Nimeamua, sitapiga kura tena!

Si hutaki kupiga kura we acha tu tutakupigia na kukuchagulia viongozi, kelele za nini?
Kelele ni kwa sababu wananipigiaga kelele ati nikapige kura. ...Tume ya Uchaguzi wananipigiaga kelele, Vyama vya siasa vinanipigiaga kelele.....serikali nayo hunipigiaga kelele nikapige kura...ndio maana nami narudishia kelele kuwa wasinisumbue, SITAPIGA KURA TENA!

Vv
 
Wanakukumbusha tu umchaguzi tayari, kupiga au kutopiga ni wewe na nafsi yako, tupo usipochagua tutakuchagulia hakuna nafasi tupu lazima ijazwe
 
Wanakukumbusha tu umchaguzi tayari, kupiga au kutopiga ni wewe na nafsi yako, tupo usipochagua tutakuchagulia hakuna nafasi tupu lazima ijazwe
Wanithibitishie kwa vitendo kuwa kura zetu zinaamua kweli? Wewe hujiulizi? Hushangai kuwa karibu asilimia 60 na zaidi hawapigi tena kura? Sasa kama asilimia zaidi ya 60 hawapigi kura, sio upotevu wa fedha ambazo zingejazia madawa na vifaa tiba mahospitalini au wanafunzi wengi zaidi wa elimu ya juu wangepata mikopo na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu?

Vv
 
Watu hawashurutishwi kupiga kura ila hukumbushwa tu sasa ni kupiga kura!
Hilo lina mantiki iwapo kura yangu na muda wangu naoutumia kwenye kujiandikisha na kupiga kura unathaminiwa. Sitapiga kura zinazohusisha kumwaga damu za watu, Sitapiga kura tena, hadi nione thamani ya kura yangu, hafi nione thamani ya maisha ya wapiga kura na wasiopiga kura, hadi nione thamani ya kura yangu. Siko tayari kuona kura yangu inahusishwa na umwagaji wa damu, ima kutoka kwa polisi au vyama vya siasa.

Vv

Vv
 
Back
Top Bottom