VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ukiwa mtanzania, unapaswa kwenda na 'beats'. Unapaswa kubadilikabadilika kulingana na muziki unaopigwa. Unapaswa kutazama viongozi wanasema au kufanya nini na kwanini nawe unaelekea huko. Hakuna namna nyingine!
Wakati wa kauli tamutamu na za mfululizo kuhusu kuhamia Dodoma, nilitangaza kuhamia huko:Natangaza kuhamia Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Lakini, muziki huo umeshazimwa na DJ.
Sasa unapigwa muziki wa Kanda ya Ziwa. Wa huko wanasikilizwa; wanatetewa; wanatazamwa kwa umakini na kadhalika. Wa huko 'wanaambiwa ukweli'; wanajengewa miundombinu ya kila msimu na wanategemewa mwaka 2020.
Kwa muziki unaopigwa sasa, nimeamua kubadili gia angani. Nitahamia Kanda ya Ziwa badala ya Dodoma. Mambo yote yapo Mwanza, Geita, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Mara.
Mwafaaaaaaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam