo madaraja ya kufikia malengo yao, hivyo naamini IPO Siku moja ntakuwa katika ngazi fulan kuwatetea wananchi kwa moyo wa dhati hivyo sipaswi kufupisha maisha yangu kwa kuwa daraja la wengine,
NB: ukizingatia mzee mkapa ndo alimkata Lowassa baada ya wengine kuwa na kigugumizi July 11 , 2015, lakin Lowassa hakujali hayo kaenda kwenye jubilee yake , siasa si uadui,
6. Muda wa Magufuli madarakani ni mfupi mno kulipo uwepo wa Tanzania, mh Magufuli hawez kuongoza nchi zaidi ya mwaka 2026, hivyo ngoja tumvumilie tu kama tulivyo wavumilia wengine na madhaifu yao, na huyu mheshimiwa tumvumilue tu muda wake utapita na watanzania watakuwa wameshapata mwamko zaidi juu ya nini wanakitaka toka kwa kiongozi anayechaguliwa ,na watakuwa na uwezo wa kupima ,
7. Matamko ya viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, matamko ya viongozi wa dini , wawakilishi wa mungu hapa dunian wametuasa tusifanye maandamano na si vema kuandamana wakati viongozi wenye maono ya mungu wametuhasa na wanayajua madhara yake,
8. Mimi kama mtanzania niwe mkweli sitaki demokrasia ila nataka wanangu wale washibe, wasome bule, nikitaka kusafiri ndani na nje ya nchi usafiri uwepo, nataka ulinzi, matibabu, maji safi, barabara, umeme, Uhuru wa kutembea bila kukabwa na majambazi, kuongezeka kwa kipato changu, kupata Huduma kwa haraka bila urasimu, sipendi mazingira ya rushwa yaendelee kuweko, nataka Huduma bora,bei ya vitu ishuke, ila sitaki demokrasia alafu nkayakosa hayo. Hivyo ikitokea Magufuli akaninyima nilivyotaja hapo juu naomba nishirikishwe maandamani yasiyo na kikomo, hapa sitamsikiliza yeyote,
9. Familia yangu na ukoo tupo watu 67 kuanzia baba, baba Mdogo, mama , na mama wadogo na watoto wao, kwa tafiti ndogo niliyofanya wapo wafuasi wa CCM 21 CHADEMA 23, TLP 2 na wengine hawana vyama, nkajiuliza tukiingia barabarani kupingana na kurushiana mawe kumbe kuna uwezekano ukakuta namtupia mzee jiwe la kisogo, naomba Mungu aepushe hiki kukombe,
Hizo ndizo sababu zangu za msingi zilizonifanya kubadili maamuzi ya kuandaman,