Nimeamua kuuza figo yangu moja ya kulia ili kulipa deni la loan board

Wewe unaishi nje ya nchi????

Watu wanauza damu kwa biskuti na sodaa
Hahahahahaha na wakija hua wanasema tuuzie damu na gharama ni biskuti na soda? No, na hua wanasema changia damu okoa maisha, siyo uza damu okoa maisha.
 
Ndg zangu habari zenu, mm mhitimu wa chuo kikuu niliyesoma masomo ya arts na kuambiwa sitopewa ajira huku nikidaiwa pesa na loan board zipatazo milioni 15 nimeamua kuuza figo yangu ya kulia ili nilipe deni hilo

Figo hiyo nimepata mteja anataka kunipa milioni 30

Ushauri wenu ndg zangu vipi niuze hiyo figo ili nilipe deni???
Ulishaamua tukusaidie je?
 
Jiangalie Wakati Wakampe Mlikua Mkishangilia Mtuakipiga Pushapu Sasa Mnapigishwa nyie Ukisha uza Badae Utauza nini
 
Sasa mkuu umekoswa njia zote za kutafta pesa umeona kuuza figo ndyo suruhisho inamaana kusoma kote huko lengo uajiliwe imekosekana ajira umeona ujikaange mwenyewe kwa mafta yako,pambana achana na mawazo finyu tena msomi,Elimu mnaishusha kabisa kwa mwendo huu
 
Duh nimekumbuka andiko moja kwenye Biblia linasema ni heri kuingia katika Ufalme wa Mungu na mguu mmoja kuliko kwenda jehanam na miguu yote.
 
Ndg zangu habari zenu, mm mhitimu wa chuo kikuu niliyesoma masomo ya arts na kuambiwa sitopewa ajira huku nikidaiwa pesa na loan board zipatazo milioni 15 nimeamua kuuza figo yangu ya kulia ili nilipe deni hilo

Figo hiyo nimepata mteja anataka kunipa milioni 30

Ushauri wenu ndg zangu vipi niuze hiyo figo ili nilipe deni???
acha uongo wewe sheria ya board inataka ulipe deni mwaka mmoja baada ya kupata ajira
 
Uza tu kimfaacho mtu chake... na uo mkopo umekosea kusoma jinsi ya kuulipa... kausome teena vizuuri afu ndo utunge hadithi... usijari utakuwa tu maarufu JF.. kitu rahisi saana... katunge vizuri.
 
Usimdanganye. Mungu alipotuumba na figo mbili usidhani kuwa alikuwa mjinga. Ukiwa na figo moja den ikafail utafanyaje?
wewe una tatizo la elimu kwaiyo kila alichoumba Mungu mwilini kina umuhimu basi niambie umuhimu wa kidole tumbo, binadamu anaishi na figo moja bila tatizo lolote.
 
Asante lakini aliyeweka Figo moja sio punguani...na pengine hujui vema tafsiri ya ulemavu
Mkuu kuna watu wanazaliwa na figo moja na kuna watu wanazaliwa na figo tatu, ueelewa wa figo kwa watanzania upo chini sana hata uwe na figo 10 haumzidi mwenye figo moja ikifika muda wa kufeli figo zinafeli kwa pamoja nina uelewa sana wa figo mkuu sikubishii bure.
 
Yaani nimefurahi mno. Umekosa kazi mda mrefu, ukaja na idea yako hii ya namna ya kupata mtaji sio?? Yaani, ni wewe pekee tz hii uliyekopeshwa hiyo pesa?? Au ni wewe pekee tu umebaki unadaiwa na hiyo serekali?? Kama woote wataamua kuuza hizo figo zao, wadhani tz tutakuwa na vilema wangapi??
Nenda kauze, ulipe deni ili serekali iwasamehe hao wengine kwa dhabihu yako.
 
Uza tu Figo ila jua matatizo hayadumu yakiisha utatamani hata Figo ya plastic na usipate
 
Kila la kheri Mkuu ila tambua kuuza figo ni kosa kisheria. Pili,afya yako itahitaji uangalizi wa hali ya Juu baada ya kuondoa Figo moja. Tatu,kuwa makini sana usije kutapeliwa figo yako,figo unatoa na hela hupati.

Mimi nakushauri umuombe Mungu na kazi utapata na harakati za kulipa hilo deni zitaanza tu. Mambo ya kuchezea maisha kwa sababu ya Million 30 siyo kiyu cha mchezo.

Mbona wengine tuna madeni ya Million 100 lakini tunapambana tu hivyo hivyo?
Mkuu umesikia wadaiwa wa bodi wamepewa masharti gan? Hawatoki nje ya nchi, nk, namshauri auze tuuu
 
Back
Top Bottom