Nimeanza kusoma kitabu cha Kusadikika

Nimeanza kusoma kitabu cha Kusadikika

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,116
Reaction score
5,119
Wana jamvi,
Nimeanza kusoma kitabu cha Marehemu Shaban Robert kiitwacho kusadikika.
Ninakisoma kwa speed ndogo ili nielewe vizuri maudhui yake.
Naomba mlio nacho mniunge mkono.
 
ndio umekipata hivi karibuni...!?
nilikinunua muda kiasi lakini sasa ndio nimepata wasaa wa kukisoma.
Nahisi naweza kukimaliza kwa siku moja lakini naona niende polepole kwani inawezekana kukawa na falsafa nzito ndani yake na ndio maana nimewaalika wana jamvi twende pamoja.
 
sawa, changu niliibiwa, ukimaliza itabidi uniazime ndugu...
 
Wana jamvi,
Nimeanza kusoma kitabu cha Marehemu Shaban Robert kiitwacho kusadikika.
Ninakisoma kwa speed ndogo ili nielewe vizuri maudhui yake.
Naomba mlio nacho mniunge mkono.
Hicho kitabu kinaeleza yote kuhusu Tanzania. Angalia tume mbali mbali zilizoundwa kwa gharama kubwa sana na kisha kudharauliwa kwa mapendekekezo waliyoyaleta.
 
dah watu mnapenda vya kale, mimi nakitafuta kitabu cha BULICHEKA, hicho tu ndo hamu yangu ya kukipata\
 
Mwenye soft copy atuwekee jamani nasi tufaidi yaliyomo
 
Nilikisoma nikiwa kidato cha pili. Nadhani hapa Kenya kilitahiniwa katika mtihani wa kidato cha nne mwaka wa 1994, pamoja na Mashetani, Kinjeketili, na Shambal La Wanyama.
 
Back
Top Bottom