Nimebadili gia angani, nitahamia Kanda ya Ziwa!

Nimebadili gia angani, nitahamia Kanda ya Ziwa!

Ukiwa mtanzania, unapaswa kwenda na 'beats'. Unapaswa kubadilikabadilika kulingana na muziki unaopigwa. Unapaswa kutazama viongozi wanasema au kufanya nini na kwanini nawe unaelekea huko. Hakuna namna nyingine!

Wakati wa kauli tamutamu na za mfululizo kuhusu kuhamia Dodoma, nilitangaza kuhamia huko:Natangaza kuhamia Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Lakini, muziki huo umeshazimwa na DJ.

Sasa unapigwa muziki wa Kanda ya Ziwa. Wa huko wanasikilizwa; wanatetewa; wanatazamwa kwa umakini na kadhalika. Wa huko 'wanaambiwa ukweli'; wanajengewa miundombinu ya kila msimu na wanategemewa mwaka 2020.

Kwa muziki unaopigwa sasa, nimeamua kubadili gia angani. Nitahamia Kanda ya Ziwa badala ya Dodoma. Mambo yote yapo Mwanza, Geita, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Mara.

Mwafaaaaaaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kwani kanda ya ZIWA kutoa Rais ni DHAMBI kubwa sana?
Kwani watu wa huko HAWASTAHILI mema YEYOTE?
 
Huu ni uchochezi aisee, wewe toa hoja kwa mifano. Maana kanda ya ziwa ni kubwa na hata ungesema Mara bado unazungumuza kitu kikubwa sana. Wewe tuambie tu hayo yaliyofanywa MARA, MWANZA, KAGERA,GEITA,SIMIYU NA SHINYANGA ambayo hayajafanywa kingine ndani ya mwaka moja wa Rais. Acheni uchonganishi na kupalilia ukanda na udini jamani.
 
Hhaahhaa Happy New Year Mpwa, twende zetu kwenye Traffic light za Ng'ombe
Hahahahah, happy new year kwako pia..... Yaani kuna sehemu hizo taa zinahitajika sana kwa matumizi ya watu wengine wanaweka kwa matumizi ya ng'ombe?
 
Du ...
Siasa za Tz ni ujinga, fitna na majungu tu. Hivi Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kagera kuna upendeleo gani wamepewa hadi mnawatia majungu hivi, hivi hizi 4 lanes za highway zinazojengwa Arusha zingejengwa Mwanza-Mara kweli kungekuwa na amani ? Achane unafiki, siasa za kikanda hazitawapa Ikulu.
 
Nimebaki nashangaa tu...
 
Back
Top Bottom