Nimeamua kujiunga na CCM

Huu ni unafiki tu, yaani uamuzi wako wa kujiunga na CCM nao ni mada ya kujadiliwa? Kama una mapenzi ya dhati na CCM ungejiunga nao kimya kimya. Unatutangazia ili tuamini kwamba CCM bado inaungwa mkono na Watanzania? Waacheni ambao hawakufanikiwa kuunda serikali waseme, mlio serikalini fanyeni kazi, vitendo vionekane, ndipo wananchi watawakubali. Kama unafanya kazi, wananchi wataona, huhitaji kuwatangazia wananchi kwamba unafanya kazi.
 
Na mimi napata hisia kumbe vijana kweli ni tatizo katika kuona mbele. Ndiyo hawa wanaoleta thread tasa humu na wale wanaogombana kule Bavicha. They are one and the same.

Ni vijana wa ccm. vijana wa CHADEMA bado hawajawa misukule kama hawa wa magamba.
 

Rais kuruhusu uhuru wa maoni sio zawadi, ni wajibu-anatekeleza katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.

Uhuru wa kutoa maoni huko tuendako hauepukiki-mfano mtu anawezaje kuzuia uhuru wa kutoa maoni ktk social networks kama facebook? Lakini pia Rais wetu ni beneficially wa uhuru wa kutoa maoni.

Moja ya sababu ya kushinda kwa kishindo 2005 ni kuandikwa vizuri na vyombo vya habari wakati wagombea wenzake walikuwa wamebanwa kweli kweli. Hawezi kuuuma mkono unaomlisha. Sio dhambi kumkosoa Rais, maana amechaguliwa na wananchi ili awatumikie.
 
ukiamua kujiunga huna haja ya kutujulisha sisi ,upeo wako ndo umefikia hapo, pole
 
ondoa ujinga wako unasumbul4wa na elimu ndogo ya uraia hata hujui maana ya mfum6 wa vyama vingi nyie ndo mnapigwa mawe acha mawazo ya ukasuku na ulamba viatu be a man ie. Kuwa mwanaume

As if you yourself are a man enough! You wouldn't allow to be mentally enslaved by Slaa and his coterrie! You will at some stage require an emancipation in order to restore your manhood !
 
Hakuna asiyejua kwamba hiyo ni constitutional right. Lakini ni katiba ngapi zinatoa haki za msingi (bill of rights ) lakini viongozi walioko madarakani wanaamua kuzikalia hizo haki.

Ndo maana nimekupa mfano wa katiba ya Uganda ambayo iko more elaborate kuliko yetu, lakini muulize Kizza Besigye kama ameweza kuzi-enforce hizo haki zake. Kwa hiyo ni lazima uelewe kwamba kukubali kuzitekeleza hizo haki ni suala la utashi na uungwana wa mkuu wa dola.

Rais wetu ni democrat anayeruhusu watu kufikia hatua hata ya kuingilia staha yake na familia yake wakati hata huko CDM kuna watu wakimkosoa mwenyekiti tu tayari wako matatizoni. Muulize Kafulila!
 
Uamuzi wako ni kwenda CCM ni wako maana hatujui ulikuwa wapi. Nadhani unaenda kufua magamba! Hujui kabisa misingi ya Demokrasia. Demokrasia inasimama juu ya uwazi, uwajibikaji na kupinga ufisadi. CCM hakuna demokrasia hivyo nenda tu ukaendeleze unafiki wa ccm.
 

Hahahahaha, nina mashaka na maelezo yako. Kama wakishughulika kiyakinifu na hili moja la MAFISADI nitajua kweli wanakubali kukosolewa. Na hivyo wengi tutajiunga tena.
 
Nenda salama maana huoni mbali unanikumbusha 1947
 
Tumaini Letu,

Mbona umechelewa wakati nawe u-gamba la kuvuliwa
 
unajua waweza kumtambua mtu hata kwa maandishi tu.....hao wanaojiunga na chama cha magamba eti kwa sababu tu ****** mvumilivu......mmmmmh ninashaka na IQ ya hao watu !!!!!!!!! umaskini,ufisadi,rushwa na mambo yooote yanayoondelea bado kikwete anafaaa,,,,,hongereni sana nadhani kuna jambo siwezi kushangaa hata mchawi ana wapambe wake
 

Kwa akili zako hizo, mbona umechelewa sana kubaini kuwa ccm ndipo mahali pako muafaka!!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa pamoja na mapungufu makubwa ya JK kiuongozi, bado ni kiongozi aliyethubutu kuruhusu watu kujadili na kutoa maoni yao kwa uhuru zaidi, kuliko kipindi cha mkapa.

Lakini unapozungumzia chama kama ccm, binafsi nisiye na chama, ccm hakina mvuto tena na wananchi wengi wanaelewa hilo, CDM kinakubalika ni jambo lililowazi. CCM wamekubali kukosolewa kwa sababu CDM wanatoa hoja ambazo ccm hawawezi kuzipinga na kubwa zaidi wao wenyewe wamegawanyika na makundi yao.

Hivyo mtu kuhamia ccm ni uhuru wake kikatiba lakini LOGIC ya kuhamia kwa sasa siioni.
 
Uhuru wa umaskini wewe vipi ? Rais gani hajui alifanyalo? Angalia Burundi na Rwanda chumi zao zivyopaa kwa kasi pamoja na mataizo waliyapata, tatizo la wenye akili kama zako waoafikiri haki ya uhuru ni hisani ya mtu fulani hiyo hata mbiguni haipo, uhuru ni haki ya kila mtu kama ilivyo haki hupiganiwa ndivyo pia na uhuru.
 
Naamini kuwa wanaoipenda ccm na kikwete sio watanzania......
 
nimewahi soma mahali....."IF YOU CANT WIN THEM....JOIN THEM" and my teacher asked the group of boycotting students
"CAN YOU WAGE A WAR THAT YOU ARE GOING TO LOSE?" Nikumbukacho waliokuwa na masikio walisikia ...na waliokuwa "mashujaa" walisonga
 
nimewahi soma mahali....."IF YOU CANT WIN THEM....JOIN THEM" and my teacher asked the group of boycotting students
"CAN YOU WAGE A WAR THAT YOU ARE GOING TO LOSE?" Nikumbukacho waliokuwa na masikio walisikia ...na waliokuwa "mashujaa" walisonga

Hapo kweye RED ni vizuri maneno yako yangeendana na vitendo, kwa kuwa tumeshindwa vita ya kukomesha ushoga Tanzania, basi usichelewe ungana nao uanze kupakuliwa na wewe.
 

Usiku mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…